Harmorapa , Harmonize hajui kuimba anabebwa na media

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
19,477
25,403
Bwana mdogo anayekuja juu kwenye anga ya muziki anayetamba na ngoma yake ya usigawe pasi ambay
e pia anafananishwa kimuonekano na sura kwa mbali na mwanamuziki kutoka WCB ,Harmonize ,amedai kuwa yeye ni mwanamuziki mzuri kuliko Harmonize sema tu alichelewa kutoka pia amedai kuwa hata wakiandaliwa live performance yeye na Harmonize basi atamkimbiza vibaya kama Harmonize haamini hivyo waandaliwe show aone kama anachosema ni kweli au lah

Harmorapa akaendelea kusema kuwa kinachomfanya Harmonize aonekane yupo vizuri ni media zinazo mbeba na WCB nzima yeye peke yake hajui kuimba.


Harmorapa pia alidai kuwa yeye ni team kiba damu na atafanya juu chini amshirikishe kiba kwenye ngoma zake zinazokuja .


Harmorapa pia ameendelea kung'ang'ania jina hilo na kudai kuwa halibadilishi kamwe kwa kuwa atapoteza mashabiki wake atachokifanya labda kuongeza AKA tu basi .


Harmorapa amesema kwa sasa anafanya mazoezi kwa ajili ya kuweka mwili wake uwe wa kuvutia zaidi(sexy body)uwe wa ki super star zaidi kwa kuwa yeye kwa sasa si underground tena bali ni super star hivyo basi lazima ajiweke kisupee star ili aendane na jina lake na ndio maana hata zile studio alizokuwa anaenda zamani kwa ajili ya kurecord ngoma zake haendi tena kwa kuwa si hadhi yake amewaachia underground yeye anaenda studio zenye hadhi yake


Screenshot_2017-03-05-14-00-46_1.jpg


Huyu bwana mdogo naona amesahau ule usemi unaosema fanya ufanyavyo lakini sikio alizidi kichwa .
 
Huyu nimemchoka, anatujazia server tu na habari zake za kipumbavu, kanapenda kiki kazi zenyewe hatuzioni, ww mazoezi gani unafanya huku umevaa jeans na mlegezo upuuzi mtupu.
Harmorapa ft Juma nature Kiboko ya mabisho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom