Dakta Mwakyembe lete porojo nyingine!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dakta Mwakyembe lete porojo nyingine!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Divele Dikalame, Mar 18, 2011.

 1. D

  Divele Dikalame Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  * Kwa nini isiwe John Kony au Intarahamwe?

  Jambo ambalo pengine lilitarajiwa ni kuwa kwa msomi kama Dr. Harrison Mwakyembe, hata kama ni porojo au usanii, basi angalau ungekuwa wenye kufanana na ukweli na unaotoa majibu na kufukia mashimo badala ya kuacha maswali yasiyojibika.

  Tunaambiwa kuwa upo mpango wa kumuuwa Mheshimiwa Dr Harrison Mwakyembe. Na katika taarifa yake kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari, Mwakyembe anaonesha kuwa ameujua mpango huo, lakini anatoa na maelezo marefu na msururu wa wahusika ukijumuisha raia, polisi, Idara ya Usalama ya Taifa, watendaji wa serikali na magaidi wa kukodiwa kutoka Somalia.

  Undani na upana wa maelezo yanayotolewa, yanamuacha msomaji akibaki na jambo moja la uhakika. Kwamba ama hiyo ni kazi ya "counter-intelligence" au "Parallel system."


  Lakini labda tuanze kwa kuangalia nukta zifuatazo, kwanza waliotajwa kuwa katika kikosi cha mauwaji wote ni Waislamu. Ametajwa Hassani, Mustafa kutoka Uganda na raia wawili wa Somalia ambao ni Hafidh na Faraj. Wengine ni Mustafa a.k.a "Master" Mkusa na Ramika anayedaiwa kuwa mtaalamu wa kukaba watu na Rajabu Mtiula. Lakini pia inatajwa kampuni ya Caspian na kushereshwa na mwandishi kwamba mwenye kampuni hiyo ni Rostam Aziz.

  Pili, inatajwa kwamba katika harakati za kupanga mauwaji, kikosi cha mauwaji kilipoingia Dar es Salaam kilishukia "Kiwalani karibu na Kiwanda cha Mohammed Enterprises." Ikaelezwa kuwa "jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa, chini ni Msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz (Markaz) na juu ni sehemu ya kuishi."

  Labda tuulize, kilichoelezwa hapa nini? Unaposema kikosi cha mauwaji kilishukia karibu na Kiwanda cha Mohammed Enterprises, unachokusudia nini? Kuonesha uhusiano wa watu hao na mwenye kiwanda au! Lakini huishii hapo, unasema, jirani kuna Msikiti wa Waarabu ambao sehemu ya juu yake ni sehemu ya kuishi, kwa maelezo yote haya na jinsi yanavyounganishwa, kinachokusudiwa kuoneshwa hapa nini? Lakini labda tuache kwanza hilo.

  Taarifa ya Mwakyembe inadai kwamba wauwaji waliofikia (Msikitini) Kiwalani waliungana na wengine waliotokea Uganda na kupokewa na polisi kisha siku hiyo hiyo wakafanya kikao na "magaidi" wa Al Shabab. Wauwaji hao wanaoneshwa pia kupata msaada kutoka Mako Makuu ya Polisi Dar es Salaam na Idara ya Usalama wa Taifa kwa Idara hiyo kumruhusu afisa wake Mustafa "Master" kushiriki katika mpango huo.

  Gazeto la THE CITIZEN la Ijumaa tarehe 11 Machi, 2011 likiarifu kuhusika kwa usalama wa Taifa katika jinai hiyo likasema "The Tanzanian Police Force is still investigating claims made by the deputy minister for Works, Dr Harrison Mwakyembe, that there was a plot by the national intelligence, police and Al Shabab militia to assassinate him along with other prominent politicians."

  Lakini labda tuulize, hivi Usalama wa Taifa na hata Polisi na timu yao ya makachero wakiamua kumshughulikia mtu, vinahitaji mlolongo wote huo mpaka wa kwenda kutafuta msaada kwa waganga wa kienyeji Songea na wauwaji wa kukodi kutoka Somalia?

  Tunadhani pamoja na usomi wake, Mwakyembe amekuwa msanii ambaye hakufanikiwa. Amekuwa sawa na wale walioibuka na kiroja cha mtoto wa shule ya msingi kupenya ngome ya ulinzi wa ubalozi wa Marekani, akiwa na mabomu yake ya kulipua ubalozi huo. Na ndio maana sisi tungependa kumsaidia Naibu Waziri wetu huyu wa Ujenzi Mheshimiwa sana Mwakyembe kwa kumwambia aje na porojo nyingine. Lakini tumwambie pia kwamba, alipopalenga tumepaona. Tutafafanua.

  Mwakyembe anasema kuwa amekusanya taarifa zinazodai kuwa "awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka wanaharakati wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho (Al Shabab) kikashawishiwa."

  Kwa nini Mwakyembe asukiwe mipango ya kuuliwa kwa kutumia kikosi cha Al Shabab? Mwenyewe anajibu, anasema, "mimi na wenzangu watano (Reginald Mengi, Waziri Benard Membe, Anne Kilango, Dr Wilbrod Slaa na Profesa Mark Mwandosya) tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu."

  Hapa ndipo kwenye habari ambayo kwa hakika si habari kitu bali usanii na porojo. Yale yote yaliyoelezwa ikiwa ni pamoja na "details" za nani alikuwa wapi, Safari ya kwenda Songea kwa mganga wa kienyeji, nani alikwenda wapi na katumia gari gani na kapokelewa na nani, ni mapito tu. Lakini habari ipo katika nukta nne, zilizoainishwa hapo juu ambapo majina ya wauwaji wanatajwa, uhusiano wao na baadhi ya matajiri wa Kiislamu na Misikiti wanamoshukia.

  Tunavyojua sisi, Mwakyembe ni katika watu waliokuwa wakitajwa na kusifiwa kwamba ni wapiganaji na makamanda katika vita dhidi ya ufisadi. Haikuwahi kutajwa kwamba pia ni kamanda wa maadui wa Uislamu anayetumiwa kuwapiga vita Waislamu. Hili ndio kwanza analisema yeye mwenyewe katika madai yake haya.

  Na kuonesha kwamba yeye si mtu mdogo katika kikosi hicho cha watu wanaotumiwa na Kanisa kuhujumu Uislamu, imeonekana kwamba wale Interahamwe walioangamiza mamia ya maelfu ya roho za Wanyarandwa hawatamuweza Mwakyembe na mapanga yao. Ujuzi wao wa kuuwa ni ndani ya Rwanda tu.

  Itakumbukwa kwamba hawa Interahamwe ndio waliotumiwa na baadhi ya Maaskofu na Mapadiri kufanya mauwaji ya Kimbari. Sasa pengine ambacho Mwakyembe hakukisema ni kuwa wauwaji wa Rwanda walioshirikiana na Maaskofu kufanya mauwaji ya kuangamiza, hawawezi tena kutumiwa kuwadhuru ‘mawakala' wanaotumiwa na Kanisa kuhujumu Uislamu.


  Ziliwahi kuandikwa habari katika baadhi ya magazeti hapa nchini kwamba kulikuwa na magaidi wameingia nchini kuwinda wanyama katika mbuga zetu ili kuwapelekea kitoweo Al Qaida walio katika kambi za mafunzo huko Afghanistan. Kilichooneshwa katika habari ile ni kwamba magaidi walikuwa wanaingia nchini hapa wapendavyo, wengine wanajiingiza katika biashara ili wapate fedha za kufadhili vitendo vya kigaidi na wengine wanahemea kitoweo kwa ajili ya wenzao waliopo katika milima ya Kandahar.

  Maadhali kwa wakati ule habari ile ilikusudiwa kuwapaka matope Waislamu na kujenga mazingira ya kuwahujumu, serikali na vyombo vyake vya usalama vilimeza matusi na habari ile ya kuidhalilisha. Ilikaa kimyaa!


  Sasa Mwakyembe anadai kuwa Al Shabab wameingia mjini. Wamekaa watu hapa, Watanzania wenzetu, wamepanga, wamekwenda Somalia kukutana na Al Shabab na kurejea na kikosi cha mauwaji. Na kikosi hicho kimetumia magari ya serikali kwenda Songea kwa mganga wa kienyeji na sehemu nyingine mbalimbali huku wakipata usaidizi wa polisi na usalama wa taifa ili kumuuwa Mwakyembe, Reginald Mengi na Dr Slaa. Halafu polisi wanasema wanachunguza! Hiki ni kiroja na porojo nyingine ambayo tafsiri yake ni kuwa vyombo vya dola vimeshiriki katika igizo hili mithili ya vile vichekesho vya King Majuto. Maana hata Mzee Kipara, Onyango na Bi Nyakomba wana afadhali.

  Ufupi anachosema Mwakyembe hapa ni mambo mawili: Ama serikali ndiyo iliyoandaa mpango huu wa kumuuwa au sio serikali, lakini watu ndani ya Idara za Usalama waliokodiwa na wafanyabiashara maarufu kama linavyoarifu gazeti la The CITIZEN.

  Habari hii inakwenda mbali zaidi na kuleta jambo la hatari katika nchi. Anachosema Mwakyembe ni kuwa Waislamu wamewaalika Al Shabab kupambana na ‘watumishi" wa Kanisa kama yeye. Na katika madai hayo, wanaingizwa "wanausalama" Waislamu. Hii ni sawa na kupandikiza fitna na farka baina ya "wanausalama" Wakristo na "wanausalama" Waislamu. Pili, anajenga chuki baina ya Mawaziri Wakristo kama yeye (pamoja na watumishi wengine wa serikali) na Mawaziri Waislamu. Na tatu, katika ujumla wake, chuki na fitna miongoni mwa wananchi.

  Namna yake anawarai na kuwakusanya Wakristo waunganishe nguvu kupambana na hawa Waislamu walioingiza wanamgambo wa Al Shabab kupambana na Wakristo akina Mwakyembe na Mheshimiwa Waziri Membe. Na kiufundi Mheshimiwa Membe ameingizwa kwa sababu amekuwa akitajwa katika makongamano ya Waislamu kuwa alibadili msimamo wa serikali kutokana na maelekezo ya Kardinali Pengo. Anachofanya hakuna tofauti na kile walichofanya waliobuni Interahamwe kule Rwanda.

  Interahamwe ni neno la Kinyarwanda ambalo maana yake kwa Kiingereza ni "those who fight/attack together." Yaani wanaosimama/wanaoungana kushambulia pamoja. Na katika mauwaji ya kuangamiza ya Rwanda, hawa walifanya mauwaji bega kwa began a baadhi ya maaskofu na watawa wa kike (ma-sister) wa Kikatoliki.

  Katika taarifa moja-"
  The Cross and The Genocide: The Involvement of the Christian Societies in the Rwanda Genocide", lipo swali moja la msingi anajiuliza mwandishi, anasema: "How could God fearing nuns, and even a bishop, take part in the most cruel crimes against humanity committed on African soil? Even worse, several church societies allegedly were co-responsible for the growing hatred that led to the genocide. It remains an enormous contradiction to the Christian Message of Love."

  Kwa maana kwamba ni jambo la kushangaza ilikuwaje maskofu, wanaojiita watu wa Mungu kushiriki katika jinai hii ya kikatili ambayo inakwenda kinyume kabisa na ujumbe wa upendo unaodaiwa kufundishwa katika Ukristo?

  On 7 May 1994 soldiers and militias arrived at Shyogwe Diocese aboard a red pick-up vehicle to transport civilian Tutsi refugees to the killing sites. "On that day Bishop Samuel Musabyimana was present and, addressing the soldiers and militias, publicly stated that he did not oppose the killing of Tutsis, but that he did not want killings at the Diocese and that the Tutsis should be taken to Kabgayi to be killed." (Indictment by the International Criminal Tribunal for Rwanda against former Anglican Bishop Samuel Musabyimana).

  "Teacher, which is the great commandment in the Law?" And He said to him, "You shall love the Lord your God with all your heart, and with all your soul, and with all your mind. This is the great and first commandment. And a second is like it, you shall love your neighbour as yourself. On these two commandments depend all the Law and the Prophets."
  (Matthew 22:34-40).

  On 22 April 1994, Séraphine Mukamana had hidden herself in a garage when militias attacked a convent in Sovu in southern Rwanda. "We sought refugee in the garage and closed and barricaded the doors. Outside a bloodbath is going on. Suddenly an orphan begins to weep as it gets to hot in the garage. At once, the killers approach the garage." As the refugees refuse to come out, the militia leader Emmanuel Rekeraho decides to burn them alive in the garage. "'The nuns are coming to help us. They are bringing gasoline,' I heard [Rekeraho] say. Looking through a hole that the militiamen meanwhile had made in the wall, I indeed saw Sister Gertrude and Sister Kisito. The latter was carrying a petrol can. Shortly upon that, the garage is set on fire." Testimony against two Catholic nuns, Sisters Gertrude and Maria Kisito in a Brussels court, May 2001.

  Sasa labda tuulize, anaposimama kiongozi mwandamizi ndani ya serikali na kudai kwamba wafanyakazi wenzake ndani ya serikali wameungana na kuandaa njama za kuwadhuru wafanyakazi Wakristo ndani ya serikali, maana yake nini? Hii si sawa na kuwachochea Wakristo wenzake waungane kupambana na Waislamu?

  Katika madai yake, Mwakyembe anawaunganisha Waislamu wa mitaani, wafanyabiashara wakubwa Waislamu na watendaji wa serikali, katika njama hii ya kumuuwa yeye kama "Wakala wa Kanisa" ndani ya serikali. Sasa hii kinyume chake, ni kuandaa "Interahamwe" ya Wakristo. Kwa maana ya kuwaunganiusha Wakristo wa mitaani, katika vyombo vya dola n.k. kupambana na Waislamu.

  Serikali ya Marekani ilipotaka kupitisha ile sheria ya kijambazi na kidhalimu Patriot Act, ilikuja na kitisho cha ugaidi wa kimeta (Anthrax Terror Attacks). Watu walitumiwa barua zenye unga wa kimeta ambapo saba walikufa. Waliotumiwa barua hizo walikuwa ni pamoja na…Na kisha habari zikasambazwa kwamba waliokuwa wakifanya shambulio hilo ni akina "Hafidh" wa Al Qaida. Na ili kuthibitisha hilo, barua zilizodaiwa kutoka kwa Al Qaida zikawa na maneno ya Kiarabu kama Allah ili kujenga hoja kwamba kweli walioandika ni Waislamu. Lakini Mwakyembe anajua kama wanavyojua akina Manumba aliowapelekea taarifa zake za kutaka kuuliwa kwamba kimeta kile kilitengenezwa na kusambazwa na makachero wa serikali ya Rais Bush kwa lengo la kuwatisha wananchi na wabunge ili wapitishe ile sheria aliyoitaka Bush.

  Sasa si ajabu kwa Mwakyembe kuja na porojo hizi za akina Hafidh na……kutoka Somalia na mlolongo huu wa waigizaji wanaotumia magari ya serikali. Ila tu tunachosema ni kuwa hoja iliyopo mezani hivi sasa ni juu ya "Mfumo Kristo" unaiotishia amani ya nchi hii.
  Tunachowataka akina Mwakyembe ni kujibu hoja za msingi, kwa nini mpaka sasa serikali haijasema chochote kuhusu ile Tume ya Majeshi ya Kivita (Commission of Armed Forces" ya Kanisa Katoliki? Tume hii kazi yake nini? Je, inafanya kazi ndani ya Jeshi letu (JWTZ) au ndani ya Kanisa? Tume hii inatofautiana vipi na wale Iterahamwe waliotumiwa na Maaskofu kuchinja watu kwa mapanga Rwanda? Hizi ndio hoja za kujibu, sio hizi porojo za Al Shabab.

  Waislamu wanauliza, inakuwaje serikali ikusanye kodi kutoka kwa wananchi wote, Waislamu na Wakristo, halafu irudi ikae pembeni na Wakristo pekee kupanga mipango ya kwachotea Wakristo fedha peke yao? (Rejea MoU). Wanachotaka Waislamu ni majibu na kubwa zaidi kukomeshwa udhalimu huu na kulipwa fidia. Sasa Mwakyembe asidhani kwamba atawatoa Waislamu katika agenda hii kwa kuja na usanii huu wa akina "King Majuto."

  Waislamu wanao ushahidi jinsi watoto wa Kiislamu walivyokuwa wakikatwa majina yao na kunyimwa nafasi za kupata elimu ya juu. Tunachotaka ni akina Mwakyembe kusema na kupeleka hoja Bungeni ama serikalini kuwataka Waislamu walete ushahidi wa madai yao. Huu ndio utakuwa uzalendo na neno la uhakika la kusaidia amani ya kudumu ya nchi hii. Huu usanii wa Al Shabab na makazi yao jirani na kiwanda cha Mohammed Enterpises Kiwalani, ni kutaka kuendeleza dhulma na mfumo wa kibaguzi ambao kwa miaka 50 umekuwa ukiwadhulumu Waislamu.

  Serikali na vyombo vyake vya usalama hapana shaka kama vilivyoombwa na Mwakyembe vitakuwa na namna yake ya kulishughulikia suala hili. Lakini sisi tunadhani hatuna sababu ya kuhangaishwa na Mwakyembe. Wa kushughulika naye ni huyu anayepiga zumari Mwakyembe akicheza pamoja na wale aliowataja katika mlolongo wa madai yake.

  Kama kipo cha kuwashughulisha Waislamu, ni huu mfumo anaoutumikia Dr Harrison Mwakiyembe. Mfumo ambao hauoni vibaya kutukanwa na kudhalilishwa kwamba kuwepo kwake hakuna maana yoyote linapokuja suala la usalama wa nchi. Usalama wa nchi utakuwaje na maana iwapo unaweza kuwepo ukiwa na kila aina ya mbwembwe na vitendea kazi, lakini wanaweza wakapenya "magaidi" na kupanga mipango ya mauwaji bila ya wao kuwa na habari mpaka atoke mtu Kyela kuja kuwastua?

  Sasa huu mfumo ndio wa kuwashgulisha Waislamu. Sio hawa ambao inaonekana wao na wale Interahamwe washirika wa Maaskofu wanaweza kuwa ndugu moja
   
 2. b

  banyimwa Senior Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huu ni upotoshaji uliovuka mpaka na kuanza kuitumia hoja ya kidini ku-trash hii complaint ya Mwakyembe, tena hii inafanyika wakati Polisi wanafuatilia. Huyu mtu amefanya juhudi kubwa sana kutetea kitu ambacho hakina msingi.

  Brother, utake usitake, hii ni mipango ya kihalifu na haina uhusiano na dini hata kama waliotekeleza mpango huu ni wahalifu wenye majina ya kiislamu. Je, huyo Fred aliyetajwa ni muislamu. Hivi siyo vita vya kidini. Ni mapambano dhidi ya wahalifu wenye nia ya kuteketeza wenzao ambao wana nia njema na mapenzi kwa nchi hii.

  Mimi ni Muislamu lakini hata siku moja sijawahi kuwa mateka wa fikra mgando kwamba waislamu wote ni safi na kwamba wakristo wote ni wachafu kwa sababu tu ya imani yao. Ndiyo kwa stahili hii hii gazeti moja lilimtetea Rostam eti tu kwa sababu ni muislam. Wanapoiba na kupora hawafanyi hivyo kwa manufaa ya uislam na wala hawagawani na waislam wenzao.

  Suala hapa ni kwamba kama taarifa ya Mwakyembe ni ya uongo basi utolewe ushahidi wenye kuonyesha uongo wake na siyo kujificha kwenye kichaka cha dini ili kuficha uovu wa wahusika.
   
 3. k

  kajembe JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 755
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Sikuelewi jambo unalolielezea, kumbe wakristo wana Jeshi! Waislam walifaulu vizuri labda div one majina yao yakakatwa! Waislam walijenga shule zao Nyerere akazitaifisha!

  Wewe unaleta uchochezi tena mbaya sana na Damu ya watanzania ikimwagika ujue ipo siku utatoa hesabu yake mbele za Mungu, sisi tunapigika na maisha sababu ya CCM wewe unatuambia habari za udini, mimi ndugu zangu wengi waislam wala hatugombani wala kubaguana ninyi ni wapi mnapobaguana?

  Au unajribu kutuvuruga ili tuache adui wetu wa kweli CCM tuanze kugombana sisi kwa sisi! Hautafanikiwa ndugu yangu tatizo letu sio dini bali ni umaskini, wizi wa mali ya umma, huduma za hovyo za hospitali, shule za kata tulizojemgewa sisi walala hoi bila kujali dini na njaa na tunakufa na njaa, halafu wewe unatuambia habari za udini.
   
 4. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Duh huyu jamaa sijui ana Mania? Huwezi andika gazeti zima halafu utumbo. Inahitaji uwe na nguvu za kichaa kuandika utumbo wote huu.

  Mwandiko mzuri, akili mbofu.
   
 5. k

  katundu Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuna mambo makuu ya kujiuliza: ni kwa nini mara nyingi mtu akiambiwa ni mkristu hapigi kelele lakini waislam ni kulalama tu?

  Niambie ni sehemu gani waislam wamefanikiwa kuwa na maendeleo ya elimu maana badala ya kujenga shule wanajenga misikiti tena kwa kudharau serikali maana wanajenga miskiti barabarani. Niambie pia wapi uliona hospitali ni nzuri ni ya kiislam? Yote hayo ni mapungufu ya waislam japo sisi hatuitaji kabisa kuingia kwa undani.

  Mwakyembe kaisaidia sana polisi, ni wao kufuatilia. Ndugu yangu kaa chini ufikirie si kuandika maneno mengi sana ambayo mimi naona ni upupu.

  Badrika. Fikiria elimu kwanza. Dini yenyewe inakwenda mrama angalia nchi zote za kiislamu ziko vitani, wanapigana wao kwa wao. Mkwere anawapotosha maana hata yeye ukimwuliza tofauti ya good governance na management hajui.

  Poleni sana
   
 6. U

  Ugweno Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli nyani haoni kundule!umetumia nguvu nyingi kumpinga Mwakyembe kwa udini kwa kupalilia udini!!!!umaskini wa akili mbaya sana,achana na udini rafiki yangu kutumia nguvu zako kuwakomboa kiuchumi ndugu na jamaa zako
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ACHA POROJO WEWE MWENYEWE JUU YA WAPIGANAJI WETU UHAI HAUNUNULIWI DUKANI!!!

  Wewe unaona kwamba Dr Mwakyembe anadanganya je anafanya hivyo ili akapate nini cha zaidi???

  Kama ni usomi kafikia kilele, mwasheria mashuhuri, kisiasa tayari ni waziri, darasani tuliofundishwa naye wala usipime, umahiri katika tasnia ya uandishi wa habari labda ukawaulize akina Mabere Marando au Hashim Mbita wakupe darasa juu ya huyu mtu, rushwa hachuku, vyuo vikuu vyote vinamkubali na kwa wapiga kura sisi vijana usiseme ... ehe porojo ya nini tena hapo??

  Uhai hainunuliwi dukani wala kuwekewa viraka kama fundi cherehani na nguo kuu kuu, kamwambie aliyekutuma kushambulia WAPIGANAJI WETU kwamba muda umekwisha wa majungu; hapa ni vita mbele tu!!

  Ehe, lete porojo mwenyewe juu ya mpiganaji mwingine; mchafuo wako wa pili utakua unamlenga Samuel Sitta aka 'Shimita wa Siasa' au wamekuagiza ukamwage takataka zako kwenye kichochoro kinachoitwa Dr Slaa au CHADEMA??

   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  LOWASSA'S LONG-DEMONTRATED 'DOMINANT CHARACTER' HASTE AND GREED ON EVERYTHING IS SOON GOING TO TAKE 'THE LAST BREATH OF CCM'

  UVCCM meeting will be both such a crucial turning point and game-changer for the ruling party's seldomly remaining political fortunes befall an ultimate BIG BANG given the most dangerous levels of 'private' zeal, haste and greed that CGH Edward Lowasa is currently championing!!!

  Further analysis of what may follow after staring at post namber 13 MUST be considered by using twoo most reliable tools (i. SWOT-Analysis of the CCM of and a Lowassa the corner ...

  ... ii. a critical look of the entire circle of group formation - shared purpose, structres and direction in relation to the many phase of CCM under 1. Group Formation stages, 2. Group Storming, 3. Group Norming and the 4. Worst scenario Group Re-Calling stage) pale ndani na utajua kwa nini imekua necessary kutumika RUGARUGA MARCENARY kama Zitto Zuberi Kabwe, Kufulia, Mrema, Cheyo na ili vita vya mle ndani vishindwe kiaina.

  Hakika ndani ya CCM kuna janga kubwa kuliko watu tunavyoweza kufikiri. Kule Dodoma itakua mchezo wa ama 'all fisadi system go or none', yes, your guess is just as good as mine, it will be a MAKE OR BRAKE between the UVCCM Have-Not-Progressive verses the UVCCM Well-to-do Political Heathens at play.

  Go, go Benno Malisa, go!! Kuna wakati pesa hukosa thamani pale uadilifu unapojitokeza kuwa ndio bidhaa inayosakwa kote sokoni.

  Go Malisa never be afraid of the cantankerous and the political banes in the picture of Lowassa, Nchimbi, Rostam Aziz and any other, go Malisa!!
   
 9. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,393
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  mwambie huyo aliyekutuma kakosea kidogo.sababu kachagua mtu mwenye akili mgando. hivi mtu bado unafikiria udini dunia ya sasa hivi badala ya kuwaza jins ya kupambana na umaskini wako ambao mkwere alijibu kwamba hajui kwa nini wewe ni masikini.
  :target:
   
 10. D

  Divele Dikalame Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ok majibu kwa Mwakyembe yataendelea kesho tukijaaliwa, mbarikiwe nyote.
   
 11. M

  Mr CarryFoward Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  Kuweni OPEN-MINDED NYINYI, tatizo lenu mkiambiwa UKWELI mnawaka!

  Kitu gani kinachowafanya muamini maneno ya Mwakyembe na mukatae haya? Toeni hoja, msipinge tu kwa chuki binafsi.

  Tunachosema ni kwamba hii porojo ya Mwakyembe ni CATHOLIC CHURCH PROPAGANDA. Nchi hii inatawaliwa na MFUMO KRISTO ulio simikwa na maluuni NYERERE, mfumo ambao umekosa wadhamini ndani ya serikali ya sasa na ndio maana alie kuwa PADRI mmoja, sasa ni mwanasiasa, anataka nchi hii ISITAWALIKE.
   
 12. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Umenakili gazeti la An-Nuur halafu hujaadmit kunakili. Si ustaarabu.

  Acha kuwaza dini japo dakika moja ili utafakari mambo kama yalivyo upate perspective tofauti na mawazo mgando yaliyokuzunguka kila wakati. Pitia matoleo yote ya gazeti hilo uniambie ni lini liliandika kitu chochote kama kilivyo pasipo kuingiza udini.

  Mie Mkristu na nitakwambia kitu kimoja kuhusu Ukristu. Ukiondoa wajinga wachache kama wewe tulionao katika imani yetu huwa hatuna muda wa kuogopa dini gani inamiliki nini kwa kuwa hatuamini kufanikiwa kuifikia pepo kwa kushambulia dini nyingine.

