Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

wise one

Member
Joined
Sep 29, 2014
Posts
35
Reaction score
18
Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni 10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish, alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo, mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda.

Wakuu ushauri
 
Haaa kwanza asante kwa kunijuza ulinunua plot ya ten million turudi kwenye mada wanasema vitu vidogo vina maana kubwa sana katika mapenzi ni ngumu kukushauri uachane nae au uendelee nae kwa kuwa mwisho wa siku wewe ndio mwenyewe maaumuzi ndo unajua ni vipi moyo wako umemuelemea huyo dada ila kibinaadam amekosea sana gari na uhai asee mh hajui kama bila huyo mama asingekuona wewe??
 
Usifanye papara ya kuoa, tulia kwanza. Inawezekana mhemko wa kumuoa "Bi harusi mpya" ni kwa sababu umeudhiwa na mchumbwa wako. Ila kwa suala la kumuacha mchumba umeshaona taa nyekundu usingoje kupigiwa honi.
 
Kama ulikuwa umemshirikisha Mungu kupata mke mwema hakika hilo ndo amekupa jibu huyo sio mke kabisa, mimi binafsi sijamuelewa ni mchoyo kupitiliza mama yako ni mama yake. Je angekuwa mama yake hizo hela asingetoa?

Aisee yamkini huyo aliyekusaidia ndie mtu sahihi, sasa usichukue maamuzi haraka wewe endelea kumsihi Mungu, sasa hivi tulia hicho kikao peleka mbele.
 
Hata mimi nimempenda huyo aliyekukopesha hela, yule mwingine jini gari linamuongoza na kuna uwezekano likamtokomeza kuzimu.

Kwa kigezo hiki kimoja mchumba kajifelisha mwenyewe asimlaumu mtu.
 
Fikiria mara mbilimbili maamuzi yako, unaweza kuja juta mbele ya safari!
 
Huyu demu hakufai mwache akaolewe na hizo pesa zake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama ni kweli usemayo kwa maono yangu hapo huna mke, maana daima watanzania tumezoea kupimana utu wetu kwenye matatizo na hillo limekua jibu tosha kwako kuwa mkeo huyo mtarajiwa yupo kimaslahi zaidi. Kama umesema umemsaidia mengi na alikua na fedha kweli akagoma kukupa inamaana hakuona umuhimu wa mzazi wako. Vipi ingekua kwake? AKILI KUMKICHWA.
 
Dalili ya mvua ni mawingu,bora kuvunja uchumba kuliko ndoa huenda mungu amekuonesha ili ujue unaenda kuishi nae alivyo daima mtu mwema utamjua kipindi cha shida ss huyo hela ilikuwa ngumu kukukopa ht nguvu yake ya kwenda kumuuguza mm mkwe imemshinda muombe mungu wako atakupa jibu zur
 
Back
Top Bottom