Aventus
JF-Expert Member
- Mar 8, 2013
- 2,011
- 2,167
Huku kwetu.., sisi tunaendelea kusherekea kwa kutumbuliwa kwa Mramba, kesho sijui zamu ya nani.., lakini hatupigi kelele kamwe ya kutaka ahadi tarajali kutekelezwa zenye kutugusa sisi huko kwetu.., tangu 2015, November 05 ni kutumbua, kutengua, kuteua, kutumbua, kutengua, kuteua.., na sisi huko kijijini kwetu tunapiga kelele za kushangilia na vigelegele vikichombezwa na neno maridhawa, Hapa Kazi Tu!