Jamani, ninaomba muelewe kwa makini kuwa, "Kinachomfanya Nape Nnauye Ale, Avae, Alale, ni maneno ya mdomo wake na mara nyingi maneno ambayo hata yeye mwenyewe hayaamini ila akishatumwa aseme hivyo, hana budi ya kutekeleza".
Muoneeni huruma kijana mwenzetu! Siku moja ataokoka na atajivua Gamba tu....!
Lakini kumbukeni ya kwamba, hata KANU ilipokaribia kunyang'anywa madaraka nchini Kenya, "Viongozi wao, Mpaka Dakika ya Mwisho walisema, KANU hakiwezi kuangushwa na vyama kama, PNU na Vingine". Je KANU leo hii kipo madarakani?
Bwana Muhammad Saeed al-Sahhaf, Aliyekuwa Waziri wa Habari na Msemaji wa Serikali ya Aliyekuwa Raisi wa Irak, Marehemu Saddam Hussein walipovamia na majeshi ya Kimarekani, Uingereza, na NATO, hata nusu saa kabla hajakamatwa,alipiga propaganda kuwa, "...Karibu Jeshi la Irak linashinda vita ile..." Je maneno yake yalikuwa ya kweli? Walipigwa hawajapigwa?
Jamani mfa maji, Haaachi.....!
Kaka endelea kula mshahara, endeleza propaganda wasikufukuze kazi...!