Hata nyumba za ibada zinakelele za kukera sawa na kumbi za starehe

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,017
9,885
NEMC wanafanya vizuri kwenye hili la kutusaidia kupunguza kelele mitaani ila yapo mengi Zaidi ya kufanya ili kutupunguzia kelele ambazo zimekuwa kero

Kwanza itambulike naheshimu uhuru wa kila mtu, na nasema wazi kuwa ni jambo muhimu mtu kutumika uhuru wake kusikiliza chohote anachotaka, japokuwa kelele za mtu zisiathiri shughuli za mtu mwingine (Externality)

Hapo ndio pa kujua kuwa kelele zinasababishwa na vitu mbalimbali, ikiwemo, Vyombo vya moto, Nyumba za ibada na kumbi za starehe. Hivyo muongozo wa kelele uende kwa wote, mathalani, mimi natamani kuwa na muda mwingi wa utulivu ili kufanya tafiti zangu, hivyo kelele za starehe zinaniathiri sawa na kelele za ibada.

Kuwe na muongozo wa kutumika vidhibiti sauti kwa wote kwa nyumba za ibada na kumbi za starehe. Aidha kwa wanaoagiza magari, magari yenye kelele kidogo yapewe punguzo la kodi ili kufanya yawe mengi nchini.

Suala la kelele linakera kwa ndugu zangu wa din izote, wanaokesha au wanaoamka asubuhi na kusumbua kwa kelele zao, similary hawa watu wastarehe.

Na kwa watu was tarehe, ikibidi yatengwe maeneo maalumu ya recreation ili kila mmoja aendelee kufurahia uhuru wake bila kuathiri wengi.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom