Hata Shetani likizeeka linakuwa malaika

Shantel

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
2,018
1,129
Wakuu embu tujadili huu msemo, kuna mdada wa makamo alikuwa anasumulia jinsi alivyotoka mbali na
Mumewe, na jinsi alivyoteswa na huyo mume kiasi cha kuondoka home kwa mda wa mwaka na kwenda
kuishi na mwanamke mwingine

Baada ya mwaka huo akarudi akaomba msamaha kwa mkewe, wakabariki na ndoa maisha yakaendelea
ila uhuni ukaendelea kama kawaida, mara harudi kwake hata siku tatu, mke akaamua kuvumilia tu
sasa imepita miaka kibao na wana watoto watano, yule mwanaume kabadilika amekuwa yeye wa kumfata
mkewe hata salon na kumsubiria nje mpaka amalize, ofisini anaweza enda msubiria kuanzia saa tisa yuko
nje mpaka saa kumi na nusu......

Tatizo linakuja yule dada alishakufa ganzi moyo akawa anaishi maisha yake, wakati mume sasa hivi ndio
anajifanya kumuhitaji kuliko kitu chochote kile, ndio mwisho wa maongezi mdada mwingine akaibuka na huu
msemo eti hata shatani akizeeka anakuwa malaika.......Eti wakuu mnakubaliana na huo msemo???

Nawakilisha
 
Yaaani simba mzee yeye huwa anasubiria jike limkamatie nyama ndio lile, na wakati mwingine linakula mizoga, huyo mumewe pengine amerealize alichokuwa anafanya na ametubu na sasa anajutia matendo yake ya nyuma kwa hiyo kulipiza anaona amuenzi mkewe, ila huyo mdada sipande kichwa siku likijua maduka ya viagra atajuta, mwambie amsamehe kama yeye anajua dini, waishi kwa amani
 
Shetani akizeeka anastaafu lakini ushetani hauishi (the state being shetani remains). Anaacha kufanya kazi yake ya ushetani, labda ushetani wa kujitolea na si wa kipato wala mshahara. Anaendelea kufaidi pension yake kama kawaida kwa sababu ni retired shetani.

Shetani anayebadilika kuwa malaika ni yule aliyepitia kwenye mchakato wa "metamorphosis".
 
Duuu!
Noana kazunguka mpaka kachoka ameamua arudi kwa mke wake, huyo dada asamehe na amuombe mungu mme wake asijebadilika tena waishi maisha ya amani na upendo
 
watu hubadilika wakiwa na sababu za kufanya hivyo,inawezekana kabisa akziacha njia zake mbaya kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo!
 
Wakuu embu tujadili huu msemo, kuna mdada wa makamo alikuwa anasumulia jinsi alivyotoka mbali na
Mumewe, na jinsi alivyoteswa na huyo mume kiasi cha kuondoka home kwa mda wa mwaka na kwenda
kuishi na mwanamke mwingine

Baada ya mwaka huo akarudi akaomba msamaha kwa mkewe, wakabariki na ndoa maisha yakaendelea
ila uhuni ukaendelea kama kawaida, mara harudi kwake hata siku tatu, mke akaamua kuvumilia tu
sasa imepita miaka kibao na wana watoto watano, yule mwanaume kabadilika amekuwa yeye wa kumfata
mkewe hata salon na kumsubiria nje mpaka amalize, ofisini anaweza enda msubiria kuanzia saa tisa yuko
nje mpaka saa kumi na nusu......

Tatizo linakuja yule dada alishakufa ganzi moyo akawa anaishi maisha yake, wakati mume sasa hivi ndio
anajifanya kumuhitaji kuliko kitu chochote kile, ndio mwisho wa maongezi mdada mwingine akaibuka na huu
msemo eti hata shatani akizeeka anakuwa malaika.......Eti wakuu mnakubaliana na huo msemo???

Nawakilisha

Hapana shetani ni shetani wala muda hauwezi kumbadilisha. Ila kwa ishu ya huyo mbaba inawezekana amebadilika tu na ameona sio vyema kuendelea kumtesa mke wake na amejirudi kwa nafsi yake na kurudisha majeshi nyumbani. Mke kama vipi amsamehe mume wake na waendelee na maisha.
 
Ni kweli yawezekana huyo baba amebadilika maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ila pia kwa ushauri tuu, kama walikuwa hawapo wote kindoa ni bora wakapime kwanza ndo waendelee na maisha. Wanaume bwana, anaweza kujua anaumwa then akaja kumuua dada wa watu. Ni hayo tu.
 
Kama nimesoma vizuri, huyu bwana sio kwamba kabadilika - watoto ndo wanamtaiti. Siku akipata upenyo atatembea tu. Kunguru hafugiki ndg zangu tambueni hilo.
 
Mkewe kamsamehe ila ku corp na hali ya sasa anashindwa, yaani mbanano, alishazoea hata simu hapigiwi, wala haulizwi yuko wapi, na yeye alimfatilia mumewe akashindwa hivo akawa hamuulizi kabisa hata asiporudi home...ndio hivyo tena jamaa kajirudi kawa anajali
 
Kama nimesoma vizuri, huyu bwana sio kwamba kabadilika - watoto ndo wanamtaiti. Siku akipata upenyo atatembea tu. Kunguru hafugiki ndg zangu tambueni hilo.
Kama ni watoto basi asingekuwa anamfata nyuma mkewe kihivi, kilichofanya asimulie na mimi nikiwepo alimfata dada angu pale mlimani city tukawa wadada kama watano hivi ikabidi yule baba akakae pembeni amsubiri mkewe, wale wadada wakawa wanamshangaa ni huyuhuyu au mwingine, maana wanamjua shemeji yao
 
Ni kweli yawezekana huyo baba amebadilika maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Ila pia kwa ushauri tuu, kama walikuwa hawapo wote kindoa ni bora wakapime kwanza ndo waendelee na maisha. Wanaume bwana, anaweza kujua anaumwa then akaja kumuua dada wa watu. Ni hayo tu.
Kweli Mungu ni mkubwa mtu wa kuhama nyumba na kulala nje leo kawa hivi
 
Hapana shetani ni shetani wala muda hauwezi kumbadilisha. Ila kwa ishu ya huyo mbaba inawezekana amebadilika tu na ameona sio vyema kuendelea kumtesa mke wake na amejirudi kwa nafsi yake na kurudisha majeshi nyumbani. Mke kama vipi amsamehe mume wake na waendelee na maisha.
Mbona malaika anaweza kuwa shetani?
 
watu hubadilika wakiwa na sababu za kufanya hivyo,inawezekana kabisa akziacha njia zake mbaya kwa msaada wa Mungu asiyeshindwa jambo!
Kuna mwinginekamshauri wakapime labda kaukanyaga maana wazee wakishakanyaga wanatulia ili wauguzwe vizuri
 
Kweli Mungu ni mkubwa mtu wa kuhama nyumba na kulala nje leo kawa hivi

Unajua jamii huwa inapamba maneno. Inawezekana alihama kwa sababu ya maudhi ya mkewe. Tatizo la wanawake huwa warahisi kuongea ila sisi wanaume huwa warahisi wa kutenda. Wiffe akinikosea sina haja ya kumtangaza ... ni ku-take action tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom