Hapa ndipo tumefika?

sing8

Member
Dec 7, 2017
12
6
Nimepita mtaa mmoja hapa jijini Dar es salaam, nimekutana na kibao kimeandikikwa MAGU halafu mbele yake baada ya maneno hayo pamefutwa, nilipochunguza zaidi nikaona maneno yaliyokuwepo yalikuwa yameandikwa FULI. Nilipouliza wenyeji wakaniambia mtaa ulikuwa unaitwa kwa jina la huyo bwana mkubwa baadaye wakaamua kufuta maneno ya mbele. Nikajiuliza, nini maana ya hii. Hebu tujuzane, tafsiri ya hiki kitendo.
IMG_20180315_105127.jpg
 
Ni aibu kujinasibisha kwa namna yoyote ile na hilo jina la huyo mtoa roho za watu anayenuka damu za raia wasio na hatia

Hongereni sana wana mtaa huo kwa kumpinga huyu chizi kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kumfukuza na makopo yake yote ili asirejee tena
 
Magu ni jina la kitambo sana hapo Mwanza.
Jina hili lilikuwepo tangu enzi za Nyerere, na sasa palipata hadhi na kupewa wilaya.
Hapo Magu nimepita sana enzi za ujana wangu..... baada ya Igoma una enda Kisesa then Magu nakuendelea
 
Huyo analinda shamba ama eneo lake.Nadhani amri itatoka karibuni usilitaje ama litumia jina la mfalme
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom