Hata Baada ya Uchaguzi Sitaitazama Star TV

Hata Baada ya Uchaguzi Sitaitazama Star TV

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2015
Posts
567
Reaction score
1,565
Habari zenu wanajanvi

Mimi nilikua Mpenzi Mkubwa sana wa Star Tv, kutokana na vpindi vyao vingi vilikua Fair na vya kuelimisha.
Nilikua sijui kama kuna siku watanidisappoint kama wakati huu ninapowahitaji zaidi wanipe habari kwa ufair niliouzoea.

Nashangaa kuona vipindi vyao viko One Sided tu, wanaipendelea CCM pekee, kana kwamba hakuna Vyama vingine.
Hivi sheria zinasemaje kuhusu Vyombo vya Habari kua na Upendeleo?
Au Star TV ni Television ya CCM na je ilisajiriwa kama mali ya CCM?

Naapa mbele yenu hata baada ya Uchaguzi Sitaitazama Star TV
 
Me toka zamani nlikuwa siiangalii,iko bias sana hawajishtukii
 
Sasa hivi sijui hata hiyo tv ipoje kwani niloacha muda mrefu kuiangalia
 
Mimi.huwa naangalia itv tu....so hizo nyingine nilishaziblock kwenye kingamuzi changu,hata menu akitaka kuangalia atajibiwa no signal
 
Na sidhani kama itakuwepo kwa muda mrefu baada ya uchaguzi
 
Inasikitisha sana na inauma sana maana miongoni mwa vituo bora ilikuwa startv lkn siku hizi kimekuwa chombo cha upande mmoja.TCRA wawachuguze startv maana wanatunyima haki yetu yakupata habari zote
 
Dada usijali sana...hata marekani huwezi kukuta Fox News inaelezea story nzuri za Democrats..kama jinsi ilivyo hapa Tanzania huwezi kusikia ITV au chombo cha habari cha yule Mchagga R. Mengi kinatoa story nzuri za CCM.
 
Mwaka huu na majira na msimu huu itabid tuseme msemo mmoja wa marekani.

Haijalishi Kama Ataleta Maendeleo au la! Tutamchagua Obama Kuuonyesh a Ulimwengu Kuwa Marekani ni ya Kila Mtu.

Na sisi watanzania Kwa Umoja wet bila kujali tofauti zetu ndogo nyakati hizi ni nizakusema haijalishi kama Lowassa ataleta Maendeleo au la! ni wakati wa kumchagua LOWASSA wa CHADEMA/ UKAWA ili pia pamoja na ILANI elimu bure, katiba mpya, kufungua mawasiliano hasa reli ya kati pia uuonyesha na kuudhihirishia Ulimwengu kuwa Tanzania Siyo ya cicimu pekee.

Tuma ujumbe huu kwa Watanzania wasiopungua 1000 ili kuamsha na kuchochea mabadiliko ya kweli. Fursa hii ya Mabadiliko tukiipoteza itatuchukua miaka 30 tukikumbuka Mwaka 2015 tulijinyima mabadiliko ya katiba, mfumo, maendeleo.

Lowasa Mabadiliko
Mabadiliko Lowassa.

Samahani pia kama utakwazika imebidi kuonyesha Uzalendo kwa Taifa letu lenye miaka 54 ya Uhuru.

Maajabu likipitwa na hata jirani zetu Kenya aliyepata Uhuru kwa kuchelewa miaka 3 sasa ametupita kimiundo mbinu, elimu, utalii, kilimo, kiuchumi, Katiba Mpya,nk.

Na hata Rwanda iliyotoka vitani miaka ya 90 inatupita ingawa sisi ndio tuliowahi pata Uhuru, kujaliwa Rasilimali hata zisizo duniani mpaka zikaitwa majina yetu kama Tanzanite, mito, maziwa, Bahari-Bandari, vivutio vya utalii, ardhi yenye rutuba rasilimali adimu duniani ili tuanze kukimbia badala ya kutambaa kimaendeleo.

Kamueleze mumewako huo ujinga wa kumchagua Lowassa bila kujiuliza kama ataleta maendeleo au la, you foolish mongoose!
 
Ulikuwa hujui kuwa star TV ni ccm, TV yenye usawa katka habari ni ITV peke yke
 
Samahani pia kama utakwazika imebidi kuonyesha Uzalendo kwa Taifa letu lenye miaka 54 ya Uhuru.

Maajabu likipitwa na hata jirani zetu Kenya aliyepata Uhuru kwa kuchelewa miaka 3 sasa ametupita kimiundo mbinu, elimu, utalii, kilimo, kiuchumi, Katiba Mpya,nk.

We muumini wa Mbowe..South Africa ni moja ya nchi hapa Africa iliyopata uhuru mwishoni kabisa and yet, iko mbele sana kimaendeleo! Hii pekeyake itakulazimu urudi kwenye historia ujaribu kupata jibu la kwanini nchi za africa bado maskini.. sitaongea mengi, nakishauri tu uruhusu oxygen humo kichwanikwako ili huo ubongowako ufanye kazi ipasavyo la sivyo utakuwa kichekesho mjini
 
Startv yani nikiona tuuu hata kwa bahati mbaya nasikia kichefu chefu. Jembe itv azam tv hawa ndo wanajua wanacho fanha
 
Mi ntaacha hata kuangalia Dira ya Dunia na kumshawishi boss wangu asipeleke tena matangazo ya biashara kwenye hili li channel lisilo sawa.
 
Hata CNN kwa kawaida huwa upande wa republican lakini huwa wanatoa usawa kwa habari za wagombea wote
 
Dada usijali sana...hata marekani huwezi kukuta Fox News inaelezea story nzuri za Democrats..kama jinsi ilivyo hapa Tanzania huwezi kusikia ITV au chombo cha habari cha yule Mchagga R. Mengi kinatoa story nzuri za CCM.
Mkuu mbona itv wako fair kuliko TV channels zote hapa tz, ungekuwa na mfano relevant kama ungetumia uhuru.
 
Back
Top Bottom