PreGE2025 Hashim Rungwe: Waliojiondoa CHADEMA bado hawajafika CHAUMMA

PreGE2025 Hashim Rungwe: Waliojiondoa CHADEMA bado hawajafika CHAUMMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiendelea kukumbwa na mtikisiko wa ndani, mamia ya wanachama wake wanaripotiwa kujivua uanachama, huku wakihusishwa na mpango wa kujiunga na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), kikiwa miongoni mwa vyama 19 vilivyosajiliwa rasmi nchini.

Licha ya wanachama hao kutotangaza hadharani chama wanachokusudia kujiunga nacho, duru za siasa zimeelekeza vidole kwa CHAUMMA kuwa ndiyo chaguo lao jipya, kutokana na historia ya wazi ya kupokea wanachama kutoka vyama vingine.

1747224747039.png
Kwa mujibu wa tovuti ya Mwananchi, Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe, amesema mpaka sasa bado hajapokea rasmi wanachama hao, lakini amesisitiza kuwa milango ya chama chake iko wazi kwa Watanzania wote.

"Wana uhuru kujiunga na chama chochote. Hadi sasa hawajaja CHAUMMA, nami nasikia kwenye vyombo vya habari tu. Tukikutana nao tutawaeleza bayana," amesema Rungwe.

Ameongeza kuwa vyama vya siasa ni mali ya wananchi na si mali binafsi ya viongozi, hivyo mtu yeyote ana uhuru wa kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine bila lawama.

"Hiki chama si changu, ni cha wananchi. Hakuna mwenye mamlaka ya kumzuia Mtanzania kuhamia chama kingine," amesisitiza.

Rungwe pia ameeleza kuwa mchakato wa ndani wa kupata wagombea wa nafasi mbalimbali katika chama hicho umeanza, lakini mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Mei 11-12, uliahirishwa hadi Juni 27-28, 2025, kutokana na changamoto ya kifedha.

Anasema mkutano huo utakuwa wa kihistoria kwa kuwa utafanya uteuzi rasmi wa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar kwa tiketi ya CHAUMMA.

Akizungumzia msimamo wa chama chake kuelekea uchaguzi mkuu ujao, Rungwe amesema CHAUMMA haitasusia uchaguzi kama vyama vingine vinavyolalamikia mfumo wa uchaguzi, bali itaendelea kushiriki na kutoa maoni ya marekebisho ya sheria na kanuni kwa njia za kisheria.

"Sheria zina matatizo, lakini haziwezi kutufanya tusishiriki uchaguzi. Tutalalamika kwa utaratibu, lakini hatujawahi kususia uchaguzi," amesema Rungwe.

Akijibu kauli kwamba amekaa muda mrefu kwenye uongozi wa chama hicho, Rungwe amesema: “Wengine wanasema nimekaa sana, lakini Nyerere alikaa miaka 25 na hakuna aliyelalamika hadi alipoamua kuondoka mwenyewe.
 
John Mrema Alidhani Hashim ni kama Yule muhaya aliyedhulumiwa chama chake cha TLP na Lyatonga

Hashim ndio alifungua uuzaji wa magari used kutoka Japan kwenye Yard 😁😁 ndio baadae wakafuatia akina Mazrui, Mtawali, Toto Kanko nk 😂🇹🇿
 
Nahisi kuna mpango ulitakwa kusukwa kwa msajili ili walazimishe chadema wao wawe ndio wanatambulika sio wengine.
Lilipo kujwa swala la kusema msajili wa chama hatambui wenyekiti wa chadema ili wafanye kama ile CovD-19 ambao waliingia bungeni sijui kupitia chama gani huku wakilazimisha kusema ni wanachadema
Meza kwanza ndiyo uongee
 
John Mrema Alidhani Hashim ni kama Yule muhaya aliyedhulumiwa chama chake cha TLP na Lyatonga

Hashim ndio alifungua uuzaji wa magari used kutoka Japan kwenye Yard 😁😁 ndio baadae wakafuatia akina Mazrui, Mtawali, Toto Kanko nk 😂🇹🇿
Hapo anaenda kukwama na tamaa zake, pia hata kaa muda mrefu kabla ya kukimbilia CCM
 
Nahisi kuna mpango ulitakwa kusukwa kwa msajili ili walazimishe chadema wao wawe ndio wanatambulika sio wengine.
Lilipo kujwa swala la kusema msajili wa chama hatambui wenyekiti wa chadema ili wafanye kama ile CovD-19 ambao waliingia bungeni sijui kupitia chama gani huku wakilazimisha kusema ni wanachadema
Msajili amebanwa haswa
 
John Mrema Alidhani Hashim ni kama Yule muhaya aliyedhulumiwa chama chake cha TLP na Lyatonga

Hashim ndio alifungua uuzaji wa magari used kutoka Japan kwenye Yard 😁😁 ndio baadae wakafuatia akina Mazrui, Mtawali, Toto Kanko nk 😂🇹🇿
Amekutananna mtoto wa mjini, og long time kwneye game 😂😂😂
 
Anaposema Bado hawajafika CHAUMMA ana uhakika wapo njiani
 
Si ubweche upo!!!! Wananunua ndizi mbivu kwanza na visalufeti ili ukibaki wawapelekee na wanyumbani
 
Back
Top Bottom