Handbag ya Madam

kila binadamu na hulka yake hivyo basi busara inaitajika ktk swala hili na wala siyo kukurupuka
 
ipo hivi,sio wanaume tu,kila mtu anapokuwa ana wasiwasi na mwenzake hufanya ufukunyuku wake kwa namna anayoona yeye itamfaa kuthibitisha wasiwasi alionao juu ya mwenzake,mme wako kachagua kupitia kwenye pochi.

kama hauna madudu yako binafsi mwache even for thousands years mpaka atakapokuwa na imani nawe tena!kwani kwenye pochi yako kuna kitu mmeo akiona utakwazika?

kama unachepukaga pembeni na hutaki mmeo ajue basi mzuie utabambwa bure,jamaa anajua anachokifanya.kama ulikuwa hujui nikuambie tu wadada huacha alama nyingi za usaliti ktk pochi mfano handkerchief iliyotumika ktk majambo,bikini za hatari ambazo mtu hawezi kuvaa akienda kazini bali ktk game,ky-kuna kesi moja ilikuwa humu inazungumzia mambo ya ky,cheni ya kiunoni ambayo mdada humvalia mumewe ktk special days umeenda umeivaa huko umerudi umeisahau ktk pochi inampa jamaa clue kuna jambo linaendelea,na mambo lukuki(ninyi wadada mnayajua zaidi) ambayo jamaa akikuta humo atapata hint.
 
khaaaaaaaaaaaaaaaaaa wanaume wengine wakoje jamani? au anasilika ya udokozi?

sasa wewe wala usijali sometimes wanaume wa namna hiyo inabidi na wewe uwe bandidu...

akirudi tu mpige search, kwenye gari, wallet yake simu yake mkague mifukoni, nakwambia mara 3 tu ataacha mwenyewe
 

Hiyo red inahusika sana
 

Kwa hoja yako Kambaku hapo kuna kaukweli
 
Kwa hoja yako Kambaku hapo kuna kaukweli

Umeona eeenh? Haina haja kujisikia vibaya kama mwenzio akikagua pochi yako, mfukoni kwako au handbag yako, akiona kitu haelewi si anakuuliza na unamwambia tu? Sioni ubaya wowote kukagua, hata kama anakuamini au hakuamini ni haki yake kukagua tu. Kwanza tusiite kukagua ni kuangalia
 

Nadhani hapa Naima anazungumzia kukagua kwa siri na si kukagua maana hata password za emial na FB kampa.......swala ni kwanini anakagua kwa siri????
 
Nadhani hapa Naima anazungumzia kukagua kwa siri na si kukagua maana hata password za emial na FB kampa.......swala ni kwanini anakagua kwa siri????

Hapo ndio anapokosea, anatakiwa awe huru tu kila wakati kuangalia hata akiwepo mwenyewe Naima.

Hivi ni nini unadhania unaweza ukakiona kwenye pochi ya mke kama humuamini, pesa za ziada isiyo na maelezo? Kaganda ka iliyotumika? risiti ya guest au nini? Ni kujitafutia mapresha yasio sababu tu
 
HAKUNA TATIZO LOLOTE NDIO HOBBY YAO JAMANI , ACHENI WAPEKUE ROHO ZAO ZI RIDHIKE. Nina uhakika wakishajificha akipekua akamaliza na wewe hujamuona anajiona bingwaaaa, raha mustarehe, muache mmeo afurahie bana. Si umeona ulivyomsema amenuna?
 
Wewe shukuru anakagua handbag yako wenzio huwa wanaambiwa "wewe mama nani hii hebu njoo hapa" anakuvua nguo na anachukua tochi anachungulia ndani kuona kama kuna kitu kimefanyika..ushauri wangu: siku moja weka "lady pepeta" kwenye handbag yako.
 
ah wee ndio hapo ulipokosea kumwambia...wewe kama huna lolote la kuficha mwache tuu apekue kwa raha zake itafika sehemu atachoka tuu
 
Huyo lazima atakuwa ana tabia ya wizi (udokozi)
 
Amsterdam nimecheka sana hapo red daaah!
 
Last edited by a moderator:
Pole N. Ni bora akague na kuondoka kuliko akuibie. Kuna mtu mmoja yeye alimsachi mkewe akitafuta vito vyake vya thamani na akaviiba akenda kuuza na kugawia wanawake mahawara ili awaonyeshe kuwa ana hela. Mkewe alivyostuka ikabidi ahamishe vitu afungie sandukuni tena kwa kofuli na akahamishia chumba cha wageni lile sanduku. Kumbe mwanaume yule akatafuta tena vile vitu vya thamani hakuvipata na siku moja alipoona sanduku lina kofulu basi akasubiri usiku wamelala akaamka na akaenda kuvunja lile kofuli la sanduku na kuiba vile vito vya mke wake pamoja na vitu vya thamani. Kesi hii ilitua kwangu na kwa tathmini ya haraka haraka ilionekana alichukua vitu vya zaidi ya milion 60 vya huyu mkewe. Nilisuluhisha but kwa kweli hadi ninapoandika hapa ile ndoa ni gumzo. Hakuna amani kabisa na mke alikuwa ni mama wa familia kwa kujitoa sana kumsaidia mume kwa kuwa mume ni the so called wafanyabiashara wasio na ofisi mujini!!!

Ni jambo la fedheha kumkagua mwenzako hasa kama mwenzi huyo hana tabia za kutia wasiwasi. Na mbaya zaidi kumwibia!!! Yaani hadi leo nikikumbuka kisa hiki huwa natema mate kisikumbe kizazi changu. Mume kumuibia mke ni laana ambayo haina kipimo, mbaya sana.
 
Hao ndo wanaume ambao ukinunua nguo mpya atakumind,mkiwa mnatoka ukipendeza sana anaghairi msitoke
ila saa nyingine anasababu zake za msingi trust me kuna vitu anahisi juu yako anafanyia uchunguzi
sasa mpe suprise nunua kadi ya ai lavu yuu my husband
kisha piga saini "nakupenda mume wangu nimetaka kukusuprise na nilijua hii kadi utaikuta huku"
love you kisses
 

hahahahahaha yaani umeongea mzaha wenye ukweli 100%. Umemaliza kila kitu na hiyo ndio dawa
 
Unajua nivigumu sana kushauri au kutoa hukumu,endapo kama umesikiliza upande mmoja tu!unajua huyo bwana anahofu fulani juu yako kukagua hbag yako kama mkewe sio mbaya chamsingi hunabudi kumuuliza huwaana tafiti nn? Ushauri wangu achana na mitandao ya vijana fb kwani yaweza kuvunja ndoa yako kama unayo jmf haina shida.kumbuka hakuna dwanaume asie na wivu naasiena hofu juu ya mwenza wake hasa kama anampenda kwa dhati.jaribu kujua nn tatizo hofu yake lake.pia inaekana wewe unakwenda na wakati kuzidi mmewako. Pia umri wake na wako kama ana 50yrs na wewe 28 to 30yrs mvumilie huo ndio wivu wa kizee.
 
ni tabia mbaya mi binafsi siipendi.mi naona huyo mumeo hajiamini. nakumbuka kuna siku nilikua naongea na dada mmoja ye akasema mume wake huwa akiamua anamkagua hadi PICHU na sehemu za siri. kha ni ujinga tu.

ongea nae umwambie kuwa hupendi hii tabia.
 

yap ni kweli maybe mume ana wasiwasi na nyendo zako,but alipaswa kukuuliza ajue ni nini tatizo kuliko mabo ya kuviziana kama mwizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…