Harmo Rapa atimua mbio baada ya Mh. Nape kuoneshwa bastola

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Msanii Harmo rapa leo alienda kwenye kikao cha Mh. Nape kilichokuwa kinafanyia kwenye hoteli ya Protea. Baada ya kutokea sintofahamu askari/usalama alitoa bastola na kumnyooshea Nape Nnauye, tukio lile lilimpa wazimu Harmo Rappa na kujikuta anatimua mbio asijue aendako.
[HASHTAG]#HarmoBolt[/HASHTAG]
[HASHTAG]#BoltRappa[/HASHTAG]



 
Hivi huyu Jamaa aliemtolea Nape Bastola ni nani?

Yaani kabisa ndio wamefundishwa hivyo huko TISS? Yaani yeye hawezi kujenga hoja? Au anafikiri mtu mpaka kufikia hatua ile anaogopa hizo Risasi?

Kwanza kavaa jeans ya kishamba sana kapelo ya kikoromije! Wenzake wote wako smart and Busara za Hali ya juu.

Inamaana yeye Ndiye aliambiwa Kamtoe akikataa PIGA RISASI ILKUSUDI TUTAWALE BILA OBSTACLES?

Mimi kama Mtanzania sijapenda kabisa lakini uzuri wa KARMA ni kama Kioo, Haidanganyi hata ufe Leo, Itakuandama tu.

Ewe mtoa uhai kwa Bastola Amewaaibisha sana Wenzio Leo, Huyo Bado ni Mbunge na Anajua siri nyingi sana za chama na serikali huenda kuliko wewe na huyo mwenzio aliebariki matumizi ya Bastola.. mmeona Bunduki na Bastola ndio mkombozi Wenu...

Mungu Haendi Likizo.

 
Habari Wadau..

Tafadhari, Nimeiona video ambayo Nape Ametolewa bastola na mtu ambaye tumeambiwa ni Afisa wa Usalama Wa Taifa..

Ki ukweli kwa jinsi Nape alivyokipigania Chama Cha Mapinduzi si kwa Amri au kwa kuamua mtu mwenye akili timamu anaweza kufanya vile mbele ya vyombo vya habari.

Cha kusikitisha katumia nguvu mno na kujigeuza kichaa kabisa..

Naamini CCM haimdai Nape ila nape anaidai CCM kwa alichoifanyia kipindi kile imepoteza Heshima..

Na hata wakati wa kampeni Nape aliwahi kutoa kauli isiyo ya kidemokrasia kwamba "ccm itashinda hata kwa bao la mkono"..

Kama Mwana CCM nina heshima kubwa mno kwa Nape..

NINAOMBA TUMTAMBUE TU HATA KWA JINA TU YULE ALIYEMDHALILISHA ICON WA CHAMA CHETU KWA KUMTOLEA BASTOLA NA KUMSUKUMA KAMA PUNDA..(KWA ANAYEMJUA)

Nasisitiza mtu yeyote ambaye anaipenda CCM na kutambua mchango wa Nape Ndani ya CCM na hata uchaguzi wa 2015 hajafurahishwa na jambo hili.

NIMECHUKIZWA MNO KAMA MWANA CCM.

 
Jamaa anaonesha alidhamiria kuua kabisa, tushukuru Mungu tu hilo halikutokea, ukiangalia alitoa bastola kwa haraka sana na hakukua na mabishano makali kivile ya kumfanya atoe ile bastola, anyway ukombozi wa nchi hauwezi kuja ghafla toka ijumaa na hii week naona tupo kwenye njia ya ukombozi, soon tutakuwa wote tuna haki sawa na nchi yetu itafuata misingi ya haki na sheria.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom