Hard working woman

Hard working woman

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,714
Happy Valentines Day kwenu nyote.

Katika kusherehekea siku hii napenda kuwa na ninyi nyote na kwakua ni ngumu sana kuwa na kila mmoja physically basi naomba hapa ndani ya key board tuwe pamoja tukijadili hili.

Sitaki sana kuinglia fani ya Mtambuzi ila kwa siku ya leo ningependa kuongelea maisha ya ndani ya ndoa yale ya ukweli kabisaaa jinsi ambavyo watu wengi wanaishi ndoani na ii ni ili kuwasaidia wale ambao ni juniors kwenye hii fani ambao hawaishi kutuma Pm za kuomba ushauri.

ukweli halisi wa maisha ya ndoa umegawanyika katika mafungu tofauti tofauti kutokana na jinsi nilivyoona (from anecdote) ila naomba niongelee kundi moja tu lakini ndilo kundi kubwa kati ya makundi mengi nalo ni hili ambalo mama ndiye mwajibkaji zaidi.

kwenye maisha tunategemea baba na mama wawajibike kila mtu kwa nafasi yake ili maisha ya ndani yaendelee. lakini hali halisi haiko hivyo kabisaa...............kwani kwenye familia nyingi utakuta mama ndiye mwajibikaji na mfanyaji wa vitu nyumban hasa vinavyohusu hela.

akina mama walioangukia katika kundi hili hujikuta wakilazimika kutafuta hela zaid ili maisha ya nyumban yaende kama vile watoo kusoma, ujenzi wa nyumba na ufanyaji wa kazi za maendeleo. ilihali waume zao wao hujua kupenda tu na kucare basi.

kibaya zaid waume wanaoangukia kwenye aina hii ya ndoa kwa matendo yao mazuri hujikuta wanawaziba mdomo wake zao kwenye maswala ya fedha kiasi kwamba mama huwa anasahahu ama anashindwa kuulizia pesa ya kufanyia jambo fulan kisa tu ma love na ma care anayopewa.

sasa mama inabidi akili imkae sawa kwenye kumake things happen na asipojitahidi huyu mama mwisho wa siku huumbuka yeye.

wanaume ambao wakao kwenye aina hii ya maisha wao hujua kupenda tu, yaaani ikiwa umeangukia kwenye kundi hili la ndoa ni ngumu sana kumkuta mumeo na maswala ya kucheat na tena atakujali sana wewe, na atakusaidia kazi za ndani ikiwa inabidi na tena ni watu ambao hawaoni aibu kujipa raha na wake zao popote pale. Lakini yote hii hutumika kama njia ya kumfunga mwanamke mdomo, hivyo mama akajikuta hawazii mapungufu mengine kwa mapenzi anayopata yanamtosha kabisa.

mama hujikuta akifikiria na kubuni njia mbadala za kipato iwe kwa biashara ma kwa upatu na vikundi ili kufidia gap ambalo baba hajalijaza. na mama huyu huakikisha hashindwi kabisa kwenye anachotaka kukifanya. mathalan kama mama atataka nyumba ipakwe rangi basi utakuta hata kama kamwambia baba, baba huishia kusema lakini ni kweli mke wangu ukuta umechafuka sana ila humkuti akiingia mfukoni kutoa pesa ukuta upakwe rangi. na mama kwa kuona hapa sina haja ya kumuuliza basi hulazimika kutafuta pesa na kupaka rangi.................baba yeye huishia kusema mke wangu hongera sana ukuta umependeza.......

tena wanaume wanaoangukia kundi hili wengi hata kama ni kazi za ukweni kwa mume basi mke ndiye mtendaji iwe ni za sherehe ama misiba ama ugonjwa na baba hubaki kupokea sifa tu kwamba amefanya mambo yamekuwa.

CC snowhite, cacico mwaJ
 
Last edited by a moderator:
mwalimu, wengine working hard is like a hobby. kiukweli hata ningeolewa na mfalme wa arabuni, nahisi ningekuwa bored stiff and to the core. hata nipewe kila kitu with a gold spoon to eat from, nadhani i still need some kind of work kuweka hii kichwa sawa.

msimamo wangu ni kuwa kila mtu anahitaji kufanya kazi kama sehemu ya kujamiiana.
uwe na valentine njema.
 
well said King'asti, ni kweli kuna watu hard working ni hobby but hobby hii imeharibu wanaume wengi sana. mfano nimeangalia maisha niliyokulia mama ni mchapa kazi kuliko baba nikajiuliza ingekuwa yule mama alifunga mikono yake this story would be otherwise..............

sasa nimeangalia maisha ambayo ninaona watu wanaishi bado wamama wengi ni wachapa kazi kuliko wababa. na hapa imekuwa sasa wamezoea kuwa wavivu huku wakiwaacha wake zao kuchapa kazi na kuendesha familia.
 
Last edited by a moderator:
ukisikia mahaba niue ndo hayo......

Lakini mwl wanawake wanaoishi kwenye ndoa za namna hii toka uchumba waliliona hilo (unakuta mwanaume hagharamii hata pipi) lakini wanaingia ndoani, matokeo yake inabidi achakarike mwenyewe badala ya kuchakarika na mumewe.

Nadhani mwl inabidi kuwa na kitchen pati humu. Wanawake ambao hawapo ndoani wapeee mafunzo aina za wanaume nini cha kukubali nini cha kuepuka nini cha kushirikiana na wenza wao hadi kiondoke
 
ni kweli japo mara nyingi wababa watabisha. lakini ukiwa na strategy, unakuwa hardworking and you push your man to work hard too.

tatizo analipata mdogo wangu (baby dont read this, lol), she is hard working na anabarikiwa haswa. mume yuko busy na competition ila in a good way. mwisho wa siku wanaendelea.

ndio maana nasemaga hapa, baba aangalie familia yake entirely! alipe bills, alipe ada etc. Mama atachip in kwenye maendeleo. Kama mkitaka kununua gari na kujenga nyumba, haidhuru kama mama akatoa hela hata zaidi ya baba. kuna rafiki yake Paw aliwahi kusema ameandikisha kila kilicho chake kwa mkewe. kwa sababu ana uhakika siku mkewe akifa hakuna atakaemsumbua, ila yeye akifa anajua mkewe atasumbuliwa. na anakiri yeye na mkewe wanasaidiana maendeleo.
well said King'asti, ni kweli kuna watu hard working ni hobby but hobby hii imeharibu wanaume wengi sana. mfano nimeangalia maisha niliyokulia mama ni mchapa kazi kuliko baba nikajiuliza ingekuwa yule mama alifunga mikono yake this story would be otherwise.

sasa nimeangalia maisha ambayo ninaona watu wanaishi bado wamama wengi ni wachapa kazi kuliko wababa. na hapa imekuwa sasa wamezoea kuwa wavivu huku wakiwaacha wake zao kuchapa kazi na kuendesha familia.
 
Inaelekea watu wengi wanatoka kwenye familia yenye mama wachapakazi kweli kweli. Ingawa baba ni the main breadwinner, mama siku zote alikuwa na anaendelea kuwa mchapakazi, risk-taker, na mtu anaesaidia meli isizame mambo yakimuendea baba kombo. Ingawa siwezi kusema kuwa wazazi wangu wako so in love, lakini ni ile tu heshima ya kuwa pamoja miama karibia 30 sasa. Kwa namna nyingine nimeshuhudia kukwepa majukumu toka kwa baba kwa sababu hiyo, jambo ambalo sikufurahishwa nalo, laiti wote wangekuwa wanachapa kazi pamoja na kuungana kwenye project zao nadhani familia yetu ingekuwa mbali zaidi. Lakini inabidi nikumbuke kuwe wazazi ni binadamu pia, wana madhaifu yao.

As a new parent I hope to emulate what my mama does na kujitahidi kuwa na familia imara na bora. Msisahau kutuma message za valentine kwa wazazi!
 
ni kweli japo mara nyingi wababa watabisha. lakini ukiwa na strategy, unakuwa hardworking and you push your man to work hard too.
tatizo analipata mdogo wangu (baby dont read this, lol), she is hard working na anabarikiwa haswa. mume yuko busy na competition ila in a good way. mwisho wa siku wanaendelea.
ndio maana nasemaga hapa, baba aangalie familia yake entirely! alipe bills, alipe ada etc. Mama atachip in kwenye maendeleo. Kama mkitaka kununua gari na kujenga nyumba, haidhuru kama mama akatoa hela hata zaidi ya baba. kuna rafiki yake Paw aliwahi kusema ameandikisha kila kilicho chake kwa mkewe. kwa sababu ana uhakika siku mkewe akifa hakuna atakaemsumbua, ila yeye akifa anajua mkewe atasumbuliwa. na anakiri yeye na mkewe wanasaidiana maendeleo.

umenikumbusha kitu hapa, unaona mume imebidi amsaidie mkewe kwa kuandika mali kwa jina lake?? sasa kwann binadamu tu wasione kwamba gy kaish na gfsonwin leo hayupo hzi mali ni za mkewe?? kwan walichuma wote kwann dunia haioni kama mwanamke naye anafanya vitu??
 
Wanawake hardworking uangalie mahali anakotoka kama Rombo mashati au Rombo tarakeea huko! Sisi wanawake wa pwani asili yetu ni kujipaka hina na kushinda barazani ikauke.

Hata tusome vipi uvivu na kulalamika kazini kuacha mwiko, hata promotion inabidi tutumie shortcut ambapo ndo the only sector we are best at.

Afu wanaume wa siku hizi kauzu zaidi ya dagaaa, ukijifanya hardworking kidogo na mtoaji mbona majukumu yote anakutelekezea hapo. Utalipa ada zote, utalisha familia, utajenga, yaani ukija kustuka you are alredy 50yrs, More than 20yrs of your life umefujwa fujwa tu.

Mwenzangu ukiona mtu hatoi na wewe jikaushe kau! Kama hajigusi kujenga we jenga kwa siri, kama chakula hanunui na wewe jikaushe kau! Ada jikaushe hivohivo hata watoto wakirudishwa poa tu, mbona atalipa. Hii inakuwaga mnyonge mnyongeni! @ Mama lara kuku zikipitishwa ofisini lazima amuulize baba lara achukue ngapi na pesa yake atarudishiwa lini?

Ila kuna EXTREME CASES! za wanawake too much is harmfull

1.Wamama wa pwani! Jamani tupunguze, wajiremba wewe tu, kujishindilia midhahahabu tuuuuu, na make up za ghali sanaaa! Midera ya laki 3, miguo kabati ya milango 4 haifungi, ila kila siku wapika maharage! Wanao rafurafu. Ukipata hata mia wawekeza kwa sonara au botique.

2.Wamama wachaga! Kila senti wawekezaaa tu! Kutwa kutuma hela nyumbani kwenu. Kila siku wajenga tuuuu! Nani ataishi humo mijumba yote hiyo? Huli kwa rahaaa na kujinafasi, Hujipendezeshi, hujitreat! Kutwaaa wewe kusave na kusave tu. Kujenga kwenue, sijui nini! Khaaaaaaaa! Wanao na mumeo hawafaidi kisa unainvest!

3. Wamama Wanyamwezi na wamanyema! Kutwaaa pesa yote kusaidia nduguzo. Hata hamuendelei wewe ndo umejitwisha familia yenu mazimaaaa! Haihusu kabisaaaa. Pesa zote watuma nymbani!!!
 
Inaelekea watu wengi wanatoka kwenye familia yenye mama wachapakazi kweli kweli. Ingawa baba ni the main breadwinner, mama siku zote alikuwa na anaendelea kuwa mchapakazi, risk-taker, na mtu anaesaidia meli isizame mambo yakimuendea baba kombo. Ingawa siwezi kusema kuwa wazazi wangu wako so in love, lakini ni ile tu heshima ya kuwa pamoja miama karibia 30 sasa. Kwa namna nyingine nimeshuhudia kukwepa majukumu toka kwa baba kwa sababu hiyo, jambo ambalo sikufurahishwa nalo, laiti wote wangekuwa wanachapa kazi pamoja na kuungana kwenye project zao nadhani familia yetu ingekuwa mbali zaidi. Lakini inabidi nikumbuke kuwe wazazi ni binadamu pia, wana madhaifu yao.

As a new parent I hope to emulate what my mama does na kujitahidi kuwa na familia imara na bora. Msisahau kutuma message za valentine kwa wazazi!
dah! hii ni experience ambayo sitoka niisahau maishani mwangu, my dad used to be a king aisee. kwanza alikuwa ni mtu anayejipenda sana na hapendi tabu zaid ya starehe, my momy used to be a hard working woman ambaye alihakikisha things are happening katika each angle. she dared to risk even our lives just for the sake of hard working so as to make things happen.
 
Wanawake hardworking uangalie mahali anakotoka kama Rombo mashati au Rombo tarakeea huko! Sisi wanawake wa pwani asili yetu ni kujipaka hina na kushinda barazani ikauke.

Hata tusome vipi uvivu na kulalamika kazini kuacha mwiko, hata promotion inabidi tutumie shortcut ambapo ndo the only sector we are best at.

Afu wanaume wa siku hizi kauzu zaidi ya dagaaa, ukijifanya hardworking kidogo na mtoaji mbona majukumu yote anakutelekezea hapo. Utalipa ada zote, utalisha familia, utajenga, yaani ukija kustuka you are alredy 50yrs, More than 20yrs of your life umefujwa fujwa tu.

Mwenzangu ukiona mtu hatoi na wewe jikaushe kau! Kama hajigusi kujenga we jenga kwa siri, kama chakula hanunui na wewe jikaushe kau! Ada jikaushe hivohivo hata watoto wakirudishwa poa tu, mbona atalipa. Hii inakuwaga mnyonge mnyongeni! @ Mama lara kuku zikipitishwa ofisini lazima amuulize baba lara achukue ngapi na pesa yake atarudishiwa lini?

Ila kuna EXTREME CASES! za wanawake too much is harmfull

1.Wamama wa pwani! Jamani tupunguze, wajiremba wewe tu, kujishindilia midhahahabu tuuuuu, na make up za ghali sanaaa! Midera ya laki 3, miguo kabati ya milango 4 haifungi, ila kila siku wapika maharage! Wanao rafurafu. Ukipata hata mia wawekeza kwa sonara au botique.

2.Wamama wachaga! Kila senti wawekezaaa tu! Kutwa kutuma hela nyumbani kwenu. Kila siku wajenga tuuuu! Nani ataishi humo mijumba yote hiyo? Huli kwa rahaaa na kujinafasi, Hujipendezeshi, hujitreat! Kutwaaa wewe kusave na kusave tu. Kujenga kwenue, sijui nini! Khaaaaaaaa! Wanao na mumeo hawafaidi kisa unainvest!

3. Wamama Wanyamwezi na wamanyema! Kutwaaa pesa yote kusaidia nduguzo. Hata hamuendelei wewe ndo umejitwisha familia yenu mazimaaaa! Haihusu kabisaaaa. Pesa zote watuma nymbani!!!
lara 1 again,

yaani haya uliyoongea lara ukisema ukayafanye humo ndani wanao very soon watavimba utapiamlo. uzuri jamani mtasema hivyo hujakuwa ndani ukiwa ndai kwanza hutaelewa kumwona mwanao haendi shule kisa kakosa ada, ama hali kisa hakuna chakula na hii ndio hali halisi ya maisha ya ndoa.

muulize mama lara atakuambia kwamba muda miwngine alishindwa kuvaa vzr ili nyie msome na kula na mtibiwe na hapo so kwamba baba lara hayupo ama wamegombana hapana lkn hatoi tu.

tena ujue kwa wanwake wengi wanaojitambua kuomba hela kwa waume zao ni kitu kigumu sana sana sasa unamkuta mtu anaona kabasaa hapa pana tatizo lkn hadi uombe hela ya kutatulia why?? basi mtu kama mm siombi nafanya niwezavyo ishu ipite basiiiii. ndani ni tofauti sana na haya ambaayo huwa tunatamanai yawe hivyo
 
Last edited by a moderator:
kwa nini mwanamke ulishe mwanaume ,tena huku mjini? .mapenzi au ushamba?
hhahahaha! natamani maisha yangekuwa kama unavyodhani wewe mdogo wangu. wafikiri kuhudumia familia toka huko ni kazi ya baba?? mie nilipita kwenye familia ambayo nimeona mama ndo mwezeshaji wa kila kitu na hata ukirudisha ada mma anaumiza kichwa baba yupo na kila siku nakupenda mke wangu.............usiseme hayo kabisa.

tena unakuja kukutana na utunzaji wa familia wakwe zako wewe unajitoa kuliko hata unavyojitoa kwenu, na hapa unajua kabisa nikilega amani itatoweka na mm sitaish kwa raha basi ngoja nijitoe ili iwepo siku zangu ziwe nyingi. kwenu wakiomba hela kila siku mama sina na ukweli unakuta huna lkn ndugu wametoka huko watokako wana shida ni wa mume huwezi kuwachunia itakulazimu wale wanywe na kama wanatibiwa waende hosp ama kama ni harusi waende wakiwa wamependeza
 
Nani kama mama. Always able to make things happen.

Yeye ndie aliye take over mambo ya ada na kodi ya nyumba niliopoenda chuo. Baba ni kama ali give up baada ya mwaka mmoja. Muda wa graduation ulipofika akasema nauli hana ya kuja. Nilichukia, lakini mama alikuja. See what I mean?? Yaani mtoto wao wa kike pekee halafu nauli ikushinde kuenda graduation. Nina daddy issues as you can tell. Lakini yote yamepita, now for new beginnings in 2013. Inasikitisha mwanamme kubweteka, yaani kuwa so helpless when you are in a position of power. Sijui ni nini kinasababisha hii tabia.

Wanaiita Learned Helplessness- the condition of a human or animal that has learned to behave helplessly, failing to respond even though there are opportunities for it to help itself by avoiding unpleasant circumstances or by gaining positive rewards.

dah! hii ni experience ambayo sitoka niisahau maishani mwangu, my dad used to be a king aisee. kwanza alikuwa ni mtu anayejipenda sana na hapendi tabu zaid ya starehe, my momy used to be a hard working woman ambaye alihakikisha things are happening katika each angle. she dared to risk even our lives just for the sake of hard working so as to make things happen.
 
hhahahaha! natamani maisha yangekuwa kama unavyodhani wewe mdogo wangu. wafikiri kuhudumia familia toka huko ni kazi ya baba?? mie nilipita kwenye familia ambayo nimeona mama ndo mwezeshaji wa kila kitu na hata ukirudisha ada mma anaumiza kichwa baba yupo na kila siku nakupenda mke wangu.............usiseme hayo kabisa.

tena unakuja kukutana na utunzaji wa familia wakwe zako wewe unajitoa kuliko hata unavyojitoa kwenu, na hapa unajua kabisa nikilega amani itatoweka na mm sitaish kwa raha basi ngoja nijitoe ili iwepo siku zangu ziwe nyingi. kwenu wakiomba hela kila siku mama sina na ukweli unakuta huna lkn ndugu wametoka huko watokako wana shida ni wa mume huwezi kuwachunia itakulazimu wale wanywe na kama wanatibiwa waende hosp ama kama ni harusi waende wakiwa wamependeza
sijamaanisha full kuuchuna.i mean maisha ni kusaidiana.nazungumzia wauza sura ambao wanapenda wanawake wao wawafanyie kila kitu
 
Aiseeee i wish i was such type of woman,maybe i am ila bado sijaexpirience,ila asante kwa ujumbe coz all you said is true familia inyingi za siku hizi mambo ndivyo yalivyo.
 
Opps, hapo blue, ndo mnafanya socialization kwa jinsi hii?

Mie kuna siku nilikuuliza, je ukiolewa na Baresa unaacha kazi uwe pika pakua?

mwalimu, wengine working hard is like a hobby. kiukweli hata ningeolewa na mfalme wa arabuni, nahisi ningekuwa bored stiff and to the core. hata nipewe kila kitu with a gold spoon to eat from, nadhani i still need some kind of work kuweka hii kichwa sawa.

msimamo wangu ni kuwa kila mtu anahitaji kufanya kazi kama sehemu ya kujamiiana.
uwe na valentine njema.
 
sijamaanisha full kuuchuna.i mean maisha ni kusaidiana.nazungumzia wauza sura ambao wanapenda wanawake wao wawafanyie kila kitu

sijui nikuelezeje yaani kuna wanaume ambao wao sijui ndivyo walivyo ama ndivyo walivyoumwa yaani kwao kujishughuisha apate hela zaid ya mshahara wake ni ngumu sana, na huyu hata kama mama atafanya nini pia haoni kama alipaswa na yeye kusaidia yaani ataappreciate tu na kukusifia na inapokuja kwenye mapenzi yaani anakutoboa ubongo kabisaaa.

manake ana macare na malove ya hali ya juu na wewe ukitoka job ukishapewa ma love davi basi mwali akini inatuliaaa huon tena hata haja ya kumsumbua zaid sana utakagua wallet yake kama haisomi basi utamwekea hata nauli ya kazini. sijui hii ni nini aisee.
 
Aiseeee i wish i was such type of woman,maybe i am ila bado sijaexpirience,ila asante kwa ujumbe coz all you said is true familia inyingi za siku hizi mambo ndivyo yalivyo.
usijali nawe pia ni mmoja wao jiangalie tu.

mimi nimejaribu kuuliza wengi sana ninakuta kama vile wote mambo ni yale yale nikajiuliza hivi wanaume hawa wametulisha nini?? yaani kama ni kuhonga ama kutuhadaaa basi hawa wameturubuni manake zaid ya care na love tumeridhika hatutak kitu kingine kwao. mpaka wamelemaa kabisaaa.

halafu sasa ile familia ambayo mama ni too demanding unakuta baba ni mtafutaji balaa ili aweze kutimiza majukumu yote kwa mama na yake
 
Back
Top Bottom