Hasara zipi unazipitia kwa kuwa na tabia za introvert?

Najitahidi kujichanganya ila sipendi kelele ata nikionja pombe naongea kidogo sana ukijumlisha na utamaduni wa jamii forumu wa kuficha ID watu wanaishia kukuogopa bila sababu.

Introvert kwanza ni kujijua na kufanya vitu exception watu watakutafuta wenyewe wakuletee pesa. Mimi najiweka zaidi upwork kama freelancer, kuandika vitabu, majarida, kusoma lugha mpya. Ukijua kipaji chako utafanya maajabu pia kusoma mavitabu ya kukuwezesha kuendana na mabadiliko kama kuondoa useriousness, siasa kidogo na kuijua dunia. Pia mbinu ya kujiweka low profile ili uonekane wa kawaida usipewe attention sana
 
Washikaji wanaopenda jifungia ndani mara nyingi wanakuaga wachafuuuu...

Ukiingia ghetto yake ndio wale unapata sahani zipo kwa bed, soksi na vinasa vimeanikwa kwa dirisha n.k
 
Washikaji wanaopenda jifungia ndani mara nyinhi wanakuaga wachafuuuu...

Ukiingia ghetto yake ndio wale unapata sahani zipo kwa bed, soksi na vinasa vimeanikwa kwa dirisha n.k
Mimi napenda usafi kuliko maelezo niko tayari kurudia nguo kila siku ata mwaka mzima ila iwe tu imefuliwa ni safi fashioni hazinisumbui usafi tu na usalama wa eneo ndio kipao mbele changu popote napokuwa naishi.
 
Introverts wako makundi makundi.

1. Super introvert,
2. Hybrid introvert,
3 Introvert uchwara,
4. Inteovert wakijani,
5. Introvert wekundu,
6. Introvert domo zege,
7. Introvert uchoyo, n.k
Mimi ni super introvert
 
Tabia ya kupenda kukaa peke yangu bila kuwa na mazoea sana na washakaji ama majirani, kuna siku niliumwa wakuu nikakaa ndani siku nzima nakunywa maji tu hakuna anayejua kama naumwa.

Homa ilinikamata vibaya nje sionekani washakaji na majirani wakajua ndio kawaida yangu kuwa ndani kumbe mwenzao maji ya shingo, niko mbali na familia, wife hayupo.

Nikapiga simu kwa wife, wife akasema huyu jamaa atakufa kwa sababu ananijua sina kampani, wife akasafiri kesho yake akaja ndio ikawa afadhali yangu maana ugonjwa ukiwa peke yako unazidi.

Nikasema nikipona mimi jamani ntatafuta washkaji wa kutembeleana ili nikipata matatizo nisaidiwe, baada ya wiki kupona ndio kwanza nikazidi kujichimbia ndani na vitabu vyangu uchwara😀😀😀

Nashauri wakuu tujitahidini kuwa na watu wa karibu washkaji ama majirani, mimi imenishinda kidogo.
introvert unakuaje na mke!!!? introvert ni kupiga nyeto yaan hata bidhaa za uwanja wa fisi shopping center hununui...
 
Kushindwa kujichanganya na watu ambao kwa namna moja au nyingine khna faida kufahamiana nao na pia kushindwa kutoa hisia zangu kwa mtu nnayempenda.

Changamoto nyingine ni kushindwa kuja ma majibu ya haraka katika muda ambayo yanahitajika kwani nachukua muda mrefu kuprocess taarifa na kuja na mjibu sahihi, kitu ambacho huwa kinawakwaza wakati wengine nnaofanya nao kazi
 
Mimi pia nina hiyo tabia nikitoka job nakaa ndan tu natafuta PlayStation iko wap nikimaliza natafuta movie iko wap Yani sina muda na mtu na sipendi kelele, ukitaka kunifukuza we fungulia mziki mkubwa tu au ongea kwa kelele yan hutaniona hali inayo sababisha sipend kukaa vijiwen na hata nikikaa nakua siyo muongeaji hivyo nakua sion umuhim wa kujichanganya.

Sasa siku moja malaria ilinikamata vibaya sana, nipo ndan hoi alaf naish peke yangu tu nikaanza kutapika had nikahisi kuhishiwa nguvu, na vile huwa sina tabia ya kupika alaf hotel huwa zipo mbal kdogo na hamu ya kula sina bas nikaendelea kukomaa hivyo hivyo , nakumbuka nilitapika sana, kilicho saidia Alikuja jiran mmoja ambae yeye huwa anakuja getto kwang kuchek mechi, ni kwa bahat tu Alikuja Kama kawaida yake huwa anakuja kunipa Hi na kupesa zake siku hiyo akanikuta naumwa balaa, Jamaa ndo akaenda kumwambia mke wake akoroge uji akaniletea ndo nikapaha ahueni.

Nikasema nikipona nitakua najichanganya baada ya kupona nikawa najichanganya nakumbuka niliweza kwa wik 1 tu baada ya hapo nikarud kwenye hali yangu, ninacho zingatia ni kuto kumdharau yoyote na kuishi kwa upendo licha ya kuwa sina mazoea na watu kwahiyo watu wanatokea kunikubali sana wengne hata sina mazoea nao ya karbu
 
JF inasaidia Sana kwani imereplace unnecessary conversations ,

Mfano mtu anakuletea stori za Simba mara Yanga,

Sijui Lil Wayne kanunua gari jipya au Jenifer Lopes kaachika, unakua unaperuse mada mbali mbali.
 
Nimeshindwa mahusiano na wadada kadhaa sababu ya ukimya na kutojisikia kufanya interaction na watu ambao naona they "don't speak the language that I do" Yani mahusiano yanagoma kabisa...Sasa ni rasmi natafuta introvert mwenzangu labda tutaelewana .
 
Back
Top Bottom