Hasara katika biashara

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
DIS-ECONOMIES OF SCALE

Hiki ni kinyume cha economies of scale.

Ni kitendo cha gharama za uzalishaji kuongezeka kadri unavyoongeza uzalishaji wa bidhaa.

Mfano:
Una fuso lako la kusafirisha mizigo, mwanzoni ukaona hulitendei haki kwa kubeba mizigo michache, ukaamua kuongeza mizigo.

Kitendo cha mizigo kuwa mingi kikasababisha wewe kukamatwa na TANROAD na kulipishwa fine ambayo inakurudisha nyuma kimaendeleo.

Mfano 2:
Una kijana mmoja wa kazi wa kukusaidia kazi zako za ndani, ukaona uajiri mfanya kazi mwengine ili wasaidizane kufanya usafi.

Kitendo cha kuongeza mfanyakazi mwengine pia umeongeza gharama kama mshahara, vijana wote wanakula kwako, wakiumwa wote utahitaji kuwatibia. Kwahiyo lengo lako la kufanya nyumba iongezeke usafi gharama zimekuwa kubwa.

Mfano 3:
Una bakery, umeajiri mpishi unamlipa 400,000 na ana uwezo wa kutengeneza mikate 100 kwa siku, bei ya mkate 1 ni 1,000.

Kila siku mikate yote inauzika na bado kuna wateja 10 na zaidi wakija kuulizia wanakuta mikate imeisha.

Kwasiku 1 Mauzo yako ni = mikate 100 x bei 1,000 = 100,000

Kwahiyo una uwezo wa kuuza 100,000 kwa siku.

Kwa mwezi una uwezo wa kuuza = 100,000 x 30 = 3,000,000

Ukitoa gharama ya kumlipa mpishi mshahara

= 3,000,000 - 400,000 =2,600,000

Ukaona basi ni kheri uajiri mpishi mwengine ambaye nae utamlipa 400,000 ili atengeneze mikate 10 ya wateja wanaokosa.

Mauzo kwa siku = mkate 110 x bei 1,000 = 110,000

Mauzo kwa mwezi = 110,000 x 30 = 3,300,000

ukitoa mishahara ya wapishi =400,000 x wapishi 2 = 800,000

mauzo - mishahara = 3,300,000- 800,000 =2,500,000

Kwahiyo kwa kuongeza uzalishaji wa mikate 10 na kuongeza kumuajiri mtu mwengine kumekupunguzia kipato kwa 100,000

Na hapo hatujapigia ongezeko la gharama nyingine kama mafuta, unga, amira, umeme, maji, mifuko nk.

Tume assume gharama yako ni mshahara tu, kwahiyo kuna bidhaa nyingine unavyojitahidi kutengeneza nyingi basi gharama huongezeka maradufu

Kama mnakumbuka law of diminishing marginal return kwamba kuna sehemu ikifika hata ukiongeza kitu flani uzalishaji hautoongezeka badala yake utapungua.

Basi diseconomies of scale nayo ni ile sehemu ambayo kadri unavyoongeza uzalishaji gharama inakuwa kubwa sana.

Mfanano wa hizi theories ni kwamba, ni rahisi mfanya biashara kupata hasara akiwa katika hii position.

TOFAUTI YA DIMINISHING MARGINAL RETURN NA DISECONOMIES OF SCALE NI HIZI:

DIMINISHING MARGINAL RETURN

1.Hutokea biashara itakapoongeza kitu kimoja na kuacha kuongeza vitu vyengine ambavyo ni muhimu katika ukuaji wa biashara.

2.Hii ni rahisi kutokea katika mda mfupi kweye biashara

DISECONOMIES OF SCALE

1. Hutokea gharama za uzalishaji kuongezeka kadri unavyojitahidi kuongeza idadi ya bidhaa.

2.Hii hutokea kadri biashara inavyozidi kuwa kubwa

Mara nyengine Diseconomies of scale husababisha bei ya bidhaa kuongozeka ili mfanya biashara aweze kupata faida.

Bei ya bidhaa ikipanda inamaana itasaidia kulipa zile gharama za uzalishaji zilizoongezeka.

#law #diseconomiesofscale #diminishingmarginalreturn #opportunitycost #economics #averagecost #swahili


diseconomies_of_scale_final-db85c494049d42aca10deb37e214a013.png
 
Mkuu, mbona issue yako ni simple tu, mpaka utulete diagram? Au unakaaga na vilaza?
 
Sas unavyosema faida itabaki 2600000 Hapo other things remain constantly manake huwezi toa tu mshara na kujitangazia kuwa una profi ya 2.6 wakati cost of raw material hujaweka.

Kimsingi ujaeleza hasara ya biashra bali umeleza hatari tu inayopatikana kutokana na ongezeko la mfanyakazi wakati factor ziko nyingi za inayosababishwa na hasar katika biashara
 
Sas unavyosema faida itabaki 2600000 Happ other things remain constantly mnk uwez toa tu mshara na kujitangazia kuwa una profi ya 2.6 wkt cost of raw material ujaweka
Kimsingi ujaeleza hasara ya biashra bali umeleza hatari tu inayopatikana kutokana na ongezeko la mfanyakazi wkt factor ziko nyingi za inayosababishwa na hasar ktk biashara
Kwaio kwa kuongeza uzalishaji wa mikate 10, na kuongeza kumuajiri mtu mwengine kumekupunguzia kipato kwa 100,000
Na hapo hatujapigia ongezeko la gharama nyengine kama mafuta, unga, amira, umeme, maji,mifuko nk.

Tume assume gharama yako ni mshahara tu, kwaio kuna bidhaa nyengine unavyojitahidi kutengeneza nyingi basi gharama huongezeka maradufu

Lengo ni uelewe concept, ili iweze kukusaidia katika biashara zako, sijasema ni faida
 
Back
Top Bottom