Ufalme wa Hanscana kama Video Director umefikia mwisho- Amekuwa mwenye hofu sana sasa hivi

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
19,617
34,062
Tasnia ya utengenezaji wa video za wasanii wa Bongo fleva imeanza kitambo sana.

Kumekuwa na Directors wengi lakini mapinduzi ya video yamekuwa yakifanywa na Directors ili kuanzisha either trend mpya au Directors wenyewe kulazimika kukua baada ya wasanii kutaka video zenye ubora.

Kuna wakati Adam Juma ( Next Level ) alifanya mapinduzi makubwa sana kwenye hii tasnia lakini ghafla akatokea Nisher ( kijana wa Arusha )

Ujio wa Nisher kwenye tasnia uliwafanya wasanii wengi kufunga safari kuelekea Arusha kwaajili ya video.

Uwepo wa Nisher ndio uliomzalisha Hanscana na Khalfan.

Zaidi ya asilimia 80 ya video za wasanii wakubwa bongo zimekuwa zikifanywa na Hanscana kwa hapa Tanzania.

Fast foward sasa hivi, kumekuwa na Directors kibao wanaofanya vizuri kiasi kwamba choices zimekuwa nyingi.

Kuna Ivan, Elvis, Kenny, Msafiri, etc

Na kibaya zaidi wasanii wengine wamekuwa wakianzisha kama ilivyo kwa studio zao wenyewe, kampuni zao za video shooting.

1- Wasafi wana Zoom Extra

2- Kondegang ( tetesi wanamiliki Redshot )

Na hakuna asiyejua kuwa hawa ndio wasanii wenye kazi nyingi za video na malipo yasiyo na shaka.

Hali hii naona imesababisha Hanscana apate "Mhaho" kutokana ushindani uliojitokeza. Na asipojiangalia atapotea kama Adam Juma halafu ajifanye kastaafu🤣

Sasa hivi Hanscana amekuwa anaanzisha migogoro na wasanii isiyo na sababu, kitu ambacho kinaonekana ni PANIC ya ushindani anaoupata.

Kama hataendelea kujifua, atakuwa wa kawaida sana maana kwasasa kuna vijana wako moto sana.

1622361328556.png

Ushauri wako ni mzuri lakini ingekuwa ni vizuri ungempa private kuliko hapa jamiiforum.
 
Ni kawaida iyo hata audio producers yanawakuta sana ayo wap mr t touch. So unapopata gap km ivo unafanya kweli mida km hii unakuwa unachekea tumboni
 
Back
Top Bottom