Hapa ndipo tulipoishia kufikiri kwenye siasa, ngono, pombe na starehe

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,495
24,222
1. Siasa ndio maisha ya mtanzania kwa sasa.

2. Ngono/pombe na starehe kwa ujumla ndio maisha ya mtanzania kwa sasa.

Hivyo vitu viwili hapo juu kwa sasa vinalipeleka taifa utumwani tena, wasomi wetu hawana msaada tena zimebaki porojo, wananchi wengine mtaani kule ni mwendo wa kubet, vigodoro, chura, diamond na kiba, bongo movie na stori zake.

Kiuhakika bongo za watanzania kwa sasa hazifanyi kazi ni kama zimesimama.

Bungeni ndio hivyo tena pumba zinaendelea yaani no formula, mbunge anaongea utafikili anasoma STD 2B, hakuna dira kifupi inayoweza kutabiri future yetu.

Wasomi wamegeuka watumwa wa wanasiasa wameshindwa kabisa kulisaidia taifa na kujisaidia wenyewe hata pale pasipohitaji fundi ila ni akili yao tu kwa kile walichosomea..

Watanzania wenzangu tunafanyeje tutoke hapa??
 
Kama umegundua hayo wewe unafikiri nini kifanyike?

Ni wakati wa mimi na wewe kufikiri na kusaidia mawazo, taifa limesimama, MH JPM kwa nguvu yake anajitahidi kupambana ila kuna shida mahali kama inamkwamisha, mimi na wewe sote ni watanzania tunajikwamuaje???
 
mkuu hebu tupe mapendekezo watu waache kufanya hayo na wafanye nini hasa?

Watanzania wenzangu tunashauri nini tutoke hapo? Kwa uzoefu wako utaona kuna mahali kama Taifa linakwama pamoja na nguvu ya mh JPM, huo mkwamo unasababishwa na hivyo vitu viwili ambavyo viko kwenye akili ya watanzania, siasa,ngono na upumbavu mwingi tufanyeje mh JPM angalau anaweza kuuona ushauri wako akaufanyia kazi, maana taifa limekwama nguvu kazi inayotegewa akili ndio ziko huko tunahamaje hapa kiakili...
 
Ni wakati wa mimi na wewe kufikiri na kusaidia mawazo, taifa limesimama, MH JPM kwa nguvu yake anajitahidi kupambana ila kuna shida mahali kama inamkwamisha, mimi na wewe sote ni watanzania tunajikwamuaje???

Uzalendo umetoweka hakuna kiongozi yeyote anayefikiri kwa kina kuangali maisha watanzania wa kizazi hiki katika maendeleo yao kielimu,kiuchumi na kijamii na kufanya mchanganuo yakinifu kuwawezeza kuendana na changamoto ya mabadiliko ya dunia ya sasa.

Siasa zimetawala taaluma na uweledi wawalio wengi kwa minajili ya kunusuru chama fulani cha siasa kiendelee kutawala na sio maslahi ya Taifa.

Tumebaki kuwa kama boya baharini likifuata muelekeo wa mawimbi hakuna dira ya kweli ya kulikomboa taifa na wananchi wake zaidi ya kiakikisha kiongozi fulani ateke akili za sisi watanzania walala hoi ili ashinde uchaguzi 2020.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ili Taifa masikini liendelee lazima litumie nguvu kazi yake yaani wananchi wake kwa kiwango cha juu pamoja na rasilimali zake yenyewe kwa kiwango cha juu.

Je tujiulize Tanzania tupo wapi sasa kwenye karne hii.

Je nguvu kazi ya Taifa hili inatumika ipasavyo kwa maendeleo?

Je rasilimali tulizonazo zinatumika vizuri kwa kiwango cha juu kunufaisha Taifa hili??

Je Mwalimu alikosea kutuachia huu urithi aliosema ukae mpaka watanzania watakapo jielewa waweze kuutumia kwa maendeleo ya vizazi vya sasa na vijavyo?

Ukweli sera nyingi za kuvutia wawekezaji hazikuzingatia mazingira halisi ya mtanzania wa sasa na uwezo wake hivyo viongozi wetu wamekuwa wakitumia mbinu za mkato kwa kutaka matoke ya haraka na kuacha nchi ikitafunwa kama shamba la bibi.

Uwekezaji bila kuangalia nguvu kazi na uwezo wa kitaaluma wa watanzani tutaishia tunapiga mayowe bila msaada.
 
unayosema ni kweli mfano jaribu kupost hoja yoyote ya ngono utaona inavyopata wachangiaji wanasema ukitaka kujua tabia za nchi husika soma vichwa vya habari vya magazeti yao magazeti karibuni yote yamejaa hizo habari ambazo kiukweli hazina manufaa yoyote kwa nchi.
Nashangaa hata vile vyama kama vya wenye viwanda,au wafanyabiashara badala ya kuangalia fursa kuwekeza nao wanafanya siasa eti wanatafuta wawekezaji inabidi tujitahidi tubadilishe uwezo wetu wa kufikiri
 
Well said mkuu, wasomi wetu wanashindwa hata kutumia usomi wao kwa utaalamu husika kujisaidia na kusaidia taifa, hata kwa zile project zisizojitaji fund...
 
1. Siasa ndio maisha ya mtanzania kwa sasa.

2. Ngono/pombe na starehe kwa ujumla ndio maisha ya mtanzania kwa sasa.

Hivyo vitu viwili hapo juu kwa sasa vinalipeleka taifa utumwani tena, wasomi wetu hawana msaada tena zimebaki porojo, wananchi wengine mtaani kule ni mwendo wa kubet, vigodoro, chura, diamond na kiba, bongo movie na stori zake.

Kiuhakika bongo za watanzania kwa sasa hazifanyi kazi ni kama zimesimama.

Bungeni ndio hivyo tena pumba zinaendelea yaani no formula, mbunge anaongea utafikili anasoma STD 2B, hakuna dira kifupi inayoweza kutabiri future yetu.

Wasomi wamegeuka watumwa wa wanasiasa wameshindwa kabisa kulisaidia taifa na kujisaidia wenyewe hata pale pasipohitaji fundi ila ni akili yao tu kwa kile walichosomea..

Watanzania wenzangu tunafanyeje tutoke hapa??
Ili ufanye yote hayo kwa usahihi lazima uwe smart.na pesa.....na sio tz tuuu n dunia nzima

Unatafuta pesa kwa.nguvu,ili zitumike
 
Back
Top Bottom