Harmonize atangaza vita rasmi na WCB

music mimi

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
441
758
Msanii aliyelelewa na kutengenezwa kwenye record label ya Wasafi, Harmonize aka Konde Boy sasa ametangaza vita na Wasafi.

Ametumia page yake ya Instagram kuishambulia show ya boss wake wa zamani aliyemtoa kimuziki Diamond Platnumz.

Harmonize ameiita show ya Diamond ni mkutano wa hadhara au mkesha wa maombi kwa sababu haukuwekwa kiingilio.

Wataalam wa mambo wanasema Harmonize amechokoza mzinga wa nyuki ajipange kupambana na mashabiki watiifu wa Wasafi ambao ni asilimia 86 ya washabiki wa bongo fleva.

Inst-image-23.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1309980

Sent using Jamii Forums mobile app
Show yenyewe hata watu 1500 hawajafika.
 
Harmonize na Diamond hawana bifu lolote kinachofanyika ni kumzima aliyesadikika ni mpinzani wa Diamond kimuziki stori zake zimeshaanza kupotea kwenye vichwa vya watu saizi ni Harmonize na Diamond wakishafanikiwa kumzima kabisa jamaa atarudi nyumbani kama alivyofanya mzee wa Lumumba yule
 
Show yenyewe hata watu 1500 hawajafika.

Ningekuwa karibu na Harmonize ningemshauri afanye kazi zaidi aachane na mbwembwe za insta. Bado anaitaji kujenga ngome imara ili kuingia kwenye vita na mababa wa bongofleva. La sivyo ataishia njiani ya safari, hizi mbwembwe hata Hamorapa alikuwa nazo na hazikumfikisha popote. Apige kazi kwanza tuone na afanye vitu vikubwa kwenye muziki kama kutoa hitsongs back to back hata kwa mwka mmoja, achukue tuzo kubwa za dunia, afanye show kwenye matamasha makubwa nje ya nchi, apate endorsements nono nk nk.
Otherwise naona anajifupishia safari yake ya muziki.
 
Watu wafupi hawaoni mbele ya urefu wa kimo Chao
Katika hi dunia ukijua kuchukuliana na watu. Hata mapungufu Yao utaona sio kitu kabisa
NB; shetani alikuwa kipenzi Cha MUNGU lakini sifa zilimpumbaza akaota KIBURI akaja kuikosa thamani na heshima hata kwa vilivyokuwa chini yake
Na logout
 
Walianza wenyewe kumkejeli kuanzia meneja wao yule mwenye manyonyo hadi chawa wao. Kuna yule Juma lokole sijui yani anamkejeli harmonize kila siku. Mwacheni na yeye ajibu wamezidi kumkejeli. Yani kundi zima linapambana na mtu mmoja. Aibu!
 
Wamechanganyikiwa tanasha kuitwa Zari jukwaan kigoma
Harmonize anawanyima usingizi haki. Yaani jeshi la mtu mmoja tu lakini anawachanganya kundi zima hadi chawa wao tena kawaambia wajikaze watazoea tu.
 
Back
Top Bottom