Uchaguzi 2020 Baada ya Kamati Kuu CHADEMA kumpitisha Alinanuswe Mwalwange kugombea Ubunge Kyela, wananchi walipuka kwa Shangwe, vifijo vyatawala

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,563
217,866
Hii ni kwa sababu kwa miaka mingi sana jimbo la Kyela limekosa mbunge ambaye ni Mkazi halisi wa Kyela , kwa zaidi ya miaka 15 Kyela imekuwa na mbunge mpita njia, Mwakyembe alikuja Kyela kuomba kura ama kuja kuzika ndugu zake na kujiondokea zake , akirudi tena basi labda kuna ziara ya Waziri Mkuu au Rais.

Kuteuliwa kwa kijana wa nyumbani , mzaliwa na mkazi kunatafsiriwa kama ni kupata ufumbuzi halisi wa matatizo ya Kyela , huyu anazijua taabu halisi za wana Kyela , baada ya ccm kuchokwa kabisa kyela ufumbuzi pekee uliosalia ni kupata mtu kutoka Chadema , ambaye ni Alinanuswe Mwalwange , Kwa miaka mingi nimeandika humu kuhusiana na matatizo na changamoto za Kyela , tena kwa kutaja vijiji na mitaa yote kuanzia Ngyekye, Matema, Kapamisya, Ngana, kasumulu, ngonga, kajunjumele hadi Katumbasongwe, hakuna aliyewahi ku challenge , hii ni kwa sababu sisi watu wa Chadema Kyela tunafahamu shida za jimbo letu .

Labda kwa wale wasiojua Kinyakyusa , jina Alinanuswe lina maana kubwa sana ! kwa tafsiri ya kiswahili maana ya ALINANUSWE ni YUKO PAMOJA NASI , kwahiyo unaweza hata kuona kwamba kumbe mgombea wetu si kiguu na njia , ni mtu ambaye yuko pamoja na wanakyela , analima nao , anadhulumiwa nao stakabadhi ghalani , si mgombea wa kuja na kuondoka , inasemekana hii ndio sababu kubwa ya watu kununuliwa bia hovyo mitaani na kusherehekea jina la Mwalwange kupitishwa na Kamati Kuu.

Tutaendelea kuwaletea habari za uchaguzi za jimbo la Kyela kwa kadri tunavyozipata .

Mungu ibariki Chadema
 
Ni mwanamke uyo? Nadhan wanawake wawe tunawaombea zaidi kwani wanaume wengi wamekuwa vigeugeu sana kwan wanaunga sana juhudi wengi wao
 
Ni wewe mwenyewe mkuu. Au ni vinginevyo.?

Kama ni wewe nakuombea upite nikuskie ukautetea upinzani kwa hoja kama za jf.

Vinginevyo, hastahili.
 
Back
Top Bottom