Hapa kazi tu series in Tanzania

waltham

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,522
1,045
15941332_1334468066615378_6789046678191642301_n.jpg

HALI YA ELIMU!!!! nilidhani kila siku naskia sauti kutoka huko nyanda za kusini kusema kiswahili na tz ni mapacha!!!!!:eek:

RIPOTI KAMILI YA TWAWEZA KUHUSU ELIMU YA SHULE YA MSINGI

Imeelezwa kuwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili ambapo wanafunzi Wanne kati ya kumi sawa na asilimia 44 waliopo shule za Msingi za serikali hawawezi kusoma hadithi ya kingereza ya kiwango cha darasa la pili, ambapo wanafunzi wawili kati kumi sawa na asilimia 16 hawezi kusoma hadithi ya Kiswahili ya kiwango cha darasa la pili huku wanafunzi wawili kati ya kumi sawa na asiimia 23 hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za kiwango cha darasa hilo.
Twaweza-colour-logo.jpg

Uandishi wa Kiswahili ni majanga kwa wabongo wengi, kwanza kwenye jumbe fupi za SMS ndio huwa wanaharibu kabisa. Hata humu ni wachache sana huzingatia uandishi bora jinsi ipasavyo. Sijui huwa wanafunzwa vipi kwenye somo la insha.

Tatizo wengi wao hawana lugha ya pili, hawajui lugha zao za asili na Kingereza pia kiliwapa chenga, sasa unakuta Kiswahili walichoambulia ndio wamekiharibu kweli kweli, kuna yule @malisaa huniacha hoi kila anapoandika humu.
 
Kutozingatia tu,inategemea ulifunzwa na walimu gani ,wakati nasoma elimu ya msingi darasani tulikua wanafunzi hatuzidi 45...ni rahisi mwalimu kugundua wanafunzi wapi ni wazito kuelewa na kuwaelekeza...Madarasa ya siku hizi wanafunzi ni wengi mno,mwalimu anashindwa kutoa elimu kwa wote ipasavyo,kwa wale wazito kuelewa ndio inakula kwao zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uandishi wa Kiswahili ni majanga kwa wabongo wengi, kwanza kwenye jumbe fupi za SMS ndio huwa wanaharibu kabisa. Hata humu ni wachache sana huzingatia uandishi bora jinsi ipasavyo. Sijui huwa wanafunzwa vipi kwenye somo la insha.

Tatizo wengi wao hawana lugha ya pili, hawajui lugha zao za asili na Kingereza pia kiliwapa chenga, sasa unakuta Kiswahili walichoambulia ndio wamekiharibu kweli kweli, kuna yule @malisaa huniacha hoi kila anapoandika humu.
Hayo yote tisa,kumi ni kwamba watanzania bado tunajua kuandika na kuzungumza lugha yetu adhimu (kiswahili)kuliko wakenya .
 
Labda kwenye kuzungumza, hapo nakiri mnawazidi Wakenya wengi ambao wamekita kwenye kutumia lugha zao za asili na Kingereza, lakini likija suala la uandishi mpo mnaachwa nyuma. Shule nyingi za Kenya hususan zile za vijijini ndio hubobea kwenye somo la Insha.
 
Mbona hapa wengi wenu hamjui kuandika ?
 
Uandishi wa Kiswahili ni majanga kwa wabongo wengi,

Kwa wakenya ndo majanga zaidi! Wakenya wengi wanaweza kuandika vizuri kiingereza sio kiswahili!

Kila mtu huweza kuandika vizuri zaidi lugha anayoweza kuiongea! Kwa watz wengi shida kubwa inatokana na kuzoea kuongea kiswahili cha mtaani zaidi kilichojaa misimu mingi!

Ni sawa uende uingereza ukutane na mtu anaongea King's English, lazima utaona anaongea vitu vya ajabu kidogo kama hujamzoea!
 
15941332_1334468066615378_6789046678191642301_n.jpg

HALI YA ELIMU!!!! nilidhani kila siku naskia sauti kutoka huko nyanda za kusini kusema kiswahili na tz ni mapacha!!!!!:eek:

RIPOTI KAMILI YA TWAWEZA KUHUSU ELIMU YA SHULE YA MSINGI

Imeelezwa kuwa baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba hawawezi kufanya majaribio ya darasa la pili ambapo wanafunzi Wanne kati ya kumi sawa na asilimia 44 waliopo shule za Msingi za serikali hawawezi kusoma hadithi ya kingereza ya kiwango cha darasa la pili, ambapo wanafunzi wawili kati kumi sawa na asilimia 16 hawezi kusoma hadithi ya Kiswahili ya kiwango cha darasa la pili huku wanafunzi wawili kati ya kumi sawa na asiimia 23 hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za kiwango cha darasa hilo.
Twaweza-colour-logo.jpg

Iko shida kwenye elimu yetu hasa maeneo ya vijijini! Kutokana na sera ya serikali kuamuru kuwa shule ya msingi ni lazima, na sasa secondary pia imekuwa lazima kwa kila mtoto, baadhi hujikuta wanafuata mkumbo tu ili wamalize miaka yao shuleni halafu waondoke!

