Kuhusiana na tukio la mtoa bastola kwa nape,umakini wa wapiga picha?

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,956
Habari wana JF,
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye mada (itikadi nimeweka pembeni kwa hili).

Ni jambo la kushangaza kwani limewashtua watu wengi nchini kwa yule aliyetoa bastola kumnyooshea mh Nape moses nnauye (mb).

Mh Nape ni kiongozi na mwanasiasa wa siku nyingi ndani ya nchi hii,hasa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM na kulingana na yeye kudumu kwenye system ya uongozi ndani ya nchi hii,bila shaka yoyote ile hata maafisa karibu wengi kama sio wote wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama nchini wanamfahamu au kufahamiana.

Je kama yule afisa aliyetoa bastola ni afisa halali na alikuwa pale kutimiza majukumu aliyotumwa akose kitambulisho?

Je kama yeye hakuwa nacho,na walikuwa wameonekana zaidi ya mmoja,kama walikuwa ni maafisa usalama ni vipi hata yule au wale wenzie nao walau mmoja wao asitowe kitambulisho kile ili kumtoa hofu mh Nape,kwamba wale ni maafisa halali wa usalama badala yake atowe bastola?

Sote tunaelewa uzito wa tukio husika na kama kweli wale walikuwa ni maafisa halali wa usalama,sio siri kwamba maafisa usalama wa serikali wanapokuwa wanatimiza wajibu wao,kama ni nguvu basi sidhani ndio ile tuliyoiona pale?

Je ndugu Maulid kitenge mtangazaji nguli nchini,ana nguvu ana ushawishi gani nchini hadi aweze kwenda tena bila siraha na kukabiliana na wanaodaiwa kuwa maafisa usalama tena wenye silaha na kuwazidi nguvu,kama tulivyoona kwenye video ile nao wakamtii?

WAANDISHI NAO?

Kulikuwa na mamia ya waandishi wa habari pale protea hotel eneo la tukio na wengi wao walikuwa na camera mikononi mwao,kwa uzito wa tukio na mazingira yake,ni kwa nini hakutokea mwandishi au mpiga picha ambaye angechanganya ubongo wake na kujiongeza ili amfuatilie yule afisa,kwa mfano:

Kuhakikisha anapata picha kadhaa ikiwemo ya sura yake halisi.

Kufuatilia na kutupatia picha ya mwenendo wake baada ya tukio lile na wakati nape ana endelea kuhutubia akiwa kwenye gari,ili tujuwe kama akiendelea kuwepo au aliondoka?

Kama aliondoka basi mwandishi angepata picha mnato kadhaa au video kwamba walipanda gari fulani lenye namba kadhaa nk.

Pia kutujuza na pia wale washirika wake kama walikuwepo na ikibidi sura zao pia.

Lakini hayo yoote hayakufanyika bali wakapata muda wa kumfuatilia Harmolapa akitimua mbio ?

Ipi ingekuwa habari pale tena yenye tija kati ya mbio za harmolapa au sura ya mtoa bastola?

Badala yake wananchi tumeishia kuoneshwa clip ya picha ya video mtu mwenye kuvaa kapero kwa mgongoni akimtolea bastola mh mbunge na mnec wa CCM taifa nape nnauye?

My take:

Kwa hili waandishi wa habari wetu mmeonyesha au mmekosa umakini na kufanya uzembe ambao kama mngekuwa makini maswali wanayojiuliza wananchi lama wale walikuwa askari kweli au ni mpango maalumu ungekwisha patiwa majibu na tukawa mjadala tukiwa na ukweli kwani hata Mh mwigulu mwenye dhamana ya wizara husika angepata pa kuanzia.

Naomba kuwakilisha
 
Una matatzo ww si siri HV UNAJUA MUNKAR ALIOKUWA NAO YULE POLIS? HATA KITENGE ALIEKUWA AKIMSIHI ASITUMIE NGUVU ULIKUWA UNAMUONA JINSI ALIVYOKUWA ANAMAANSHA? NA NDIO MAANA HATA WAZIR NCHEMBA ALISEMA KWAMBA KAMA INGEKUWA UCHOCHORONI HAPAT PICHA INGEKUWAJE. SASA WW MHUSIKA ANAONEKANA VILE KWA NAPE HALAFU WW UNAMSOGELEA TENA KWA MBELE UMPGE PICHA TENA ANAKUONA KWEL? HV KUNA MTU WA KAWAIDA AMBAE ANAWEZA KUMTOLEA BASTOLA NAPEEE WEEE. WAANDISHI WAMSOGELEEE MTU ALIE MTOLEA BASTOLA NAPE KIRAHISI RAHIS KAMA UNAVYOFIKIRIA KWENYE MAKARATASI? TAFADHALI ACHA KUFIKILA KUPTIA KARATAS KUNA MUDA WA UTANI NA WA KAZ
 
Kuna watu wameiona sura ya mtoa bastola, wakiwemo Nape mwenyewe, Maulid Kitenge na wengine, kama kesi itaenda mahakamani ushahidi wao unatosha, wangapi wanavamiwa na majambazi majumbani au popote pale pasipokuwa na camera na wanatoa ushahidi mahakamani bila picha ya mtuhumiwa akifanya uhalifu?
 
Waandishi wa bongo bado sana, ukifuatilia wakati Nape anaongea nao wengi walikuwa kama washabiki vile na kuna wakati walikuwa wanamsaidia Nape kuongea yaani Nape akisema neno nao wanadakia hapo hapo.

