Hata hili nalo hatujui??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata hili nalo hatujui???

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by ngoshwe, Sep 30, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  TUMESHINDWA KUFIKIRI NA KUFIKIA HAPA?,

  HIVI kABLA YA YA MUUNGANO WA TAREHE 26 APRILI 1964; TANZANIA ILIKUWEPO?


  MBONA TUNAPOTOSHA KWA MAKUSUDI KABISA HISTORIA YA TAIFA LETU KWA JAMBO LILILO WAZI?? (HATUJUI HESABU??? HIVI TUKLIULIZWA NA WENZETU NI MAANA YA TANZANIA NAPO HATUJUI???, NA JE, WAKITUULIZA TANZANIA ILITAWALIWA NA NANI, TUNA JIBU NINI?? AU HATUELEWI TANZANIA ILIZALIWA LINI NA KWA NINI??? )..KAMA NI MUUNGANO WA TANAGANYIKA NA ZANZIBAR NDIO ULIOPELEKEA KUZALIWA TANZANIA, KWA NINI TUSIFIE MAFANIKO YA UHURU KWA MTIZAMO WA KIMUUNGANO NA SIO KI TANGANYIKA (TAIFA AMBALO KIMANTIKI NDILO LILILOZALIWA 9 DES 1961 NA SI TANZANIA)?

  EBU WASILIZE HAWA WASANII:


  Tanzania [miaka 50 ya uhuru wa tanzania] - YouTube

  KULE KWENYE TOVUTI YA TAIFA The Tanzania National Website IMEANDIKA "Taarifa ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara"
  HII INAMAANISHA "UPO UHURU PIA WA TAANZANIA VISIWANI??" ..YAANI HATUJAFAHAMU MPAKA LEO KUWA KATIKA KATIBA YETU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 IBARA YA KWANZA INATAMKA HIVI:

  "1.Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano". NA ILE YA PILI INASOMA:
  "2​
  "2(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
  pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo.

  Na ibara ya 151 (1) inatoatafsiri ya maneno "Tanzania Bara" na "Tanzania Zanzibar" kama ifutavyo:
  "Tanzania Bara" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya Tanganyika"
  "Tanzania Zanzibar" maana yake ni eneo lote la Jamhuri ya Muungano ambalo zamani lilikuwa eneo la Jamhuri ya watu wa Zanzibar na ambalo kabla ya Sheria hii kutungwa liliitwa Tanzania Visiwa"
  KIMANTIKI, IKIWA TANGANYIKA ILIKUFA KWA MUUNGANO ULIOFANYIKA NA ZANZIBAR, TUKIBAKI KUAZIMISHA UHURU WA TANZANIA, (SIO JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ) WENZETU HAWATUELEWI KWA NINI TUNASEMA 'TANZANIA" INA TIMIZA MIAKA 50 WAKATI HATUIHUSISHI TANZANIA VISIWANI AU "TANZANIA ZANZIBAR"..NA TUNASEMA ETI "TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNA SONGA MBELE", BILA KUJIULIZAA HATA HIYO "TANZANIA BARA" ILIPATA UHURU LINI??

  TUWAACHE WALE WENZETU WA UPANDE WA PILI WA MUUNGANO NDIO WANAWEZA KUSHEHEREKEA MIAKA KADHAA YA MAPINDUZI YAO (KAMA UHURU) SISI BADO TUNAHITAJI KUTAFAKARI TUNASHEREHEKEA UHURU WA NCHI IPI KATI YA TANZANIA AU TANGANYIKA??
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  mambo ya NGWOSWE muachie ngoswe mwenyewe!!
   
Loading...