Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Ukifuatilia kwa undani sakata la posho za madiwani na watendaje wengine wa halmashauri za Dar es salaam utagundua ni njia tu za kukomoana na kutafuta 'kiki'. Posho zenyewe zinasemekana ni zile ambazo haziko kisheria. Nikaja kubaini kuwa ni kwa halmashauri za Dar pekee ndizo zimeshikiwa bango. Tusubiri na Gambo wa Arusha nae aje na yake.
Kimsingi Dsm inashikiliwa na upinzani. Walianza kuwanyima mapato yatokanayo na kodi za majengo. Kwamba zitakusanywa na tra na kupelekwa serikali kuu badala ya halmashauri husika. Wakaona haitoshi wakazama kwenye hizo posho ili tu ukawa waweweseke. Kabla ya hapo utaratibu si ulikuwa huu huu?
Hii imekuja katika mazingira ambayo huwezi kuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa ni njama tu za kisiasa. Lakini pia hatujui na halmashauri zingine zina taratibu zipi za kulipana posho zisizo kisheria. Dsm si kisiwa useme kwamba yanayotokea Dsm hayawezi kutokea mikoa mingine. Dar ni mfano tu kuwa porojo za kisiasa zimeshika kasi