  Kuhusu majina ya vijana wa kiislamu kuondolewa kujiunga na elimu ya juu hiyo ni bull shit na unajua hilo. Sijui unatokea upande gani wa muungano lakini Sehemu kubwa ya bara watu wanatafuta elimu popote kama Koran tukufu ilivyoagiza. Baadhi yao wanasoma katika shule zinazomilikiwa na kuendeshwa na makanisa kwa kuwa zinatoa elimu dunia safi isiyojali dini ya mtu.

  Unadhani kwa nini Makamba anataja sana vifungu vya Biblia? Ni kwa sababu alisoma shule ya kanisa na akavutika mwenyewe kupenda maandiko yake na bado hajabadili dini.

  Akili kama zako na za An-Nuur ndo zinawafanya msiendelee kufikia elimu ya juu. Kinachohesabiwa pale ni credits bila kujali dini. Kama una watoto wapeleke shule nzuri inayoonekana kutoa elimu nzuri halafu subiri matokeo yao katika mitihani ya taifa halafu nitafute kama utakuwa bado na mawazo mgando uliyonayo.

  Kukaa vijiweni full time na kufungia watoto wa kike ndani hakuwapi nafasi ya kufikia ukomo wa uwezo wao kitaaluma. Give them a chance and believe me you will be surprised! Hata hao mafisadi unaojaribu kuwatetea kwa udini uliza watoto wao wanasoma wapi ndo utajua siri ya urembo. Shule za kata nyingi bado hazijafikia kiwango na zinatudhuru wote pasipokujali dini. Makanisa yanajitahidi kuruhusu watu kusoma bila kujali dini zao kwa kuwa ukisoma hata habari ya chuki za udini hupungua kwa kuwa unakuwa na mwanga wa kuona zaidi ya maisha ya dini. Tatizo usiposoma elimu dunia unadhani kuna Mungu pekee katika kuishi kumbe na Kaizar yupo na hata vitabu vya dini vimejitahidi kuelezea hayo. Mungu mwenyewe ameruhusu kuwepo tawala bila kujali zinaabudu kwa dini gani.

  Nikipata nafasi nitakuja na ufafanuzi zaidi maana katika vitu vinavyonichefua ni kuona mtu hajishughulishi halafu anasubiri serikali impendelee kwa kuwa tayari watu wa dini nyingine wamepewa nafasi. Unadhani mwanao ataingia kusoma Muhimbili na A ya Elimu ya Dini wakati amefail Biology, Chemistry, Physics nk. ambayo ni muhimu kwa madaktari na wauguzi?
   
 13. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,751
  Likes Received: 6,022
  Trophy Points: 280
  Nakuuliza mwanzilishi wa thread: Suala hapa siyo dini ya mtu ila kama wahalifu waliamua kukodi Al-Shabaab, hivi unategemea ndani ya hilo kundi (Al-Shabaab) ukute watu wa dini gani. Vivyo hivyo na vingine vingi vilivyozagaa duniani kote na baadhi vikifadhliwa hata na serikali mbali mbali kwa malengo wanayoyajua wao.

  Kwa taarifa yako, Pakistan peke yake kuna vikundi zaidi ya 47 vya kigaidi na serikali ya KIISLAMU ya Pakistan inatambua hilo na inapambana nao kila uchao halafu wewe mndengereko sijui wa wapi unajifanya kuujua uislamu kuliko huko ulikoanzia. Vikundi vyenyewe (vya Pakistan tu) ni hivi:

  Lashkar-e-Omar (LeO), Sipah-e-Sahaba Pakistan (SSP), Tehreek-e-Jaferia Pakistan (TJP), Tehreek-e-Nafaz-e-Shariat-e-Mohammadi, Lashkar-eJhangvi (LeJ), Sipah-e-Muhammad Pakistan (SMP), Jamaat-ul-Fuqra, Nadeem Commando, Popular Front for Armed Resistance, Muslim United Army, Harkat-ul-Mujahideen Al-alami(HuMA), Hizb-ul-Mujahideen (HM), Harkat-ul-Ansar (HuA, presently known as Harkat-ul Mujahideen), Lashkar-e-Toiba (LeT), Jaish-e-Mohammad Mujahideen E-Tanzeem (JeM), Harkat-ul Mujahideen (HuM, previously known as Harkat-ul-Ansar), Al Badr, Jamait-ul-Mujahideen (JuM), Lashkar-e-Jabbar (LeJ), Harkat-ul-Jehad-al-Islami(HUJI), Muttahida Jehad Council (MJC), Al Barq, Tehrik-ul-Mujahideen, Al Jehad, Jammu & Kashir National Liberation Army, People's League, Muslim Janbaz Force, Kashmir Jehad Force, Al Jehad Force (combines Muslim Janbaz Force and Kashmir Jehad Force), Al Umar Mujahideen, Mahaz-e-Azadi, Islami Jamaat-e-Tulba, Jammu & Kashmir Students Liberation Front, Ikhwan-ul-Mujahideen, Islamic Students League, Tehrik-e-Hurriat-e-Kashmir, Tehrik-e-Nifaz-e-Fiqar Jafaria, Al Mustafa Liberation Fighters, Tehrik-e-Jehad-e-Islami, Muslim Mujahideen, Al Mujahid Force, Tehrik-e-Jehad, Islami Inquilabi Mahaz, Al-Rashid Trust, Al-Akhtar Trust, Rabita Trust, Ummah Tamir-e-Nau.

  Source: Terrorist and Extremist Groups of Pakistan

  Hapa hujataja vya India, Indonesia, Uchina, Ufilipino, Palestina, Ulaya, na hata Marekani kwa uchache bila kuitaja Afrika. Hivi, katika vikundi hivi unategemea wanachama wakuu ni dini gani? Kilicho dhahiri hakihitaji kuthibitishwa! Use your common sense please na acha uchochezi wa kijinga.
   
 14. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Banyimwa mimi pia muislamu safi lakini ktk haki lazima tuseme. km muislamu analihujumu taifa ,lazima alaniwe regardless ya dini yake. we are all one.
   
 15. k

  kibokogiziba Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nasikitika watoa maoni hamuelewi nini mtoa maoni wa mwanzo alilenga tujue, Mwakyembe kuhusianisha mauaji yanayopangwa kwake na msikiti ni nini? Na kutoa sababu kuwa anatafutwa kuuawa maana yeye ni mpiganaji wa kanisa ana maana gani?

  Hiyo ndiyo ajenda. Maana watu mwaongea hata ambayo hamyachuji. Kwa mujibu wa uislamu dini ni bora kuliko huo uchumi na wala haina usawa wala ulinganisho na chochote, kama wewe dini ni sehemu ya kupumzikia kwa waislamu ni mfumo wa maisha, pia jueni hayo myaongeayo bila ushahidi inaonesha ni jinsi gani hamjui hata historia ya dunia kielim, Tanzania kiujumla na hampendi aguswe mumpendaye.

  Binadamu wote hukosea, kukosoana lazima, hii ina maana kama mwampenda mtu muda wowote akiwaamrisha hata baya mtatenda.

  Tupime maada na kama mtu wampenda zaidi mwambie makosa yake vinginevyo utakua ni ushabiki wa yanga na simba hata mtu akicheza rafu anasifiwa.

  Poleni sana.
   
 16. M

  Mr CarryFoward Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  Wakatoliki wanajeshi na ubalozi hapa nchini, sasa sijui nao ni nchi au vipi! Ila vikibainishwa mnakuja juu kama moto wa kifuu.
   
 17. M

  Mr CarryFoward Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 25
  Vipi kuhusu CRUSADERS, hawakufanikiwa kwa kushambulia dini zingine? Au wale sio wakristo?

  Ila jua tu nyie hamuwezi kufanikiwa bila mikono ya watawala, under level playing field you are knocked, hata round haiishi. Mshazoea kubebwa na ndio maana sasa hivi kelele nyingi.
   
 18. a

  alles JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi zote ni hasira za mipango yenu ya mauwaji kushtukiwa. Hapa hakuna hutakayempotosha tafuta jukwaa jingine.
   
 19. k

  kibokogiziba Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu yangu hongera kwa kuwaambia wenzio waache kuwaza dini. unajua bwana tatizo si lako kama uko sahihi basi majibu ya maswali haya unayo: 1.nani kakuleta duniani ? na kwa sababu gani?
  2. utakaa hapa duniani kwa muda gani?
  3.baada ya kufa utaelekea wapi? (au nini kinafuatia baada ya kufa kwako)
  4.hizo mali na uchumi ambao unauongelea zaidi utaelekea nao huko uendako baada ya kufa kwako?
  nilisoma philosophy katika moja ya vyuo vikuu, majibu ya maswali haya eti baada ya kukosekana na baadhi ya matatizo kutokua na sababu zake ndo chanzo cha kumtafuta Mungu, ok nawe tupe majibu yako , maana yatatupa picha kua wewe unaelewa utendalo otherwise wait siku utakapotiwa ndani ya kaburi utaona kua dini ingekufaa au hayo maslahi yalokugeza kibeberu wa kutukana wenzio na kujiona kua we ndo msomi kuliko wote. jioni njema mheshimiwa.
   
 20. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Kitu ambocho nimejifunza sisi waislam ni watu wa kulalama na hii inatokana na shule ndogo. Na hii tabia tumeridhi kwa mjomba wetu JK.
   
Loading...