Haruna Iddi taratibu ana mtaa Dodoma?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
HARUNA IDDI TARATIBU: DODOMA IMEMPA MTAA?

Rafiki yangu mmoja jana kanilietea picha bila ''caption,'' chini akaandika kuniuliza kama namtambua huyo aliyekuwa katika picha.

Nikamjibu kuwa simtambui.

Akanirejeshea jibu akaniambia kuwa huyo kweye picha ni Mzee Haruna Iddi Taratibu.

Picha ya Haruna Taratibu katika utu uzima wake ni hiyo hapo chini.

Lakini si wengi wanaomjua Haruna Taratibu, fundi muashi wa Public Worls Department (PWD), Dodoma aliyeasisi TANU Central Province kupigania uhuru wa Tanganyika.
1659676846056.png

Haruna Iddi Taratibu​
Upungufu huu katika nchi yetu ni katika moja ya misiba mikubwa tuliyonayo kuwa mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika hawafahamiki.

Kwa hakika nisingeweza kumtabua Haruna Taratibu kwani nilikutananae Dodoma mara moja tu ofisini kwake mwaka wa 1986 wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Wakati ule Haruna Taratibu alikuwa mmoja wa wafanyabiashara mkubwa hapo mjini.

Haruna taratibu alinipa historia ya kusisimua yake mwenyewe na ya wazalendo wengine wakati wa siku za mwanzo za kuunda TANU na misukosuko waliyopata kutoka kwa wakoloni.

Nilipata wasaa vilevile wa kuzungumza na Mzee Omari Suleiman ambae alikuwa pamoja na Haruna Taratibu katika harakati hizo.
Halikadhalika pia nikazungumza na Hassan Suleiman aliyekuwa kiongozi wa TAA Dodoma katika miaka ya 1950.

Katika kitabu nilichokuja kuandika iko sura nzima kuhusu harakati za uhuru Dodoma na nikawataja wote waliokuwapo katika nyakati zile - Hassan Suleiman, Ali Juma Ponda, Alexander Kanyamala, Job Lusinde, Amon Nsekela kwa kuwataja wachache.

Turejee kwa Haruna Taratibu.

Kwa kuwa nilikutana na Haruna Taratibu kwa mara moja tu tena miaka mingi iliyopita sikuweza kumtambua.

Mwaka wa wa 2010 nilikwenda Dodoma nikakutana na Faiz Iddi Mafungo mtoto wa Iddi Faiz Mafungo ambae baba yake yuko kwenye picha ya pili hapo chini wa kwanza kulia.

Faiz alinipa picha ya baba yake, Iddi Faiz Mafungo akiwa na Haruna Taratibu, Sheikh Mohamed Ramia, Saadan Abdu Kandoro na Julius Nyerere iliyopigwa Dodoma Railway Station mwaka wa 1956 lakini picha hii ilikuwa taaban, imechoka sana.

Picha hii nimeipa jina katika Maktaba yangu inaitwa Wamanyema Wanne na Julius Nyerere Dodoma kwa sababu hao wote waliomzunguka Mwalimu - kuanzia kulia Haruna Iddi Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo ni Wamanyema.

Majuma machache yaliyopita mtoto wa Ally Sykes, kijana Araf Sykes akaniletea picha hii ya Wamanyema Wanne lakini hali yake ilikuwa nzuri na mimi nikaiweka hapa uwanjani ili sote tufaidi.

Waliobahatika kuiona picha hii watakumbuka.

Picha hiyo mpya naiweka tena hapa ili wasomaji wangu wamuone Haruna Taratibu alipokuwa kijana wa kama miaka 25 mwaka wa 1956 na Haruna Taratibu sasa mtu mzima.

Kila ilipotokea fursa nimekuwa nikijitahidi kueleza historia za mashujaa waliosahauliwa ambao walipigania uhuru wa Tanganyika ili kuiweka sawa historia ya nchi yetu tusiache Tanganyika ikiwa nchi isiyokuwa na mashujaa wake.

Hii itakuwa aibu kwetu kama nchi.

Katika kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika niliandika makala ya harakati za Haruna Taratibu katika kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyochapwa na An-nuur.

Ndiyo nauliza, '' Hivi sasa katika kuweka anuani za makazi na kutoa majina ya mitaa Je, Dodoma imemwadhimisha shujaa wake Haruna Iddi Taratibu kwa kumpa mtaa?''

1659676939066.png
1659676979381.png
 
Back
Top Bottom