Harambee ya Kuelimisha Jamii na Kuchangia familia zenye watoto wenye Usonji zisizojiweza

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
EF824D0D-5DD2-440B-B5C3-1E6F97C773B3.jpeg


Usonji ni hali inayowapata watoto ya kuwa katika mfumo wa fahamu inayoathiri uwezo wa mtoto kuunda mawasiliano (communication), kuunda mahusiano na jamii inayomzunguka na kuathiri tabia ya mtoto na hisia nyingine mbalimbali.

Mpaka sasa duniani kote haijajulikana chanzo chake wala hauna tiba. Imethibitishwa kuwa Mazoezi Tiba (therapies) kama vile ya kuhusiana na kuongea (Speech therapy) kazi za mikono ( Occupational therapy) na tabia (Behavioural Therapy) n.k husaidia kupunguza makali au dalili za Usonji.

Gharama za haya mazoezi tiba ni kubwa sana kwa wazazi wenye watoto wenye Usonji.

Kwa mfano, Vituo vya Afya vya Serikali, gharama ni Shs 20,000 kwa wastani wa dakika 20 na vituo vya watu binafsi ni wastani wa shs 40,000 - 50,000 kwa wastani wa dakika 45, na hii ni kwa aina moja tu ya mazoezi tiba.

Hivyo Asasi ya Usonji ya Lukiza (Lukiza Autism Foundation) imeandaa harambee hii ili kuchangisha fedha kwa ajili ya mazoezi tiba kwa baadhi ya familia zisizojiweza kiuchumi. Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi

Pia, wataendelea kutoa Elimu kwa wazazi/Walezi na jamii kwa ujumla kuhusu usonji na namna ya kuwatunza watoto hawa.
 
Back
Top Bottom