Mimi sitii neno kwenye hayo ya Mwalimu, lakini ninayo hoja kwenye RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA, 2014. Nianze na Ibara ya 1 (1).
Ibara hiyo inasema kama ifuatavyo: "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi na ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa Nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 zilikuwa nchi huru."
Hiyo si ndiyo Kazi ya Tume ya Bunge Maalumu ya Katiba -Hivi kweli wajilie 300,000 per day hivi hivi tu.
Je likisomeka kama hivi situtakuwa sambamba!
Ibara ya 1 (1). "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa Nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika iliyopata uhuru wake 9/12/1961 na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar iliyopata uhuru wake chini ya Mapinduzi takatifu ya 12 Januari 1964 .