Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,820
- 218,493
Wakuu natanguliza salamu hasa baada ya mchakato wa uchaguzi unaoendelea nchini kushika kasi.
Taarifa kutoka Kyela zinathibitisha kwamba kwa mara ya kwanza Ndugu Mwakyembe maji yamemfika shingoni asijue la kufanya baada ya Wanaccm akiwemo anayeitwa KINANASI kuchoka na uongozi wake duni na hivyo kuamua kupambana naye kwenye kura za awali ,Vijana wengi wa ccm wanazungumza kwa lugha ya kinyakyusa huku wakijiapiza kwamba " ALILEPO KAKO " kwa kiswahili tafsiri yake ni kwamba AMEKULA VYA KUTOSHA , na sasa anapaswa kupisha wengine .
Ikumbukwe kwamba Mwenyekiti wa CCM amekwisha tamka hadharani kwamba hajamtuma mtu yeyote kugombea ubunge na kwamba kila mtu apambane na roho yake , bali inafahamika kwamba bila mbeleko Mwakyembe ataishia kwenye kura za maoni .
Tutaendelea kuwaletea habari za uchaguzi za jimbo la Kyela kila zinapojiri .
UPDATES:
Mwakyembe 252
Mwakifuna 288
Kinanasi 502