Hapendwi mtu, ila pochi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
Kwa maoni yangu walilofanya wachezaji wa Yanga ni kosa kubwa, sasa tusikie wanachama na wapenzi wa Yanga watakuwa upande gani katika sakata hili. Kuna uwezekano wa kuzuka Kandambili na Raizoni nyingine

Posted Date::10/13/2007
Madega aporwa timu
*Wachezaji wahamishiwa Courtyard, Kempiski

*Kisasa asimamishwa na mahakama

*Mwenyekiti kuitisha kamati kuu

Na Oliver Albert
Mwananchi

MGOGORO kwenye klabu ya Yanga jana ulizidi kuwa mgumu baada ya timu kuondolewa kutoka kambini Morogoro na kuhamishiwa Dar es salaam, muda mfupi tu baada ya mwenyekiti Imani Madega kuongea na wachezaji na kuhakikishiwa kuungwa mkono, huku katibu mkuu, Lucas Kisasa akisimamishwa na mahakama.

Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega na mfadhili mkuu, Yusuf Manji waliibua tofauti zao mapema wiki hii baada ya Manji kutangaza kujiondoa Yanga kwa madai kuwa uongozi umeshindwa kutekeleza zoezi la kuihamishia timu kwenye kampuni, huku Madega akisema zoezi hilo lina upungufu mkubwa wa kisheria na kikatiba na linahitaji muda.

Jana asubuhi, wachezaji waliandika barua ya kutaka kuonana na mfadhili mkuu wa Yanga, Yusuf Manji na kumuandikia mwenyekiti Madega kuwa iwapo hatamrejesha Manji mapema watagomea mechi ya Jumapili dhidi ya Mtibwa Sugar.

Taarifa iliyotumwa kwa waandishi wa habari kutoka Mkoani Morogoro ilisema wachezaji hao wameutaka uongozi huo kumrejesha haraka mpendwa wao Manji, ambaye aliwalipa fedha za usajili.

''Wamrejeshe haraka ikiwezekana leo usiku (jana) kwani ni mtu muhimu sana kwetu kwa kila kitu, tunataka arudishwe haraka kabla mechi ya jumapili,'' inasema sehemu ya barua yao.

Barua hiyo inasema maamuzi hayo ni ya wachezaji wote, ambao wamesaini isipokuwa Laurent Kabanda, Said Maulid na Thomas Maurice.

Baada ya kutaarifiwa suala hilo, Madega alienda Morogoro asubuhi na kuongea na wachezaji, ambao walimhakikishia kuwa wako pamoja naye, lakini muda mfupi baada ya kuondoka Morogoro, kocha Jack Chamangwana aliagizwa aisafirishe timu kuja Dar es salaam, ambako baadaye ilisemekana kuwa wachezaji wamewekwa kwenye hoteli ya Courtyard na Kempiski.

Nimesikia timu imechukuliwa,� alisema Madega. �Mimi niliongea na wachezaji na wakanihakikishia kuwa hawana matatizo. Inaelekea kiongozi wa timu Emmanuel Mpangala amezidiwa nguvu.

Lakini nitaitisha kikao cha kamati kuu ili tujadili na kufikia uamuzi. Huu sasa ni uhuni maana ni kama klabu haina timu.�

Habari zaidi zinasema kuwa mipango ilikuwa ikifanyika ili wachezaji waongee na Manji na mmoja wa wachezaji alipopigiwa simu jioni, alisema kuwa walikuwa wakielekea kukutana na mfadhili huyo.

Kuna uwezekano mkubwa, Madega na viongozi wenzake wakaomba mechi ya kesho dhidi ya Mtibwa na nyingine zinazofuatwa zisimamishwe hadi hapo hali itakapotengemaa.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu Lucas Kisasa amesimamishwa na mahakama kujishughulisha na masuala ya klabu baada ya wanachama watatu � Juma Magoma, Rashid Bhinda, Godfrey Mwaipopo kufungua kesi Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Katika kesi hiyo, wanachama hao waliiomba mahakama imsimamishe katibu mkuu na mwanachama anayeitwa David Mwakalindile, ambaye aliajiriwa kama mhasibu wa klabu, kwa kesi ambayo inatarajiwa kufunguliwa dhidi ya wawili hao.

Katika hatua nyingine, kundi la wanachama wakiongozwa na Yusuph Mzimba wamemtaka mwenyekiti Madega kutangaza kuwa mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 16 kuwa ni halali kwa kuwa aliwaahidi wanachama kuwa angeitisha mkutano katika muda wa siku 45, ambazo zinaisha Jumanne.

'' Sasa siku 45 zinatimia Oktoba 16 na tena amegeuka na mwenyekiti alisema amefuta mkutano, kama kweli ni uvunjaji wa katiba na kutokana na hilo tunamuomba katibu mkuu aitishe mkutano huo kwa sababu ana mamlaka ya kuitisha mikutano yote ya klabu,'' alisema Mzimba.

Hata hivyo, Madega alisema mkutano hautakuwepo kwa sababu hali si shwari klabuni na hivyo kuitisha mkutano sasa itakuwa ni kuhatarisha amani.

Kwanza mkutano ule ulikuwa uzungumzie katiba, lakini hakuna linalojadiliwa kuhusu katiba sasa, hivyo siwezi kuitisha mkutano hadi hapo hali itakapokuwa shwari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom