Hasira: Chanzo, ukweli na athari zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hasira: Chanzo, ukweli na athari zake

Discussion in 'JF Doctor' started by Sipo, Jul 27, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi mtu anapokuwa au anapopatwa na hasira lazima chanzo kitakuwa mtu mwingine au jambo Fulani au tukio Fulani. Sababu za hasira hazipo nje ya hapo na kama kuna hasira nje ya hapa basi hizo hasira zitakuwa za kipekee.

  Lakini je ni kweli kuwa huyo mtu au hilo tukio au hilo jambo ndio lililokufanya hukasirike?

  Ukweli ni kwamba mtu au watu hujikasirisha wenyewe kwa sababu matarajio, matamanio au mapokeo ya jambo husika ambalo halikutendeka unavyotaka.

  Kwahiyo ni kosa kusema bosi, mpenzi, rafiki, baba/mama mwenye nyumba au ndugu yako au foleni ya magari ndiyo iliyokusababishia wewe kukasirika.

  Ukweli ni kwamba kiola mmoja anajikasirisha mwenyewe, ingawa anajitahidi kumrushia mwingine lawama za hasira hizo.

  Mtaalamu mmoja wa masuala ya saikolojia hapo mwaka 2005 alitoa njia 3 za kuelezea hasira zetu:-
  • Kumkasirikia mtu kwa kushindwa kutekeleza kile tulichotarajia.

  • Kukasirikia tendo la mtu lakini siyo mtu mwenyewe.


  • Kukubali kwamba mtu anajikasirisha mwenyewe ( watu wachache sana wanaifuata na kuikubali hii njia)

  Athari za hasira
  Kimsingi tu hasira za ziada au kupitiliza sio nzuri kwa afya ya mtu. Athari nyingine ni kama:-
  • Kuugua magonjwa unayoyajua au husiyoyajua

  • Kugombana na wengine nyumbani, kazini, au kwenye daladala n.k


  • Kuvunja ndoa, uchumba, urafiki, n.k

  • Kufanya matukio mabaya husiyoyatarajia kama vile kutukana matusi makubwa, kupigana n.k
  Tuache hasira za kupitiliza/ziada
   
Loading...