barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,404
- 29,811
Kama nilishachangia watu iweje ikifika zamu yangu wasinichangie?
Huu ndo upumbavu nisioutaka!
FADHILA.
Kama nilishachangia watu iweje ikifika zamu yangu wasinichangie?
sitoagi mimi ni upuuzi
sionlogic ya kufunga harusi ya mamilion
hivi una prove nini na kwa kina nani na for what??
mimi kufurah na ndugu zangu na watu wangu wa karibu is all i want
so simple wedding with simple budget
Sisi watanzania tunalemazana sana kuhusu hii michano ya harusi, kwanini mtu usifanye harusi simple tu?!!kulingana na uwezo wako. Unaweza kukuta una kadi hadi 5 kwa mwezi eti michango ya harusi! Ukipiga hesabu kwa mwaka kama utaamua kutoa yote unajikuta umepoteza hela nyingi sana kwenye harusi tu! Na utakuta mtu anakuomba mchango, bahati mbaya kipindi hicho unaweza kuwa mtu umetingwa na mambo muhimu au huna hela kwa muda huo, mtu unamwambia sina anakasirika! Utadhani anakudai! Wanashindwa kufikiri kuwa kuna ugonjwa, misiba n.k ambapo bado unaweza kumsaidia! Wao wanaona harusi tu bila kujua kuna matatizo ya muhimu ya kusaidiana nje na michango ya harusi. Mimi huwa nachangia kwa mtu wa karibu mnoo na tena nikiwa na hela ambayo hata nikitoa haitaathiri mipango yangu.
Umenena vema mkuu ni kama tulipanga wote. Mimi nilishajitoa kitambooo! Watu watongozane huko waanze mapenzi yao halafu wanaanza kusumbua watu na kadi ili wachangiwe kufanya sherehe za harusi. Cha muhimu ndoa na haina gharama yoyote. Harusi ni starehe kama wanataka wagharimie wenyewe sio kusumbua watu kutwa nzima wanazunguka na kadi za harusi. Kuna mmoja kanikata maaini tuko msibani mahali ananikabidhi kadi ya harusi. Wanatembea nazo mpaka misibani bila aibu. Halafu utashangaa kwenye ugonjwa na misiba hawatoi michango lakini wanasaka watu wawachangie. Sasa mimi huwa najiuliza kama wana pesa za kutengeneza kadi na kuandaa vikao kibao vya kupanga harusi zao kwanini wasitumie hizo pesa za kutengeneza kadi na kuandaa vikao ambavyo humo hunywa na kula kwanini wasitumie gharama hizo kuandaa harusi kwa uwezo wao? Bora kutembeza kadi za kuchangia wagonjwa na elimu kuliko harusi. Wakisha tawanya kadi za harusi wanaanza kuzunguka kufuatilia utafikiri wakusanya kodi. Wengine simu haziishi wakifuatilia michango. Halafu pamoja na mbwembwe zote za kufanya miharusi mikubwa utashangaa kukuta ndoa nyingi hazidumu. Mwaka jana jamaa watatu wamenisumbua sana kwa michango ya harusi. Ndoa mbili kati ya hizo zimeshavunjika. Mimi nimeagiza waandishi wa waniandikie kiba ili nibandike mbele ya nyumba yangu maana sasa nimechoka na hivi tunaelekea mwishoni mwa mwaka watu wako bize kuandaa kadi. Nimewaambia sitaki kadi kabisa waandike: TANGAZO: HATUPOKEI KADI ZA KUCHANGIA HARUSIJamani tukubaliane this is to much,Michango ya harusi mjini inafilisi watu,Tutaendelea na huu utamaduni wakuchangiana mpaka lini?Tena tunapeana na kiwango "Eti 50000 ni single
Mtu unakuta mtoto wake anavaa nguo za shule zilizochanika anashindwa kumnunulia,lakini anakomaa kulipa mchango wa harusi ili jamii na rafiki wasimwone mbaya.
Kwa nini tusiwe tunafunga harusi za kifamilia tu kuepusha hili janga?
Kwa nini tusifunge harusi mtindo kama wa birthday tu washikaji kadhaa na ndugu kadhaa biashara imekwesha.
Hapa nilipo nina madeni ya michango mengi mno,Kiasi kwamba nimefikia uamuzi kuanzia sasa sintochangia mtu harusi tena
Acha nikamalizie banda langu mdogo mdogo ni hamie kwangu huku ni kutiana umasikini tu.
Ina maana itafika mwaka 2060 tunaendelea na ujinga huu tu?Mimi nimejitoa acha wanione mbaya watakuja kunielewa mbele ya safari.
sitoagi mimi ni upuuzi
sionlogic ya kufunga harusi ya mamilion
hivi una prove nini na kwa kina nani na for what??
mimi kufurah na ndugu zangu na watu wangu wa karibu is all i want
so simple wedding with simple budget
Jamani tukubaliane this is to much,Michango ya harusi mjini inafilisi watu,Tutaendelea na huu utamaduni wakuchangiana mpaka lini?Tena tunapeana na kiwango "Eti 50000 ni single