PreGE2025 Hashim Rungwe: Waliojiondoa CHADEMA bado hawajafika CHAUMMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiendelea kukumbwa na mtikisiko wa ndani, mamia ya wanachama wake wanaripotiwa kujivua uanachama, huku wakihusishwa na mpango wa kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kikiwa miongoni mwa vyama 19 vilivyosajiliwa rasmi nchini.

Licha ya wanachama hao kutotangaza hadharani chama wanachokusudia kujiunga nacho, duru za siasa zimeelekeza vidole kwa CHAUMMA kuwa ndiyo chaguo lao jipya, kutokana na historia ya wazi ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi, Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, amesema mpaka sasa bado hajapokea rasmi wanachama hao, lakini amesisitiza kuwa milango ya chama chake iko wazi kwa Watanzania wote.

"Wana uhuru kujiunga na chama chochote. Hadi sasa hawajaja CHAUMMA, nami nasikia kwenye vyombo vya habari tu. Tukikutana nao tutawaeleza bayana," amesema Rungwe.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa ni mali ya wananchi na si mali binafsi ya viongozi, hivyo mtu yeyote ana uhuru wa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine bila lawama.

"Hiki chama si changu, ni cha wananchi. Hakuna mwenye mamlaka ya kumzuia Mtanzania kuhamia chama kingine," amesisitiza.

Rungwe pia ameeleza kuwa mchakato wa ndani wa kupata wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho umeanza, lakini mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Mei 11-12, uliahirishwa hadi Juni 27-28, 2025, kutokana na changamoto ya kifedha.

Anasema mkutano huo utakuwa wa kihistoria kwa kuwa utafanya uteuzi rasmi wa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa tiketi ya CHAUMMA.

Akizungumzia msimamo wa chama chake kuelekea uchaguzi mkuu ujao, Rungwe amesema CHAUMMA haitasusia uchaguzi kama vyama vingine vinavyolalamikia mfumo wa uchaguzi, bali itaendelea kushiriki na kutoa maoni ya marekebisho ya sheria na kanuni kwa njia za kisheria.

"Sheria zina matatizo, lakini haziwezi kutufanya tusishiriki uchaguzi. Tutalalamika kwa utaratibu, lakini hatujawahi kususia uchaguzi," amesema Rungwe.

Akijibu kauli kwamba amekaa muda mrefu kwenye uongozi wa chama hicho, Rungwe amesema: “Wengine wanasema nimekaa sana, lakini Nyerere alikaa miaka 25 na hakuna aliyelalamika hadi alipoamua kuondoka mwenyewe.
Wako njiani mzee wanakuja na guta we andaa ubwabwa wa kutosha. Wenye akili tunajua hapo Tu kusogezwa mbele mkutano mkuu hadi juni haihitaji d2
 
Kwani walitangaza wapi kuwa wanahamia uko CHAUMMA?.Au ni porojo za watu mitandaoni.Maana Inawezekana malengo yao ni tofauti na hizo fununu zilizozagaa uko mitandaoni.Na inawezekana hizo fununu zilitengenezwa makusudi wakijua wabongo wengi watakurupuka nazo uku wao wakiendelea na mambo yao.
 
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiendelea kukumbwa na mtikisiko wa ndani, mamia ya wanachama wake wanaripotiwa kujivua uanachama, huku wakihusishwa na mpango wa kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kikiwa miongoni mwa vyama 19 vilivyosajiliwa rasmi nchini.

Licha ya wanachama hao kutotangaza hadharani chama wanachokusudia kujiunga nacho, duru za siasa zimeelekeza vidole kwa CHAUMMA kuwa ndiyo chaguo lao jipya, kutokana na historia ya wazi ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine.

Kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi, Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, amesema mpaka sasa bado hajapokea rasmi wanachama hao, lakini amesisitiza kuwa milango ya chama chake iko wazi kwa Watanzania wote.

"Wana uhuru kujiunga na chama chochote. Hadi sasa hawajaja CHAUMMA, nami nasikia kwenye vyombo vya habari tu. Tukikutana nao tutawaeleza bayana," amesema Rungwe.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa ni mali ya wananchi na si mali binafsi ya viongozi, hivyo mtu yeyote ana uhuru wa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine bila lawama.

"Hiki chama si changu, ni cha wananchi. Hakuna mwenye mamlaka ya kumzuia Mtanzania kuhamia chama kingine," amesisitiza.

Rungwe pia ameeleza kuwa mchakato wa ndani wa kupata wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho umeanza, lakini mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Mei 11-12, uliahirishwa hadi Juni 27-28, 2025, kutokana na changamoto ya kifedha.

Anasema mkutano huo utakuwa wa kihistoria kwa kuwa utafanya uteuzi rasmi wa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa tiketi ya CHAUMMA.

Akizungumzia msimamo wa chama chake kuelekea uchaguzi mkuu ujao, Rungwe amesema CHAUMMA haitasusia uchaguzi kama vyama vingine vinavyolalamikia mfumo wa uchaguzi, bali itaendelea kushiriki na kutoa maoni ya marekebisho ya sheria na kanuni kwa njia za kisheria.

"Sheria zina matatizo, lakini haziwezi kutufanya tusishiriki uchaguzi. Tutalalamika kwa utaratibu, lakini hatujawahi kususia uchaguzi," amesema Rungwe.

Akijibu kauli kwamba amekaa muda mrefu kwenye uongozi wa chama hicho, Rungwe amesema: “Wengine wanasema nimekaa sana, lakini Nyerere alikaa miaka 25 na hakuna aliyelalamika hadi alipoamua kuondoka mwenyewe.
Ameanza siasa za uongo uongo😂😂😂😂
 
"Sheria zina matatizo, lakini haziwezi kutufanya tusishiriki uchaguzi. Tutalalamika kwa utaratibu, lakini hatujawahi kususia uchaguzi."

Hawa watu ni watu wa ajabu sana. Hizi lugha sijui wanajifunzia wapi.
 
hiki chama si ndio kilikuwa backup plan ya team Lissu? sasa wakinyang'anywa chama na msajili wataelekea wapi?
 
Back
Top Bottom