SAYANSIKIMU
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 1,132
- 260
Kulikuwa na mshikaji mmoja ambaye alikuwa tajiri sana na pia alikuwa mfalme basi akaandaa shindano.Akawaambia Washindanaji mmeona hili bwawa lina mamba mengi basi yoyote atakaye tumbukia humu na kuogolea na kutoka upande wa pili akiwa hai nampa chochote anachotaka hata ufalme wangu wote na hili agano nimesha saini tayari kabla hajamaliza kusema kuna njemba moja ilikuwa imeshazama kwa ujasiri wa ajabu akafanikiwa kuogolea na kuvuka upande wa pili wa kisima akiwa hai mfalme alishangaa sana ujasiri wa huyu kijana.Mfalme akamwambia kijana unataka nini sasa nikupatie .Jamaa akajibu mimi sitaki fedha ,wala ufalme wala mali yoyote bali nataka yule aliyenisukumiza kwenye hichi kisima namimi nimrudishie kwa kumtumbukiza humu. NB. KUMBE HII NJEMBA HAIKUTUMBUKIA YENYEWE BALI ILISUKUMIZWA TU.