GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,548
- 108,879
Kuna Harusi moja nimeiona imefanyika nchi Jirani tu hapo ambapo Kwanza wakati Bwana Harusi anaenda Kupeleka Mahari kwa Wakwe zake alikodi Helikopta. Siku ya Harusi yenyewe ilifanyika ndani ya Ziwa Victoria ambapo kuna Meli maalum ilikodiwa na ikarembwa ambapo Wageni waalikwa wote waliingia humo Kula, Kunywa na Kusaza.
Hiyo ikiwa ni Tisa ambapo Kumi yake sasa ilikuwa ni wakati wa Kutoa Zawadi Siku ya Harusi ambapo Zawadi ndogo ambayo ilitolewa kwa Wanandoa hao ni ya Gari aina ya IST ambayo aliyoitoa alisema iwe ni ya Wafanyakazi Wao kuitumia kwenda Kufanya Manunuzi yao Sokoni au kwenda Kujazia Majiko yao ya Gesi pale ikipungua.
Harusi ilipomalizika tu Wanandoa haraka sana waliwahishwa Uwanja wa Ndege kwenda Fungate ( Honeymoon ) yao huko nchini Ufaransa katika Kisiwa kimoja maarufu na chenye Gharama sana Kutembelewa na wengi wanaotembea huko ni wale Binadamu Matajiri kuliko wengine ulimwenguni.
Najuta hata Kuisoma hii taarifa kwani imeshanivunja kabisa Moyo wa Mimi kuendelea na Mchakato mzima wa Kupeleka Mahari na Kujiandaa na Harusi kwani nina uhakika haya yaliyofanyika katika hiyo Harusi ya Kitajiri ( Kifahari ) hapo juu sina ubavu nayo na yangu itakuwa ni ya Kimasikini zaidi.
Wanaume wenzangu tujitahidi tutafute Hela Kwanza ili nasi tuwe na Jeuri kama ya huyo Mwanaume mwenzetu wa nchi jirani. Sijui Sisi wengine tumekosea au tumechelewa wapi na Sisi ama Kuzaliwa na Wazazi Matajiri au kupitiwa pembeni na Pesa ambazo Wenzetu hawa wanazo.
Tujadili.