hapa ndipo napoona ufinyu wa elimu ndugu zetu Hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hapa ndipo napoona ufinyu wa elimu ndugu zetu Hawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by muhogomchungu, Mar 12, 2011.

 1. muhogomchungu

  muhogomchungu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAHARIRI YA TZDAIMAKSerikali isaidie zaidi Loliondo JANA Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alitoa msimamo wa serikali kwamba haina nia ya kumzuia Mchungaji mstaafu wa Kanisa la KKKT, Ambilikile Mwasapile, kutoa tiba wilayani Lolindo na badala yake imemuongezea nguvu kwa kutuma timu ya wataalamu na gari moja la kubeba wagonjwa.Uamuzi huo wa serikali wa kutomzuia mtumishi huyo wa Mungu kutoa uhuduma yake kwa wananchi wa taifa hili ambao wanakabiliwa na maradhi mbalimbali ni wa busara.Hata hivyo tunasema mchango huo wa serikali bado ni mdogo ukilinganisha na maelfu ya wananchi wanaoendelea kufurika Loliondo kwa mchungaji Mwasapile kupata tiba na hivyo kusababisha magari kukwama huko kutokana na barabara kulemewa na foleni, uhaba wa vyoo, madaktari na manesi wa kutoa huduma za kiafya haraka kwa watu watakaopata magonjwa ya milipuko.Baadhi yetu tumeona kupitia televisheni mbalimbali juu ya maisha halisi ya wananchi waliofika kwa mchungaji huyo kupata tiba, tumeona wakitumia vikombe ambavyo ni vichache kunywea dawa, babu huyo akitumia nishati ya kuni kuchemshia dawa hiyo hali inayosababisha dawa hiyo kuchukua muda mrefu hivyo kufanya wagonjwa na watu mbalimbali kukaa kwa muda mrefu wakisubiri kupata dawa hiyo.Tulitegemea serikali yetu mbali na kuimarisha ulinzi pia ingehakikisha inamsaidia mzee huyo vifaa vya kutolea tiba yake kama vikombe, majiko mbalimbali ya kuivishia hizo dawa na maji safi na salama kwa ajili ya kupikia na kuoshea vyombo hivyo na hata kumuongezea wahudumu.Sisi Tanzania Daima tunaiomba serikali ione haja hata ya kulitumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupeleka wahandishi wake kijijini hapo na kwenda kutengeneza barabara za muda, kuchimba visima, vyoo ili magari yaweze kuingia na kutoka kwa wakati katika eneo hilo kwani hivi sasa tunaambiwa zaidi ya magari 100 yamekwama kwenye foleni kwa kuwa njia ni nyembamba na hayawezi kupishana.Hali kadhalika, JWTZ watumiwe kujenga mahema ili wananchi wakiwemo kina mama na watoto walio kwenye foleni kusubiri kupatiwa tiba ya mchungaji huyo waweze kujisitiri.Kama serikali itashindwa hilo basi taasisi binafsi nazo zinaweza kuliona hilo kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali ili kufanikisha huduma inayotolewa na mchungaji huyo ili watanzania wenzetu ambao wana imani kuwa wakinywa dawa ya mtumishi huyo wa Mungu watapona maradhi hayo waweze kupata huduma hiyo kwa haraka na kisha waweze kurejea maofisini kwa ajili ya shughuli nyingine za ujenzi wa taifa kwani tayari baadhi wameziacha ofisi zao na kukimbilia Loliondo kupata tiba hiyo.Pia tunaishauri serikali, kwa kuwa dawa hii ni ya kiimani zaidi pamoja na kuishughulikia kujua kama inatibu au la, pia iwaite wale wote ambao awali walipima mahospitalini na sasa wamekunywa dawa hiyo ya mchunguaji, wawatumie kubaini kile kinachozungumzwa mitaani kama dawa hiyo inaponya watu waliogundulika kuwa na magonjwa sugu kama kisukari, kansa, ukimwi, TB, pumu na mengineyo.Kwa kuwa tunaamini wagonjwa ni wengi katika taifa hili ila wana kasumba ya kujificha, kwa sasa wameamua kuwa wawazi kwa kwenda kupiga kambi Loliondo kunywa dawa, hivyo serikali yetu haina sababu ya kupuuza haraka tiba inayotolewa na mchungaji huyo.Ikiwa kama tunaamini Mwenyezi Mungu alilipenda taifa hili na ndiyo maana likawa ni taifa pekee lenye madini aina ya Tanzanite, na utajiri mwingine basi si ajabu ikatokea mtanzania mmoja akaweza kufanya maajabu hayo. Hivyo hili si jambo la kulipinga bila utafiti wa kina kufanyika na kubaini ukweli ni upi.Ni kweli kila kukicha baadhi ya waganga wa kienyeji na waumini wa dini mbalimbali wamekuwa wakijitangaza kuwa wana uwezo wa kutibu magonjwa ambayo yameshindikana kutibiwa kama ukimwi kupitia neno la Mungu na dawa za mitishamba, lakini mwisho wa siku hubainika kuwa si kweli.Tunaamini serikali yetu ina mkono mrefu na iko kwa ajili ya kuwalinda wananchi wake, hivyo tunaiomba Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi na vyombo vingine nyeti vya umma kuhakikisha inamuwekea ulinzi wa kutosha Mchungaji Mwasapile katika kipindi hiki ambacho pia dawa yake inafanyiwa uchunguzi; lakini pia kwa usalama wake na usalama wa kitongoji anachoishi.
   
 2. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi nina mtizamo tofauti; kwa maoni yangu, serikali haina budi kuachana na mtindo huu wa kuingilia shughuli binafsi bila yakuombwa na wahusika, isipokuwa kama sababu ya kuamini ya kwamba shughuli husika inakinzana na sheria za nchi.
   
Loading...