Ndio maana tasnia yetu ya habari saa nyingine inapelekea wasomaji kugawanyika mkuu
 
Kunapolisi alimlipua bomu mwandishi wa chanel 10 mwangosi iringa nyororo picha sura na kila kitu kilionekana na bado wakasema awamjui ila waandishi walipambana mno jamaa akamahakama nazani kafungwa ata ili ni jepesi tu ila je mlenga ni kikosi kipi?maana kunavikosi aviingiliwi jamani aya yetu macho na masikio
 
Jeshi la Kulinda Ikulu (JKI)
2015-kuendelea.
Kama unabisha umesikia ikulu ikikanusha wale walivamia clouds au yule aliye mvamia Nape
Watanzania jiongezeni,
 
Habari wana JF,
Bila kupoteza muda naomba niende kwenye mada (itikadi nimeweka pembeni kwa hili).

Ni jambo la kushangaza kwani limewashtua watu wengi nchini kwa yule aliyetoa bastola kumnyooshea mh Nape moses nnauye (mb).

Mh Nape ni kiongozi na mwanasiasa wa siku nyingi ndani ya nchi hii,hasa ndani ya chama cha Mapinduzi CCM na kulingana na yeye kudumu kwenye system ya uongozi ndani ya nchi hii,bila shaka yoyote ile hata maafisa karibu wengi kama sio wote wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama nchini wanamfahamu au kufahamiana.

Je kama yule afisa aliyetoa bastola ni afisa halali na alikuwa pale kutimiza majukumu aliyotumwa akose kitambulisho?

Je kama yeye hakuwa nacho,na walikuwa wameonekana zaidi ya mmoja,kama walikuwa ni maafisa usalama ni vipi hata yule au wale wenzie nao walau mmoja wao asitowe kitambulisho kile ili kumtoa hofu mh Nape,kwamba wale ni maafisa halali wa usalama badala yake atowe bastola?

Sote tunaelewa uzito wa tukio husika na kama kweli wale walikuwa ni maafisa halali wa usalama,sio siri kwamba maafisa usalama wa serikali wanapokuwa wanatimiza wajibu wao,kama ni nguvu basi sidhani ndio ile tuliyoiona pale?

Je ndugu Maulid kitenge mtangazaji nguli nchini,ana nguvu ana ushawishi gani nchini hadi aweze kwenda tena bila siraha na kukabiliana na wanaodaiwa kuwa maafisa usalama tena wenye silaha na kuwazidi nguvu,kama tulivyoona kwenye video ile nao wakamtii?

WAANDISHI NAO?

Kulikuwa na mamia ya waandishi wa habari pale protea hotel eneo la tukio na wengi wao walikuwa na camera mikononi mwao,kwa uzito wa tukio na mazingira yake,ni kwa nini hakutokea mwandishi au mpiga picha ambaye angechanganya ubongo wake na kujiongeza ili amfuatilie yule afisa,kwa mfano:

Kuhakikisha anapata picha kadhaa ikiwemo ya sura yake halisi.

Kufuatilia na kutupatia picha ya mwenendo wake baada ya tukio lile na wakati nape ana endelea kuhutubia akiwa kwenye gari,ili tujuwe kama akiendelea kuwepo au aliondoka?

Kama aliondoka basi mwandishi angepata picha mnato kadhaa au video kwamba walipanda gari fulani lenye namba kadhaa nk.

Pia kutujuza na pia wale washirika wake kama walikuwepo na ikibidi sura zao pia.

Lakini hayo yoote hayakufanyika bali wakapata muda wa kumfuatilia Harmolapa akitimua mbio ?

Ipi ingekuwa habari pale tena yenye tija kati ya mbio za harmolapa au sura ya mtoa bastola?

Badala yake wananchi tumeishia kuoneshwa clip ya picha ya video mtu mwenye kuvaa kapero kwa mgongoni akimtolea bastola mh mbunge na mnec wa CCM taifa nape nnauye?

My take:

Kwa hili waandishi wa habari wetu mmeonyesha au mmekosa umakini na kufanya uzembe ambao kama mngekuwa makini maswali wanayojiuliza wananchi lama wale walikuwa askari kweli au ni mpango maalumu ungekwisha patiwa majibu na tukawa mjadala tukiwa na ukweli kwani hata Mh mwigulu mwenye dhamana ya wizara husika angepata pa kuanzia.

Naomba kuwakilisha

Sheria hairusu kupiga Picha wana usalama wala kuweka majina yao hadharani kwa namna yeyote ile isipokuwa ilivyoriwa...

Kitenge amefanya jambo la " kishujaa" lakini wakiamua kumtia nguvuni hana pa kuchomokea...
Mambo ya utendaji kaz wa hivi vyombo vya usalama wa kulaumiwa zaid ni waliowatuma, sio wanaotekeleza....

Kwa wanaopita jeshini wanaelewa maana ya Discipline na kutii amri .......

Ni kweli askari alikosea sana... Lakini maelekezo yalikuwaje? Pressure ilikuwaje?

Wengine wanalaum waandishi, thats nonsense... Thats all they can do.
 
basi washuru hata kwa kuonesha hilo tukio la nape kutolewa bastora mkuu nani aanze kwenda na camera mbele ya mtu kashika bastora alaf amejaa jazina eti ukampige picha wakati huo huo mtu huyo ametoka kumnyoshea bastora bosi wako ukienda wewe mganga njaaa na camera yako c ndio tutangashaa umebadirisha jina marehemu nanilii
 
Inasikitisha mikamera yote ile tunaishia kuona tu clip moja ikizunguka mitandaoni. Wengine wote walikuwa wanashoot kitu gani? Halafu tunaambiwa watu wamepitia vyuo vya journalism, shame.
 
Back
Top Bottom