Habari zenu wana-Jamvi,.
Nina mpenzi wangu ambaye anaishi Dar, tumekaa kwenye mahusiano takriban miezi nane sasa bila kukorofisana kwa namna yoyote ile,.
Kwa sasa mimi nipo mkoani nikifuatilia mambo yangu binafsi huku tukiwa na mawasiliano ya mara kwa mara kupitia simu,.
Huyu mpenzi wangu amekuwa akiniuliza mara kwa mara ni lini nitarejea jijini kumpa raha maana amenimiss sana hivyo anayo hamu sana ya ku-Do,.
Nimemwambia bado kidogo nitarejea jijini hivyo asijali awe na subira tu,.
Sasa nimepata safari muhimu ya kuelekea Songea ila nitapitia ofisini Dar kabla ya kuelekea songea na nitakaa Jijini dar kwa siku tatu kabla ya safari ambayo nitachukua miezi saba bila likizo!!
Kwa sasa sihitaji kufanya mapenzi maana ninatumia dawa ambazo nimeshauriwa na daktari wangu nisishiriki tendo mpaka hapo atakaponipa ruhusa,.
Wadau nipo njia panda maana sijui mpenzi wangu atanichukuliaje kumuacha bila kumgegeda ukizingatia ni mda mrefu sijakutana naye kimwili,.
Na kama nitaenda Songea bila kumfahamisha sijui atakuwa katika hali gani mpaka nitakapopata likizo tena,.
Dada zangu na Kaka zangu naombeni mnisaidie ili huyu mpenzi wangu anielewe basi, hamtakosa la kunishauri tafadhalini,.
Natanguliza shukrani,..