Hasara za kuwa mchepuko

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
How are you neeeeeeeeeeeeee...

Bila shaka suala la KUCHEPUKA limekuwa tatazo sugu kwa wana ndoa.Ewe mchepukaji zijue hasara pengine utamtafuta wakwako wa halali.

1. Huna mamlaka na mwenza huyo
2. Huwezi post picha yake kwenye mitandao

3. Huna utambulisho rasmi i mean unamtambulisha nani wako.

4. Hutambuliki kidini wala kiserikali hivyo sheria zote zipo kwake hata akifa huwezi jitokeza, hata Kama ulimuwezesha kiuchumi akatajirika hupati urithi.

5. Ukizaa nae mtoto Hana identity ulazimishe tu.

6. Huna haki yoyote anaweza akakupa gari kadi akawa nayo siku akiamua anakunyang'anya mbele za watu.
Anaweza kikupangishia au kukupa nyumba yake ukae akiamua anakufukuza Kama mbwa Kala mayai.

7. Huwezi kuwa na Uhuru nae anaweza kuwa katikati ya mechi akapigiwa cm na mkewe akavaa na kutoka mbio.

8. Masharti mengi anakupangia muda wa cm, hataki marafiki wajae alipokuweka, wivu sasa utadhani hata Kama kwenu wanamjua.

9. Akikufia ndani utaisaidia polisi

10. Huna hadhi hata Kama mzuri kushinda mkewe, umpe mapenzi yote bado we choo cha public tu anaingia kwa dharura hata kiwe kizuri namna gani lakini havunji choo chake cha nyumbani.

Mchepu amka utaishi gizani mpaka lini Kama dini inaruhusu mwambie akuweke kwenye nuru ama hataki subiri atakuja wa kwako naamini ukijituliza wapo tele ndege wetu hawa.

Kuliko kuishi na MTU anakuzibia riziki ya kumpata mwenza wako nawe hata mkila ugali na dagaa LA kuchoma mnalia uwanjani kuliko kuku wa kulia uvunguni.

Anakuzeesha hata walokuwa wanakumezea mate watakuona wa nini.
Acha kuwa spair tyre unaweza ishi bila yeye.

Hakuna binadamu wa nyongeza
Jishughulishe kutafuta riziki, sali na omba Mungu anamsikiza kila aliyemuumba.
 
Hahahahahahaahahahah aseee ni ukweli mtupu na inaumaje ? ila sasa kale kabint kweli unazani nirahis kwa haya maneno yako ya reja reja mimi niamue nimuache aende zake ? hapana umetupa jiwe gizan nakiri limenipata ila simwachi wife nampenda na kabinti nakapenda flan sio sana sijui kameniloga sijui na sijui picha litaishaje
 
Ujumbe wa mwaka 2017
 
Mbona bi mdogo wa machache anakula raha kwa uhuru tele miradi anayo watoto ndo hao na bonge la nyumba kajengewa, washauri wakiwa na waume za watu waangalie ana upendo kweli ampe miradi yake nyumba ya jina lake na asiwe bahiri, na wanawake wakiolewa wasibweteke kisa pete na karatasi eti ndoa hawezi kuniacha, kamuulize mke wa mchungaji lusekelo
 
Ama kweli leo ni ijumaa ya mwisho kwa mwaka 2016 mana mada za leo moto moto.
Za kufungia mwaka.
 
Mbona bi mdogo wa machache anakula raha kwa uhuru tele miradi anayo watoto ndo hao na bonge la nyumba kajengewa, washauri wakiwa na waume za watu waangalie ana upendo kweli ampe miradi yake nyumba ya jina lake na asiwe bahiri, na wanawake wakiolewa wasibweteke kisa pete na karatasi eti ndoa hawezi kuniacha, kamuulize mke wa mchungaji lusekelo
Eeeeh mkuu em funguka kidogo mke wa mchungaji Lusekelo yamemsibu yepii
 
Sasa je nkiwa nimeolewa na nina mchepuko itakuaje. Na Mchepuko wenyewe una mke. Ebu fafanua hapo hiyo legue. Maana hapa kuna vitu mchepuko unasidia haswa kupata ajila.
 
sasa si ndo maana ya mchepuko yenyewe hio asee, mchepuko atapewaje haki sawa na mke au mchumba , hapo sema hizo ni tofaut kati ya mke na mchepuko
 
Back
Top Bottom