Hapa serikali inabidi iweke sera madhubuti za kumaliza tatizo hili! Kuweka elimu bure haitoshi!
 
Mbona hapa wengi wenu hamjui kuandika ?

Wakenya waliopo humu JF sidhani kama wanazidi ishirini, hivyo sio idadi tosha ya kutathmini uelewa wao wa lugha. Wakenya wako vizuri sana kwenye somo la insha, mwanangu wa darasa la sita huwa anaandika hadi napata raha lakini kuongea ndio huwa kunampa matatizo maana wamezoea Kiswahili cha mtaa, Kingereza na lugha ya asili.

Kwetu Kenya huwa aibu kwa mtu asiyeweza kuongea lugha yake ya asili, yaani mtu mzima mwenye umri wa miaka kama hamsini umewakuta watu wamekusanyika pamoja kijijini wanabadilishana mawazo kwa lugha ya asili halafu wewe huna lolote maana huijui, wanakuona mtumwa kabisa.
 
Huyo mwanao utakua unamuharibu maana wewe hujui kiswahili halafu unamsahihisha kiswahili uko serious kweli na usemacho hapa

Tafuta kitabu chenye hadithi ya pwagu na pwaguzi utaelewa zaidi namaanisha nini
 
Wakenya waliopo humu JF sidhani kama wanazidi ishirini, hivyo sio idadi tosha ya kutathmini uelewa wao wa lugha. Wakenya wako vizuri sana kwenye somo la insha, mwanangu wa darasa la sita huwa anaandika hadi napata raha lakini kuongea ndio huwa kunampa matatizo maana wamezoea Kiswahili cha mtaa, Kingereza na lugha ya asili.

Kwetu Kenya huwa aibu kwa mtu asiyeweza kuongea lugha yake ya asili, yaani mtu mzima mwenye umri wa miaka kama hamsini umewakuta watu wamekusanyika pamoja kijijini wanabadilishana mawazo kwa lugha ya asili halafu wewe huna lolote maana huijui, wanakuona mtumwa kabisa.
Kwa tathmini yangu nahisi wakenya mliopo humu mnaelimu ya kutosha (mna elimu ya sekondari na ku endelea) hivyo ni kipimo tosha kuweza kudadavua japo kidogo kuhusiana na wakenya na lugha ya kiswahili ,kiukweli mnajitahidi lakini bado sana kutufikia
 
Wakenya waliopo humu JF sidhani kama wanazidi ishirini, hivyo sio idadi tosha ya kutathmini uelewa wao wa lugha. Wakenya wako vizuri sana kwenye somo la insha, mwanangu wa darasa la sita huwa anaandika hadi napata raha lakini kuongea ndio huwa kunampa matatizo maana wamezoea Kiswahili cha mtaa, Kingereza na lugha ya asili.

Kwetu Kenya huwa aibu kwa mtu asiyeweza kuongea lugha yake ya asili, yaani mtu mzima mwenye umri wa miaka kama hamsini umewakuta watu wamekusanyika pamoja kijijini wanabadilishana mawazo kwa lugha ya asili halafu wewe huna lolote maana huijui, wanakuona mtumwa kabisa.

ukabila na majungu ndo vinawafanya mshikirie lugha za asili. you have no common language which unites all tribes. besides, you don't feel and have ownership on both Swahili and English. unlike bongo where people are fond of Swahili and feel the language belongs to them.
 
Hamna cha ukabila, nimesema mara nyingi kukumbatia asili yako sio ukabila, maana kuna watu huongea lugha moja lakini wanabaguana mpaka ahera. Kwa mfano Wasomali wana lugha moja, dini moja lakini hawaishi kuchinjana na kulipuana.

Kuna baadhi yenu Watanzania japo wachache hili mumelifahamu na kujirekebisha. Nilikua hapo Bongo kwenye live band usiku na marafiki zangu, halafu wimbo ukachezwa wa Saida Karoli wa Kihaya, hapo tulikua na Wahaya wakanyanyuka wote na kuchangamkia huku wakicheza mtindo fulani hivi wa kiasili. Walitufunza jinsi ya kuucheza huo wimbo kwa style yao ya Kihaya, tulifurahia sote na kuwa na wakati mzuri na hapakua na cha ukabila wala nini.

Hatimaye walitupea maneno ya huo wimbo na hadi leo najifunza kuimba, huko ndio tunaita kukumbatia asili yako na kuipenda na kujitambua, sio kuishi kama mtumwa mvaa milegezo usiyekua na asili kama wale weusi wa Marekani. Ambao hadi leo wanaishi kwa machungu na hasira maana hawajui chimbuko lao, hawajui asili yao, wamejikuta kwenye jamii inayoongea Kingereza na kulazimishwa kuishi maisha fulani ya ovyo.
 
Kitu ambacho hujui ni kuwa asilimia kubwa hapa tz mbali ya kiswahili wanaongea lugha zao na kuenzi asili zao!

Kumbuka hao wahaya uliokuwa nao ni watanzania na si wakenya! Hivyo usijaribu kuwabagua wao eti ukitoa wahaya wengine hawajui!

Labda nikusaidie, kama hujawahi kuhudhuria harusi yoyote hapa tz basi nakusihi ufanye hivyo! Huko karibia kila harusi huwa kuna segment ya kucheza nyimbo za asili! Karibia kila kabila linalokuwepo pale nyimbo zao hupigwa na watu huonyesha ufundi wao!

Kinachokutuma wewe kung'ang'ana na usemi kuwa hatuenzi makabila yetu ni kipi hasa? Labda tukusaidie maana unaonekana kutoelewa baadhi ya mambo
 
Sing'ang'anii maana ni kitu nimekiona, kaka nimeishi Tanzania na kutembelea hiyo nchi yenu sana na naijua vizuri tu, yaani naifahamu hata zaidi ya wengi wenu ambao labda kwa maisha yenu yote hamjatoka nje ya mitaa ya Dar. kazi yangu inaniwezesha kusafiri hii Afrika na kutangamana na watu wa asili mbali mbali na desturi zao, hususan ndani ya jumuia.

Wahaya ni Watanzania na hamna sehemu nimewabagua, nilisema baadhi ya Watanzania bado wanaenzi asili zao lakini wengi mumetelekeza kwa kujifanya Waswahili wa Dar. Hao Wahaya na Wanyambo huenzi sana mila na desturi zao, na hili huonekana kwa makabila yenu yanayoishi mipakani maana wanapata 'exposure' kutoka kwa mataifa majirani.

Angalia Wanyakyusa, Wanyasa, Waha, Wasukuma, Wanyambo, Wahaya, Wamaasai, Wajaluo, Wachagga, Wapare, Wadigo, Wamakonde n.k. Utaona wanadumisha sana tamaduni zao.
 
Sing'ang'anii maana ni kitu nimekiona, kaka nimeishi Tanzania na kutembelea hiyo nchi yenu sana na naijua vizuri tu, yaani naifahamu hata zaidi ya wengi wenu ambao labda kwa maisha yenu yote hamjatoka nje ya mitaa ya Dar. kazi yangu inaniwezesha kusafiri hii Afrika na kutangamana na watu wa asili mbali mbali na desturi zao, hususan ndani ya jumuia.

Wahaya ni Watanzania na hamna sehemu nimewabagua, nilisema baadhi ya Watanzania bado wanaenzi asili zao lakini wengi mumetelekeza kwa kujifanya Waswahili wa Dar.
Kitu ambacho kinakusumbua ni kimoja tu! Kazi zako zinakuwezesha kufanya kazi maeneo mengi ya mjini ambapo ni wazi kwa vijana waliozaliwa miaka ya 2000 wengi hawaoni haraka umuhimu wa lugha za asili! Hii ipo kote, hata hapo kenya ni hivyo hivyo, hawa vijana wa kuzaliwa hapa 2000 wao wanapenda kuiga kila kilicho ka mzungu!

Ndo maana wewe na umri wako huo huwezi kuongea na hao watoto sheng mkaelewana, lazima atakutoa kwenye mchuano mapema sana! Hebu sema ukweli kama mtoto wako yuko fluent kwenye kuongea kikikuyu kama wewe ulivyo!

Na hao vijana wachache niliosema ni proportion ndogo sana ambao hawatoshi kutoa ruling kuwa taifa zima hatujui kuhusu makabila yetu, la hasha!

Halafu kuna kitu huwa nakwambia mara kwa mara kuhusu maeneo ya mjini watu kutoongea lugha za asili, ni kwa sababu mijini kuna watu wa kabila nyingi sana, hivyo sio rahisi kumwongelesha mtu lugha asiyojua. Ndo maana kikawepo kiswahili ili kutuunganisha! Mabaya zaidi tz kuna makabila huwezi kuyajua kwa kutumia lafudhi kama ilivyo Kenya, hapo kwenu ukimsalimia mjaluo, mkikuyu au kelenjin maneno matatu ushajua kabila lake, akiwa wa kabila lako mnaweza kuongea bila kuambiwa!
 
Back
Top Bottom