Harrison Mwakyembe afanya siasa za udini kanisani Mbeya

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
CCM MAHMUMU, CHALIII KIFO CHA MENDEEEE;

Ameandika Malisa J.

Tunapotafuta madaraka ya kisiasa tunatumia mbinu mbalimbali, lakini ni muhimu kutumia mbinu ambazo hazitaharibu mahusoano yetu na Mungu wala hazitadhalilisha imani ya wengine.

Mzee wangu Harrison Mwakyembe hiki unachokifanya Kyela kutumia makanisa kama "platform" ya kufanya vikao vya chama chako si sahihi hata kidogo. Sikemei kwa kuwa wewe ni CCM, hasha! Hata Mbowe angefanya hivi ningekemea pia. Tena kwa nguvu kubwa zaidi.

Mimi kama Mkristo nimefundishwa kuheshimu hekalu la BWANA. Hata Yesu alipokuta watu wanafanya biashara hekaluni alipindua meza zao na kumwaga bidhaa zao chini. Akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi (Mathayo 21:13).
_
Sasa wewe umegeuza kanisa kuwa kijiwe cha siasa. Hadi eneo la madhabahu umegeuza "high table" ya viongozi kukaa na kuzungumza na wanachama wenu? Vitambaa vya kupamba madhabahu vimeondolewa na kuwekwa vitambaa vya chama chako. Mzee wangu umelinajisi kanisa. Mbaya zaidi wewe ni Mkristo tena uliyeokoka. Tukueleweje?

Kuna maeneo mengi hapo Kyela mngeweza kukutana na kupanga mipango yenu si lazima kuipangia kanisani. Mngeweza kukodi ukumbi au mkatumia kumbi za mashuleni (sekondari na vyuo) ambazo mngeweza kuziomba na kupanga mipango yenu badala ya njia hii ya kulinajisi kanisa. Tafadhali tubu, na tafuta njia nyingine ya kukutana na watu wako. Usilazimishe hasira ya Mungu ikawaka juu yako.!

As written by Malisa J.
FB_IMG_1593860207904.jpg
 
Katika watu wanajuwa kuwachezea watu wq kyela ni Mwakyembe jamaa ni akili kubwa sana.Sema kyela mda mwingine hawana shukran ndo maana naye huwa anawaacha tu.
 
Katika watu wanajuwa kuwachezea watu wq kyela ni Mwakyembe jamaa ni akili kubwa sana.Sema kyela mda mwingine hawana shukran ndo maana naye huwa anawaacha tu.
Endelea kuwadharau watu wa Kyela , safari hii utakiona cha mtema kuni
 
Hapana tusimlaumu sana Mwekyembe, yuko sahihi, nyoka hawezi kuzaa mbuzi, wala huwezi kupanda mahindi ukavuna machungwa. Tulimsikia mwenyekiti wa chama chake akitamni kuwa kiongozi wa malaika, haikutosha sana wapambe wake wakamuita yesu. kwa hiyo huwezi kuitwa yesu halafu watoto wako wasifanyie vikao kanisani.
 
Mwalimu Nyerere alisema kwenye kipindi kama hiki cha uchaguzi kuna wale watu ambao wakishindwa kupata kura kwa sera basi watatumia dini.
Naona Mwakyembe yupo kanisani na Wakiristo wenzie akinadi sera zake, Sijui waislamu nao wanaweza kuhudhuria humo kanisani ili wasikilize sera za mheshimiwa? au watashindwa maana watapewa wakati mgumu kuingia kwenye nyumba za ibada za watu wengine lakini huku wakiwa na shauku ya kumsikiliza mheshimiwa wao!.

Mfumo kristo eventually sasa hauoni aibu unaanza kujionyesha waziwazi bila hofu
 
Kyela wanasifika dharau na misimamo lakini kwa Mwakyembe wamepatikana ......
 
Anafuata mfano wa mwenyekiti, kila jumapili akienda kusali basi anatumia ibada hiyo kama platform ya kupiga siasa.
 
Nimesoma andiko la kaka yangu malisa kwa makini sana nione msingi wa tuhuma zake kwa mwakyembe nikaishia kuona porojo za kisiasa tu...malisa wewe ni mkristo,tuambie ni andiko gani linaloharamisha siasa kufanyikia mahala pa kukutania ambapo wewe umepaita 'kanisa' ingawa kanisa ni kitu kingine kabisa?...yesu mwalimu wetu mkuu alifanya siasa popote na kama hujui yesu kristo alikuja na agenda moja tu 'kuusimika ufalme(serikali) wa MUNGU Duniani na alitumia eneo lolote kuwakosoa watawala,makuhani,wandishi n.k (that was politics)..sasa kaka yangu unapolialia mtoto wa kiume tena ukijaribu kumshambulia mwakyembe kana kwamba kafanya dhambi tena unajaribu kutumia kisa cha yesu hekaluni kupindua meza ambapo unapaswa uketishwe chini upewe darasa kuhusu nini yesu alikataa pale hekaluni unlike wewe unayeunganisha two unlike things..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom