Hapo zamani za kale

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,908
30,253
THOSE WERE THE DAYS...HAPO ZAMANI ZA KALE

Kifo cha Prince Philip.

Nimelisoma jalada la siku ya uhuru katika Nyaraza za Sykes.
Najuta hii leo.

Sikulipa umuhimu mkubwa akili yangu ilitekwa na harakati za uhuru wenyewe kwa ajili hii nikaona ikiwa uhuru wenyewe ushapatikana kuna nini tena?

Nakumbuka kwenye jalada lili kulikuwa na barua inatoka kwa Peter Colmore, Nairobi anamwandikia Ally Sykes anamuomba ahakikishe kuwa yeye Colmore anapata mwaliko rasmi kuhudhuria sherehe za uhuru.

Hili Ally Sykes alilifanya na Peter Colmore alipata mwaliko rasmi wa kuhudhuria sherehe za uhuru.
Mwaka mmoja nyuma au tuseme miezi michache nyuma Peter Colmore alimuomba Ally Sykes ampeleke kwa Julius Nyerere wafahamiane.

Hili pia Ally Sykes alilifanya na Peter Colmore akakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Magomeni.

Bahati mbaya siku ile Ally Sykes na Peter Colmore walipokwenda kwa Nyerere ilikuwa ndiyo siku Patrice Lumumba ameuliwa.

Walimkuta Nyerere ana majonzi makubwa sana kwa hiyo hawakuwa na maongezi mazuri.

Pamoja na Ally Sykes na Peter Colmore katika msafara ule alikuwapo mwanamuziki mashuhuri Eduardo Masengo.

Hizo picha hapo chini ya Julius Nyerere na Bi. Titi Mohamed, Prince Philip na Mama Maria Nyerere wakicheza dansi ilikuwa Independence Ball, Diamond Jubilee Hall na wapigaji wa muziki siku ile zilikuwa bendi mbili - Royal Marine Band, bendi ya wanamaji wa Kiingereza ambao manowari yao ilikuwa imefunga gati Dar es Salaam na Shell Merry Makers ambae band leader wake alikuwa Ally Sykes.

Nimesoma Ratiba nzima ya hii Independence Ball ambayo ilionyesha hata nyimbo ambazo zilipigwa na bendi hizi mbili.

Mitindo ya dansi ilikuwa Foxtrot, Jive na Waltz.

Picha hiyo ya tatu ni vijana wa Merry Blackbirds picha hiyo ilipigwa Zanzibar miaka ya 1950.
Huyo aliyevaa suti nyeusi ni Ally Sykes na kulia kwake ni Ahmed Rashad Ally.

Vyombo vya bendi hii vilinunuliwa na Mzee Kleist mwaka wa 1947 hasa akimkusudia mwanae Ally aliyekuwa na miaka 21.

Kisa cha Mzee Kleist kumnunulia mwanae bendi ni kisa cha kusisimua.

Ahmed Rashad ana historia ya pekee katika siasa za ukombozi wa Afrika kwani aliondoka Zanzibar kwenda Cairo na huko akawa mtangazaji wa Radio Free Africa.

Radio hii ilianzishwa na Gamal Abdel Nasser kwa ajili ya propaganda kusaidia ukombozi wa Africa.

Ahmed Rashad alikuja Dar es Salaam mwaka wa 1961 kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika na alikuwapo Diamond Jubilee Hall kwenye Independence Ball.

Miaka miwili baadae 1963 Ahmed Rashad ataalikwa na Jomo Kenyatta kuhudhuria sherehe za uhuru wa Kenya na Kenyatta atamwalika Ahmed Rashad ofisini kwake kumshukuru kwa msaada wake wa kupigania uhuru wa Kenya na kufanya kampeni ili yeye na wenzake wafunguliwe kutoka jela ya Kapenguria walikofungwa na Waingereza.

Katika kukutana huku Kenyatta atamkumbuka Ahmed Rashad kuwa walipata kukutana Nairobi mwaka wa 1950 Ahmed Rashad alipomsindikiza Abdul Sykes kuonana na yeye.

Nilikuwa sichoki kumsikiliza Mzee Rashad.

Katika picha hiyo kwa kuwataja wachache yuko Abbas Sykes, Said Kastiko, Matesa na James Msikinya.

James Msikinya alikuwa kijana kutoka Afrika Kusini aliyekuja Tanganyika kutafuta maisha akikimbia ubaguzi uliokuwako kwao miaka ile.

Picha nyingine ni ya Said Kastico, Ahmed Rashad Ali na Eduardo Massengo.

Wote hawa wametangulia mbele ya haki isipokuwa Abbas Sykes na Mama Maria Nyerere.

Namshukuru Mungu kuwa baadhi ya hawa niliowataja hapa mimi niliwajua na walikuwa wazungumzaji wangu sana.

Kutoka kila picha naweza kuandika sura nzima katika historia ya hawa wazalendo.

Yako mengi sana.

Kuanzia Mama Daisy akimfunza Mama Maria namna ya kupika kwa vifuu na makumbi kupunguza gharama hadi kufikia kisa cha Nyerere kudhaniwa kalishwa sumu nyumbani kwa Abdul Sykes.

Bi. Titi kumshurutisha Nyerere kula chakula katika Mkutano wa Kura Tatu Tabora mwaka wa 1958 pale Mwalimu kwa kuelemewa na wapinzani wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir ndani ya TANU walipotishia uhai wa chama, alikosa raha akawa hata chakula kinamshinda kula.

Vita baridi baada ya uhuru kupatikana baina ya Ally Sykes, Peter Colmore kwa upande mmoja na Julius Nyerere kwa upande wa pili.

Hakika yako mengi.

Wengi katika wale ambao Prince Philip alikuwanao Diamond Jubilee Hall usiku ule kusheherekea uhuru wa Tanganyika walimtangulia mbele ya haki miaka mingi sana nyuma.

Prince Philip kafa akiungalia mwaka wa 100 mbele yake.
Hesabu yake haikukamilika imekuwa pungufu kwa mwaka mmoja.

Ni mengi hatuyajui kwa kweli.
Adrenaline,
Aliingia Sister Gerda darasani akakuta mwenzetu mmoja amechora picha ya Swastika.

Aliuliza kama tunafahamu maana yake.

Hatukuwa tunafahamu.

Akili ya kitoto ndiyo iliyomfanya mwenzetu aichore.

Sister Gerda alikuwa anataka kutoa machozi alipotuhadithia historia ya Nazi Germany.

Pale St. Joseph's shuleni kwetu masista waliokuwa pale walikuwa wanatoka Switzerland.
 
Adrenaline,
Aliingia Sister Gerda darasani akakuta mwenzetu mmoja amechora picha ya Swastika.

Aliuliza kama tunafahamu maana yake.
Hatukuwa tunafahamu.

Akili ya kitoto ndiyo iliyomfanya mwenzetu aichore.

Sister Germany alikuwa anataja kutoa machozi alipotuhadithia historia ya Nazi Germany.

Pale St. Joseph's shuleni kwetu masista waliokuwa pale walikuwa wanatoka Switzerland.
Una content nyingi sana Mkuu..
 
Duuh..
Aisee Mzee Said, Heshima yako , wewe kweli unajua unachojua
Vijana wa siku hizi ndio wanaokubeza 🖖
 
Tatizo sisi vijana tumelishwa matango pori kama wanavyosema wenyewe, Mzee wetu amesimamia haki ya kile anachokijua kwa uweledi wa hali ya juu, ndiyo maana kila anayetaka kum-challange anashindwa miserably.
 
Maisha ya mwanadamu ni maua - tenda wema ili roho yako ikapate pumziko la amani !!

Mama Maria naona alikuwa kwenye age ya 30's bado kabisa !! aisee.
 
Tunapita pale Barabara ya Bibi Titi Mohamed, ila kumbe alikuwa mrembo hivi though kakwepesha sura kwenye Camera ha ha ha
 
Tatizo sisi vijana tumelishwa matango pori kama wanavyosema wenyewe, Mzee wetu amesimamia haki ya kile anachokijua kwa uweledi wa hali ya juu, ndiyo maana kila anayetaka kum-challange anashindwa miserably.
Vumi...
Ahsante sana.
 
..Sheikh Mohamed Said asante sana kwa kumbukumbu nzuri....ndio maana wanasema Mzee (kama Mohamed Said) akitutoka, ni sawa na maktaba imeungua...Mungu akupe umri mrefu uwezo kutujuza zaidi! Khair ya Ramadhan!
 
Kilembwe,
Ahsante.
 
THOSE WERE THE DAYS...HAPO ZAMANI ZA KALE

Kifo cha Prince Philip.

Nimelisoma jalada la siku ya uhuru katika Nyaraza za Sykes.
Najuta hii leo.

Sikulipa umuhimu mkubwa akili yangu ilitekwa na harakati za uhuru wenyewe kwa ajili hii nikaona ikiwa uhuru wenyewe ushapatikana kuna nini tena?

Nakumbuka kwenye jalada lili kulikuwa na barua inatoka kwa Peter Colmore, Nairobi anamwandikia Ally Sykes anamuomba ahakikishe kuwa yeye Colmore anapata mwaliko rasmi kuhudhuria sherehe za uhuru.

Hili Ally Sykes alilifanya na Peter Colmore alipata mwaliko rasmi wa kuhudhuria sherehe za uhuru.
Mwaka mmoja nyuma au tuseme miezi michache nyuma Peter Colmore alimuomba Ally Sykes ampeleke kwa Julius Nyerere wafahamiane.

Hili pia Ally Sykes alilifanya na Peter Colmore akakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Magomeni.

Bahati mbaya siku ile Ally Sykes na Peter Colmore walipokwenda kwa Nyerere ilikuwa ndiyo siku Patrice Lumumba ameuliwa.

Walimkuta Nyerere ana majonzi makubwa sana kwa hiyo hawakuwa na maongezi mazuri.

Pamoja na Ally Sykes na Peter Colmore katika msafara ule alikuwapo mwanamuziki mashuhuri Eduardo Masengo.

Hizo picha hapo chini ya Julius Nyerere na Bi. Titi Mohamed, Prince Philip na Mama Maria Nyerere wakicheza dansi ilikuwa Independence Ball, Diamond Jubilee Hall na wapigaji wa muziki siku ile zilikuwa bendi mbili - Royal Marine Band, bendi ya wanamaji wa Kiingereza ambao manowari yao ilikuwa imefunga gati Dar es Salaam na Shell Merry Makers ambae band leader wake alikuwa Ally Sykes.

Nimesoma Ratiba nzima ya hii Independence Ball ambayo ilionyesha hata nyimbo ambazo zilipigwa na bendi hizi mbili.

Mitindo ya dansi ilikuwa Foxtrot, Jive na Waltz.

Picha hiyo ya tatu ni vijana wa Merry Blackbirds picha hiyo ilipigwa Zanzibar miaka ya 1950.
Huyo aliyevaa suti nyeusi ni Ally Sykes na kulia kwake ni Ahmed Rashad Ally.

Vyombo vya bendi hii vilinunuliwa na Mzee Kleist mwaka wa 1947 hasa akimkusudia mwanae Ally aliyekuwa na miaka 21.

Kisa cha Mzee Kleist kumnunulia mwanae bendi ni kisa cha kusisimua.

Ahmed Rashad ana historia ya pekee katika siasa za ukombozi wa Afrika kwani aliondoka Zanzibar kwenda Cairo na huko akawa mtangazaji wa Radio Free Africa.

Radio hii ilianzishwa na Gamal Abdel Nasser kwa ajili ya propaganda kusaidia ukombozi wa Africa.

Ahmed Rashad alikuja Dar es Salaam mwaka wa 1961 kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika na alikuwapo Diamond Jubilee Hall kwenye Independence Ball.

Miaka miwili baadae 1963 Ahmed Rashad ataalikwa na Jomo Kenyatta kuhudhuria sherehe za uhuru wa Kenya na Kenyatta atamwalika Ahmed Rashad ofisini kwake kumshukuru kwa msaada wake wa kupigania uhuru wa Kenya na kufanya kampeni ili yeye na wenzake wafunguliwe kutoka jela ya Kapenguria walikofungwa na Waingereza.

Katika kukutana huku Kenyatta atamkumbuka Ahmed Rashad kuwa walipata kukutana Nairobi mwaka wa 1950 Ahmed Rashad alipomsindikiza Abdul Sykes kuonana na yeye.

Nilikuwa sichoki kumsikiliza Mzee Rashad.

Katika picha hiyo kwa kuwataja wachache yuko Abbas Sykes, Said Kastiko, Matesa na James Msikinya.

James Msikinya alikuwa kijana kutoka Afrika Kusini aliyekuja Tanganyika kutafuta maisha akikimbia ubaguzi uliokuwako kwao miaka ile.

Picha nyingine ni ya Said Kastico, Ahmed Rashad Ali na Eduardo Massengo.

Wote hawa wametangulia mbele ya haki isipokuwa Abbas Sykes na Mama Maria Nyerere.

Namshukuru Mungu kuwa baadhi ya hawa niliowataja hapa mimi niliwajua na walikuwa wazungumzaji wangu sana.

Kutoka kila picha naweza kuandika sura nzima katika historia ya hawa wazalendo.

Yako mengi sana.

Kuanzia Mama Daisy akimfunza Mama Maria namna ya kupika kwa vifuu na makumbi kupunguza gharama hadi kufikia kisa cha Nyerere kudhaniwa kalishwa sumu nyumbani kwa Abdul Sykes.

Bi. Titi kumshurutisha Nyerere kula chakula katika Mkutano wa Kura Tatu Tabora mwaka wa 1958 pale Mwalimu kwa kuelemewa na wapinzani wakiongozwa na Sheikh Suleiman Takadir ndani ya TANU walipotishia uhai wa chama, alikosa raha akawa hata chakula kinamshinda kula.

Vita baridi baada ya uhuru kupatikana baina ya Ally Sykes, Peter Colmore kwa upande mmoja na Julius Nyerere kwa upande wa pili.

Hakika yako mengi.

Wengi katika wale ambao Prince Philip alikuwanao Diamond Jubilee Hall usiku ule kusheherekea uhuru wa Tanganyika walimtangulia mbele ya haki miaka mingi sana nyuma.

Prince Philip kafa akiungalia mwaka wa 100 mbele yake.
Hesabu yake haikukamilika imekuwa pungufu kwa mwaka mmoja.

Chapisha kitabu
 
Back
Top Bottom