Tuelewane tu hapa na tuwekane sawa kiroho safi.
Kutumia pombe kuna hasara yake ila hakuwezi kuzidi hasara ya kuacha pombe. Kuacha pombe kuna hasara kubwa (nyingi) zaidi kuliko faida katika muktadha ufuatao:
Ukiacha pombe;
1. Utakosa marafiki wengi sana ; wazuri na wabaya
2. Utakosa mambo mengi sana ya mtaani na ya kidunia (kiuchumi kijamii na kisiasa)
3. Utakosa ramani /dili nyingi sana za kukupatia kipato . Walevi wengi hukaa na kuweka mikakati bar na huwa inafanikiwa
4. Utachelewa sana kujenga nyumba na kuwa na gari . Walevi wengi wana magari mazuri na wana mijumba mingi sana
5. Utashindwa kumudu familia yako na utakuwa unagombana na mkeo /mumeo kila siku. Maana kila siku mnakodoleana macho tu home.
7. Utakuwa mtu wa majungu tu na unafiki kazini na mtaani pia
8. Utakuwa mchawi na mpenda ushirikina sana
9. Unakuwa ' mwanaume wa Dsm'. Mwanaume laini laini
10. Utakuwa unapigwa sana na mkeo
11. Nchi itakosa mapato kwa kunywa soda sana
Tunywe tu pombe maana hatuna namna!
Waiter ongeza moja.