Vizuri kabisa!Kuna njia nyingi sana za kuujua ukweli, moja wapo ni kuuliza yanayo endana na uhalisia.
Leo hii naweza nisijue kwanini tunaambiwa Virusi vinatengenezwa, ila naweza kujua ukweli kwa kuuliza kwa yule anae sema Virusi vinatengenezwa. Huu ni mfano tu.
Kwahiyo kuona au utufikishie ujumbe unatakiwa pia utuambie na utujibie maswali yanayo gusa msingi au misingi ya kile unacho tuelezea.
Pili, mimi sina majibu ila mimi nina uhalisia wa mambo jinsi yalivyo na tunavyo yadiriki mambo ya nadharia na kuhakiki vitu kwenye makaratasi ndio ambayo hatuyataki na yameshapitwa na wakati sababu hayaakisi uhalisia wa mambo zaidi ya dhana na kubahatisha. Hakuna nadharia ambayo inaweza kuthibitisha ukweli wa nadharia nyingine mzee. Leo huwezi kutuambia "Dark Energy " ndio imeshikilia uhai wetu, bila kutuambia imetoka wapi na inafanya vipi kazi na ipo wapi na ni nani wakwanza kusema hivyo na ilikuwaje mpaka akahitimisha hilo ?Akili salama inakataa hizi porojo.
Tatu, suala la mtu kutokueleweka lina sababu nyingi sana, miongoni mwa sababu hizo nji watu kuukataa ukweli kwa makusudi, na wengine kupeleka mapenzi mbele pasi na kuhoji, hata huyo anae elezea mambo hayo laiti angeamua kuhoji asingeendelea kuandika haya.
Nne, kadhalika lengo langu sio wewe unielewe au wengine wanielewe au wale wanielewe, bali lengo langu ni kuufikisha ukweli basi na ukweli unafika kwa njia hii pia.
Ahsante.
Hapa umekiri kwamba unauhalisia wa mambo yalivyo.
Sasa nikuombe kitu kimoja hapa kuhusiana na mada husika. Hebu tupe uhalisia wa Mambo yalivyo katika yafuatayo na ututhibitishie kwamba ndio uhalisia wenyewe kwa kutupa ushahidi usio na shaka:-
1. Tupe uhalisia na ushahidi kwamba katika elimu ya namba na maumbo hakuna siri yoyote iliyofichwa ama iliyokusudiwa kufichwa na waanzilishi wa elimu hizi au namba na maumbo yapo yapo tu havina siri wala kitu chochote zaidi ya kutumika kufundishia mashuleni.
2. Toa uhalisia na ushahidi wako kwamba hakuna kitu wanasayansi wamegundua na kukiita "Dark energy"
3. Tupe uhalisia na ushahidi kwamba hakuna virus wanaotengenezwa na kundi la watu maalum kwa malengo yao ya kimkakati katika dunia hii
Nadhani hizo ndo hoja kuu zilizomo humu na ambazo unaona kama zimeongelewa isivyo na uhalisia! Hebu tupe uhalisia ulivyo
Sent using Jamii Forums mobile app