Nani ana dhambi?
Askofu aliendesha harambee kuchangia ujenzi wa kanisa. Wakristo wakatoa Tshs 750,500 tu. Ghafla majambazi wakateka kanisa na kuamrisha kila mtu atoe alichonacho! Wakakusanya Tshs8,945,800 na kumkabidhi askofu ili aendeleze ujenzi. Je majambazi wana dhambi au wakristo wanathawabu? Toa maoni yako.
Majambazi wana dhambi tu kwani watu wanamajukumu hata mengine sio hela yote ni ya kujitolea kwani hautaeleweka ukibakiza watoto nyumbani kisa ada yote umetoa kanisani kwa ajili ya ujenzi, utasomeka kuwa na dhambi wewe, dawa ni kumshauri mchungaji awarudishie watu hela baada ya majambazi kuondoka.
Ahahahaaah kumbe kuna kanuni za kijambazi!Jamani wana JF mbona hamsumbui kichwa, jambazi ni fani na ina taratibu zake na kanuni zake hapa ukifuatilia hakuna sifa za jambazi zilizofuatwa, huu ulikuwa mchezo wa kuigiza tu na zoezi zima limekiuka kanuni za kijambazi hivyo ni batili