EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,119
Kesho kuna uwezekano mkubwa wa kuwa na sikukuu mbili kwa mpigo, yaani Eid El Fitr pamoja na Nanenane.
Zingatia; Kwangu hakuna cha tofauti na siku nyingine hivyo msione sijawakaribisha maana wengi mmeandaa matumbo ya kuwatia hasara wenzenu.
CC; snowhite, Kongosho, AshaDii, Bishanga, charminglady, Mwali, Smile, Preta, Madame B, Lizzy, afrodenzi na wengine wote.......
- Kwa wale wanaosherehekea Eid El Fitr kesho nawatakia EID MUBARAK!
- Kwa wakulima wenzangu nawaambia, "Kulima tutalima tu, tusipolima tutakufa na njaa" siku ya kesho haina maana sana kwetu zaidi ya wafanyakazi ambao hawaendi kazini.
- Kwa wale mliokufanya hela ili mkale "Bata, Kuku na kunywa Senetor, Empire na Viroba" nendeni pole pole huku mkichukua tahadhari ya kutosha.
- Kwa wale mliopanga kula sikukuu na wake au waume za watu, jueni kila mla cha mwenzie na chake huliwa.
- Kwa wale mliokuwa kwenye mfungo wa kweli, Mola awabariki sana, awape furaha ya kumaliza mfungo na pia awape nguvu ya kuanza kufunga sita baada ya sikukuu hii.
Zaidi zaidi nawatakia wote sikukuu njema!
Zingatia; Kwangu hakuna cha tofauti na siku nyingine hivyo msione sijawakaribisha maana wengi mmeandaa matumbo ya kuwatia hasara wenzenu.
CC; snowhite, Kongosho, AshaDii, Bishanga, charminglady, Mwali, Smile, Preta, Madame B, Lizzy, afrodenzi na wengine wote.......
Last edited by a moderator: