sagaciR
JF-Expert Member
- Jun 17, 2017
- 644
- 875
Sina maana ya kutotambua wanasheria wasomi wengine ila nampongeza sana Dragoo kwa mchango wake wa kuanzia uzi maarufu sana hapa jukwaa la sheria wenye maneno "Legal documents na uchambuzi wa masuala ya kisheria".
Kwa kuwa uzi tajwa hapa juu, unahusu sheria yoyote (to mention few Company, Land, Criminal, Tort, Contract, Insurance, Tax, Legal books, papers etc) basi nimeona sio mbaya kama tukiwa na platform/ roundtable ya maada maalumu kwa ajili ya Sheria za Ardhi pekee.
Mwalimu wangu wa chuo kikuu mwaka wa pili (2nd year) alitusisitiza kupenda sheria za Ardhi kwa maneno/usemi ufuatao:-
"We live on the land, we walk on the land, we build on the land, we are buried on the land therefore we must know land laws/land law is inevitably"
Kifungu cha 2 cha sheria ya Ardhi Na. 4/1999 pomoja na Na. 5/1999 kinatoa maana ya Ardhi kwa maneno haya:-
"Ardhi inajumuisha ardhi iliyo juu ya uso wa nchi na ardhi iliyo chini ya uso wa nchi, pamoja na maada zote isipokuwa madini na petroli ambavyo ni sehemu ya uso wa nchi au chini ya uso wa nchi, vitu vyenye kuota kiasili juu ya ardhi, majengo na miundo mingineyo iliyokaziwa kwa kudumu juu ya ardhi"
Kutoa elimu ya kisheria kwa umma sio biashara (na ndo maana hakuna kodi) ila Kutoa huduma ya kisheria ni biashara (na ndo maana ina kodi)
KARIBUNI KWA MASWALI NA UCHANGIAJI WA HOJA ILI TUPEANE ELIMU YA KISHERIA
Sent using Jamii Forums mobile app