Hata kama una haki....

Yuko mmoja anayedai anahaki ya kufanya mikutano ya siasa kokote na wakati wowote. Binafsi sijapata kuona mropokaji kama yeye.

Wewe mleta mada, sijui haya maneno ni ya kwako au ya 'nyani' (sisiem) anayemkejeli mwenye shamba (wananchi) baada ya kuiba mali ya umma kwa miaka zaidi ya hamsini (ikiwemo ile ya tanu na eiespi)?

Huyu 'mtukufu' kati ya miungu ya ya kufikirika, eti yeye yuko juu ya sheria na katiba ya nchi na ana haki ya kutukana au kukejeli yeyote huku akishangiliwa na wengi waliojitoa ufahamu kama wewe! Kuwa mkuu hakumpi haki mtu yeyote kudharau wengine na huyu 'mtukufu' is only human in blood, flesh and souls, no different to you and I. 'kinyago tulichochonga' wenyewe chapata wapi haki ya kuwadharau waliokichonga?

Iko siku wewe utamzomea huyu mtu. Yaani hii mada yako inamhusu huyo mtukufu siyo TAL. Think again GT!
 
Naam, hata yeye huu ujumbe unamhusu.
Kama unamuhusu kwanini na yeye hujamjumuisha hapo? Au kuweka picha yake?
Mkapa alaita watu wapumbavu na malofa, mbona hukutema hilo povu lako?

We jamaa siku hizi umekuwa na akili kama jingalao.
 
Ni kweli Tundu Lissu anatumia lugha kali. lakini unaweza kuona kwamba mtu kama huyu anasikika sana hivi sasa kwa sababu ya aina ya utawala uliopo. watu kama hawa wapo tu, na wana haki ya kuwepo kama wewe na mimi. kama vile wewe una haki ya kumkosoa Tundu Lissu, yeye pia na wengine, wana haki ya kuwakosoa walio kwenye mamlaka, hasa kama hao wenye mamlaka wanaonesha dalili za u-mungu-mtu
 
Huyo Mkurya Mwita Waitara bado tu ana ambatana na mtu aliye wakejeli wana Mara kuwa wanapendelewa
 
Sasa tupo awamu ya tano.

Nina yupi Rais msema hovyo asiye na staha katika wote watano?

Nani anaongoza kuomba kuombewa?

Kwa sababu gani aombewe?
Hayo yaliyofanyika kukabiliana na kuchukua hatua dhidi ya wahalifu kutoka hewa kila mahali hadi rushwa kubwa zilizokuwa zimewekwa kapuni..wewe ungeweza??? waliomtangulia kwa nini walishindwa..sifa muhimu ya serikali yoyote ni kuwa powerful!!! madaraka si kufanya watu wacheke kijana..
 
Kama ana haki na anaitumia vibaya,si mshinde kesi na kumfunga?
Kama anawashinda mahakamani ujue anaitumia vema haki yake.
Halafu kati ya waropokaji wakubwa nchi hii,Lissu anamfikia huyo "mkuu wenu" wa na katerero!?
 
Kama anafanya yaliyo sahihi, wasiwasi wa nini?

Hao "wanyonge" wanaonufaika na kazi zake watamuombea bila kuwaomba.

Wapinzani wanamzuia vipi kutimiza wajibu wake? Mafisadi wapo upinzani au CCM?
 
Kweli kabisa...

Sidhani kama hizo sheria ambazo Lissu anasema zinalinda uhuru wa kukosoa hazina mipaka kwa kulinda pia haki za yule anayekosolewa.

Kwa kifupi hakuna uhuru bila mipaka. Yaani hakuna kupayuka kusiko na ukomo. Nchii hii ni yeti sote ila wengine ni maadui wa ndani ya taifa letu. Watatumia uzalendo na uzawa kupromote ujinga kama anavyofanya Lissi ila kumbe wanatumiwa kuangamiza taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini si tunaambiwa anapendelea kanda ya ziwa? Iweje sasa aliwatukana na kuwadhulumu pesa zenu mlizochangiwa na Watanzania?
Akitaka hata aweke ukoo wake wote sawa tu (Hayanihusu hata chembe): Hizi tabia siyo ngeni kwenye siasa za Tanzani. Ila kinachonihusu mimi ni kwamba Magufuli alitutukana matusi makubwa sisi Wahaya na kutufanyia dhuluma kwenye haki zetu na hilo (Rest Assured) litakuja kumgharimu siku si nyingi.
 
Kama ana haki na anaitumia vibaya,si mshinde kesi na kumfunga?
Kama anawashinda mahakamani ujue anaitumia vema haki yake.
Halafu kati ya waropokaji wakubwa nchi hii,Lissu anamfikia huyo "mkuu wenu" wa na katerero!?
Akifungwa mtasema kaonewa.
 
Mbona wewe umeropoka hapa? Unataka kujimilikisha "haki" ya kuropoka? Kuusema ukweli ambao unaaminiwa na wengine, hata kama wewe huuamini, haiwezi kuwa ni kuropoka! TL na wengine wanatatizwa na mkuu wa nchi kuteua mtoto wa dada yake ndiye awe Mlipaji Mkuu wa serikali, na amekuwa akifanya malipo kwa kushauriana tu na mjomba wake bila kufuata taratibu za ulipaji. Lisu amekemea hili, kama kwako ni sawa tu, basi baki na mtazamo huo, lakini Lisu hajaropoka bali ameusema ukweli ambao unaaminiwa na wengi, hata kama wewe sio mingoni mwao.

Lisu ameeleza ukweli, kwamba: mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi, mwendesha mashitaka wa serikali, mwanasheria mkuu wa serikali, kaimu jaji mkuu, mkuu wa usalama wa taifa-hawa wote wanatoka kanda moja. Ukweli huu umeaminiwa na wengi kuwa unaleta ukanda, kama wewe huna tatizo na hili, baki na mtazamo huo-lakini Lissu ameusema ukweli huo, na hajaropoka!
 
Lissu hajui saying the right thing wrongly and saying the wrong thing have the same effect and penalties.

Lissu pia hajui kuwa inahitaji busara kumtukana au kumsuta mkubwa. Hakujifunza alivyobezwa na JK wakati anamuomba aingilie mchakato wa katiba mpya kwa mamlaka ambayo yeye mwenyewe aliyapigia kelele na kumnyang'anya rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…