Hanscana, bakiza hela zetu Tanzania!

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,716
Kama kuna director wa video za mziki anayejituma na kufanya kazi nzuri huyu dogo ni namba moja kwa sasa hapa bongo!
Huko nyuma walikuwepo Wananchi Video Production, wakaja Visual Lab wakawapoteza kwenye gemu, hapo katikati akatokea Kallage Pictures baadae akakimbilia Bongo movie na miaka ya hivi karibuni akavuma Nisher kwa kitambo kifupi ghafla tu ajulikani ameishia wapi na kaka yao Adam Juma naye ameamua astaafu kabisa..

Mungu mkubwa, ameibuka huyu dogo! Anajiamini, mbunifu na anajituma na anaonekana ana njaa ya kufika mbali..
Somtimes inakera kuona kila msanii sasa hivi anakimbilia SA kutengeneza video na director wa kule na kulipa pesa nyingi ambayo ingebaki nchini ingeweza kusaidia kukuza ajira kwa vijana wengine.. Lakini hakuna jinsi coz bado directors wa bongo hawathubutu kutengeneza kazi zenye level za kushindana na washindani wetu wa Afrika magharibi na Kusini! Binafsi nakuona Hanscana una potential ya kutuvusha hapa kwenye ombwe la kutokuwa na directors wabongo wanaofanya vizuri kimataifa.. Unaweza kutubakizia hela zetu hapa hapa bongo zikatengeneza ajira kwa vijana wengine..

Jambo la msingi jitahidi kuwa makini kuna wenzako wengi walikuja na tumeshawasahu!! Usitake kufanya kila kitu mwenyewe, wekeza pesa, ajiri vijana wengine wa kusaidiana nao kwenye kazi zako! Kuwa professional..
Mfano video yako iliyotoka karibuni, Arosto ya G-Nako nimecheki kwenye channel yako ya YouTube ina negative comments karibia zote.. Watu wanalalamika 'mirangi rangi' mingi yani umeremba mazingira mpaka yameboa.. Ndio maana nasema, wekeza pesa, ajiri watu usifanye kila kitu..

Lakini jambo la msingi naona potential uliyonayo, naona njaa ya mafanikio uliyo nayo! Ukikaza naamini unaweza kutuvusha na kutubakizia hela zetu nyumbani.. ALL THE BEST!
 
kinachowakimbiza south africa ni mahitaji mfano nyumba,magari,banks....kwa bongo hii huwezi tumia gari ya jeshi kwenye video ila south You can
 
BONGO urasimu, huwezi funga barabara ukashoot, huwezi kukodi mavazi ya askari mf,jeshi jwtz,polisi kwa wakati, kuna vikwazo vingi hapa BONGO ,bora waende huko huko nje HAPA tz wasanii wanathaminika wakati wa KUPATA KURA tu.
 
Wabongo kujituma ni wito alikuja Epidu wa showbiz define akazima video zote zilizotengenezwa na wabongo.... nakumbuka best video yake naipenda mpaka kesho ni Bongo fleva "chid benz ft mzee yusuf,kipindi hiki adam juma alikimbilia wapi?
 
Yap! Ni kweli lakini nadhani wenzetu kule SA industry yao imekuwa kibiashara na ya muda mrefu kidogo kuliko sisi.. So kuna vitu vingine hapa nyumbani serikali na taasisi nyingine (banks etc) bado hawajavizoea lakini kama wadau wenyewe wa entertainment industry wakiendelea kufanya lobbying lazima serikali na taasisi zitafunguka kifikra..
BONGO urasimu, huwezi funga barabara ukashoot, huwezi kukodi mavazi ya askari mf,jeshi jwtz,polisi kwa wakati, kuna vikwazo vingi hapa BONGO ,bora waende huko huko nje HAPA tz wasanii wanathaminika wakati wa KUPATA KURA tu.
 
Wabongo kujituma ni wito alikuja Epidu wa showbiz define akazima video zote zilizotengenezwa na wabongo.... nakumbuka best video yake naipenda mpaka kesho ni Bongo fleva "chid benz ft mzee yusuf,kipindi hiki adam juma alikimbilia wapi?
Hahahah!! Wabongo ndo tulivyo ushamba umetuzidi, yani hiyo drone sasa hivi imekuwa kero.. Kuna vipande vingine vya kushoot kawaida utashangaa wanatumia drone!!
Tukikuwa tutaacha, ushamba tu
 
hanscana bado ni director wa kawaida sana, labda apewe muda amaweza kuachieve, kupeleka video zetu kimataifa inahitaji juhudi zaidi ya hizi... umejiuliza kwa nini video zinashootiwa na madirector wa kigeni zimepasua anga na zinazoshutiwa na wetu zimeishia clouds, lazima kuna kitu ambacho hatuna wenyewe wanacho na wasanii wanakifuata huko huko, leo wasanii wakifanya nyimbo siriously wanaipekeka south, ya kuzugia wanampa Hanscana, bado uwekezaji kwenye video industry ni mdogo ukilinganisha na audio kwa bongo.
 
na hilo suala la Arosto watu wanafanya comparison na video aliyofanya nisher, ndio maana unaona negativity nyingi, hiyo video hata mimi karata yangu nimeitupa kwa nisher nikiringanisha na ya hanscana.

hii ni ya nisher
na hii ni ya hanscana, nafikili waweza kuona tofauti kubwa hapo
 
Well said mkuu..
 
Yeah inakuwa compared na video ya nisher but pia amezidisha marangi rangi dizaini kama video zake nyingi siku hizi anaweka mapambo mengi ya marangi rangi mpaka yanaboa hasa kwa video za rap zinakuwa zinapoteza maana.. Dizaini kama kipindi kile kallaghe naye alikuwa na tabia kila video yake akitoa utaona kuna meza inamatunda na tuna la nanasi halikosi... Hahahah!!
 
yes kwa staili yake ni vigumu kugundua ipi ni video ya hiphop na ya kuimba, kuwnzia color collection na locations, tatizo nililoliona kwenye arosto ni kama nililoliona kwenye nyimbo ya Sugu na nyimbo ya Darasa, Nisher anajitahidi sana kuitengeneza location inayoenda na mahadhi ya wimbo
 
Nisher namuelewa sana ila sijui ndio kisa mtoto wa kishua hana njaa maana hataki kukaza kabisa anafanya biashara kibishoo.. Ila angekomaa na gemu ni bonge la kichwa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom