Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,192
- 1,978
"Pwani ya Tanganyika na Zanzibar ya sasa zilikuwa pamoja kwa muda mrefu sana kabla ya kutengwa na Wakoloni Waingereza na Wajerumani. Kama zingebaki zimetengana, kwa "wazalendo" hao hiyo ingekuwa ni halali, maana zilitengwa kwa hila na mitutu ya bunduki za Mabwana. Lakini uamuzi wa Tanganyika huru na Zanzibar huru kuungana, na hivyo kuwaunganisha tena ndugu waliokuwa wametengwa na Mabeberu, tendo hilo kuna viongozi wetu wanaosema kuwa halikuwa halali.
Hatukutafuta maoni ya watu kwa njia ya demokrasia wanayoijua wao. Wajerumani na Waingereza walitafuta maoni ya wazee wetu kwa tutu wa bunduki! Hiyo ilikuwa ni halali. Nchi walizoziunda kwa njia hizo zilikuwa halali. Tunatakiwa tujivunie Utanganyika na Uzanzibari uliopatikana kwa njia hizo; lakini tuuonee haya Utanzania, tunda la uhuru wetu wenyewe.
Sikuamini kuwa Wakoloni walifaulu kiasi hiki kuzinywesha kasumba na kuzitawala akili za baadhi yetu!"
(Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Julius K. Nyerere, uk. 59).
Hayo yalikuwa ni maneno ya Mwalimu Nyerere juu ya hoja ya "Utanganyika" na "Uzanzibari" ilipofikia katika hali ya kutisha.
Mimi sitii neno kwenye hayo ya Mwalimu, lakini ninayo hoja kwenye RASIMU YA PILI YA KATIBA MPYA, 2014. Nianze na Ibara ya 1 (1).
Ibara hiyo inasema kama ifuatavyo: "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi na ni Shirikisho lenye mamlaka kamili ambalo limetokana na Muungano wa Nchi mbili za Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla ya Hati ya Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 zilikuwa nchi huru."
Ukisoma Ibara hiyo ni kama vile Nchi za Tanganyika na Zanzibar hazitakuwa huru baada ya Muungano wa Serikali 3! Lakini ukipitia Ibara nyinginezo utakuta kuwa katika Rasimu hii kuna NCHI 3 na vile vile SERIKALI 3!
Ukisoma Ibara ya 44 na 60 (3) zinatamka Serikali za "Nchi washirika!" Ibara ya 64 ndio inayotafsiri hizo "Nchi Washirika" ni kitu gani! Nanukuu kutoka kwenye Ibara hiyo:
"64 (1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(2)........
(3)........
(4) Nchi washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Katiba hii na Katiba zao.
(5) Nchi washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba za Nchi Washirika."
Ibara nyingine inayozungumzia "Nchi Washirika" ni Ibara ya 65 inayosema kwamba kila "Nchi Mshirika" itakuwa na haki na mamlaka ya mambo yote yasiyo ya Muungano!
Kwa upande mwingine, Ibara zinazozungumzia "Serikali 3" ni hizi zifuatazo: Ibara ya 64 (2) inasema kama ifuatavyo: "Serikali ya Tanganyika itakuwa na mamlaka ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanganyika." Ibara ya 64 (3) inasema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka ya mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar. Ibara ya 65 (3) inazungumzia juu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba ushirikiano kutoka kwenye "Nchi Washirika!"
Hoja yangu ni kwamba, japokuwa Warioba amezungumzia sana juu ya "Serikali 3" lakini kilichojificha nyuma ya pazia ni "Nchi 2" ndani ya nchi nyingine ya 3! Ndio maana katika Hotuba yake Warioba amedai kwamba itakuwa ni vigumu sana kwa Wazanzibari ni VIGUMU sana kubadili katiba yao iondoe kipengele cha "Zanzibar ni Nchi!"
Kusema kweli Rasimu hii iliyopo ni ya kuvunja Muungano na si vinginevyo, kwani huwezi kuwa na nchi mbili zikawa ndani ya nchi nyingine na ukadai huu ndio Muungano! Na kama lazima kuwa na nchi 2 ndani ya nchi 1, lazima hiyo nchi moja inayobeba nchi 2 iwe na NGUVU ya kiuchumi ya kuzibeba. Kwa mujibu wa Rasimu, Serikali ya Muungano ina mapato kidogo sana ukilinganisha na "Nchi Washirika!"
Ni Rasimu ya ajabu sana kuhusu Muungano, kwa maoni yangu!
Hata hivyo, tujadili zaidi, ikiwezekana iwe hapa hapa kwenye Jukwaa la Katiba Mpya!