mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,306
- 6,514
Ahlan wasaala....
Mbetini,
Kwanza nakushukuru kwa kuileta picha hii hadharani.
Mimi ndiye mtu wa kwanza kuiona picha hii nje ya wenyewe.
Hii picha nilipewa na watoto wa Sheikh Abdallah Chaurembo
katika miaka ya 1980 na mimi nnilifanya mipango ipatikane nakala
yenye ubora na hilo lilifanyika.
Picha hii ilipigwa 1956 shambani kwa Sheikh Abdallah Chaurembo
Mtoni Dar es Salaam.
Ukoo wa Chaurembo una kawaida ya kufanya hawli kila mwaka na hii
inaendelea hadi leo
Katika hawali ya mwaka ule Mwalimu Nyerere alialikwa.
Pamoja na Nyerere kuna watu wengi maarufu katika picha hiyo.
Nyerere amekaa katika ya Liwali Ahmed Saleh kushoto na Sheikh
Bilal Mshoro kulia.
Yupo Rajab Diwani, Liwali Ahmed Saleh, Sheikh Bilal Mshoro
kutoka Tabora, Sheikh Ramadhani Abbas, Saleh Muhsin huyu alikuwa
TANU kisha akatoka pamoja na Zuberi Mtemvu kuunda Tanganyika
African Congress (ANC) mwaka wa 1958 kufuatia Uchaguzi wa Kura Tatu,
katika watoto waliokaa chini yuko Said Mahfoudh mmoja wa vijana wa
kwanza kuingia Chuo Kikuucha Dar es Salaam katika miaka ya awali ya
1960.
Hii picha ilipotea kwa miaka zaid ya 20 hata wenyewe akina Chaurembo
wakawa hawana nakala ya picha hii.
Nimefurahi kuiona tena hii picha.
Alhamdulilah.
Nimeiweka picha hii katika blog yangu:
Mohamed Said: KUTOKA JF: HAKUNA PICHA INAYOELEZA HISTORIA YA WAISLAM NA MWALIMU NYERERE KAMA HII
CC: Yericko Nyerere