Hamza Aziz na karabai za misikiti ya Kariakoo 1940s

sasa unalalamika lalamika umeme unakatika,kwani mnashindwa kununua jenereta?
Lukubuzo...
Hapana sijalalamika...

Nimeeleza fikra zangu hunirudisha nyuma kufikiria misikiti ya Kariakoo ilivyokuwa wakati umeme ulipokuwa bado pale umeme unapokatika hivi sasa.
 
Historia nzuri... Umenifanya nifahamu wanini mtaa wa kwa Azizi Alli.... Je waweza fahamu huyu mzee wakidigo alifika Dsm mwaka gani? Na elimu yake ya engineer wa majengo alisomea wapi?
Kajembejr,
Aziz Ali amekuja Dar es Salaam mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.

Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizokuwa akifanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi akaajiri mafundi.

Kwa hakika jina lake hasa ni Ali Kidonyo.

Hili Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.

Yeye alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa muda hadi atakapoweza.

Nyumbani kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.

Ndipo wakamwita "Aziz" yaani "Mpenzi." Ikawa wakimtaja jina wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali."

Kidonyo jina hili la kwao Tanga likafa kabisa.
Aziz Ali alikuwa mcha Mungu sana.

Alikataa kumwanzisha shule mwanae mkubwa Waziri maarufu kwa jina la Dossa hadi ahitimu Qur'an.

Hii ikapelekea Dossa kuanza shule darasa la kwanza akiwa na miaka 14 akawa darasa moja na Abbas Sykes mdogo wa tatu kwa rafiki yake Abdulwahid Sykes.
 
kaka taa ya kandili ya nini msikitini wakati msikiti unapangaboi?

Hata mimi nampenda Mzee Mohamed kwa historia zake za jiji la Dar Es Salaam lakini tatizo lake kubwa ni udini,historia zake zinakuwa za kuwaenzi watu ambao ni wa dini ya Kiislam na huu ni ubaguzi ambao hata katika maandishi ya vitabu vitukufu yanapinga,sisi sote ni waja wa mwenyezi Mungu,hakuna aliyezaliwa Muislamu au Mkristo,hizi dini tunarithi tu kutoka kwa wazazi kwa hiyo sio dhambi kuwa mkiristo au mwislamu au usie na dini.Tunataka huyu mzee aongelee maisha na historia ya Dar Es Salaam bila kuegamia upande mmoja,najua atasingizia kuwa ah wakazi wengi wa Dar Es Salaan na mikoa ya pwani toka enzi hizo wengi wamekuwa Waislamu,swali je unapoongelea mambo ya maisha ya jiji la Dar Es Salaam lazima uislamu uingizwe ?ni sawa na kusema basi tunapoongelea kwa mfano London au Washington lazima tuingize ukristo au makanisa badala ya kuzungumzia kwa mfano reli za chini zilivyojengwa au watu walivyokuwa wanateseka.Mzee Mohamed kweli ni nguli wa historia na simulizi na hata uandishi wake ni wa kutukuka unaposema unapata raha lakini angekuwa kama marehemu Shaabani Robert.
Mfianchi,
Hii hofu ya kuogopa Uislam katika historia ya Tanganyika imewapa shida wengi sana na hadi leo wapo wanaotaabika wanaponisoma.

Lakini tufanye nini na hii ndiyo historia yenyewe?
Hatuwezi kuifuta.
 
Kidudu,
Hapana katika dunia yangu uongo ni mfano wa gharika.

Ikijulikana kama mimi ni muongo na maisha yangu kama mtafiti ndiyo itakuwa
mwisho wake.

Yote ninayoandika ni kweli na ikiwa kuna mahali unahisi nasema uongo niulize
nikupe ushahidi wa kauli yangu.
Mkuu, wewe na Yeriko mn tabia inayofanana, kwa maana mnasoma vitu halafu mnafanya presentation kwa hisia zenu za Udini, Yeriko akitetea Ukiristo na wewe ukitetea Uislamu.

Hii ndiyo maana yenu kubwa na mmeshindwa kabisa kuwa Neutral kitu ambacho ni kibaya kuliko Gharika.
 
Ahsante kwa historia hii, ninaomba kufahamu kuhusu msikiti wa kwa Mtoro pale kariakoo? Je ni mmoja wapo wa misikiti kongwe? Na ulijulikana kwa jina gani enzi hizo?
 
Mzee Aziz Mungu ampumzishe salama. Amen. Alikuwa muungwana na mkweli. Na aliithamini kazi yake. Tusimuhusishe na mambo asiyohusika....Unafiki
 
Ahsante kwa historia hii, ninaomba kufahamu kuhusu msikiti wa kwa Mtoro pale kariakoo? Je ni mmoja wapo wa misikiti kongwe? Na ulijulikana kwa jina gani enzi hizo?
Adverse,
Misikiti yote Kariakoo ni mikongwe ila ipo ambayo ni ya zamani zaidi.

Msikti wa Mtoro unachukua jina lake kutoka kwa Sheikh Mtoro Mwinyi
Mangara
aliyeujenga.
 
Mkuu, wewe na Yeriko mn tabia inayofanana, kwa maana mnasoma vitu halafu mnafanya presentation kwa hisia zenu za Udini, Yeriko akitetea Ukiristo na wewe ukitetea Uislamu.

Hii ndiyo maana yenu kubwa na mmeshindwa kabisa kuwa Neutral kitu ambacho ni kibaya kuliko Gharika.
Kidudu,
Bahati mbaya kuwa umenifananisha na Yericko Nyerere.
Sisi ni watu tofauti kwa kila hali.

Kweli mimi natetea Uislam wala sioni aibu kukiri hilo.
Hilo la ''kusoma vitu,'' sijaelewa umekusudia nini.

Lakini mimi ninachoandika sisomi kwani hiyo ni historia ya wazee wangu
na ikiwa ni historia ya wazee wangu hiyo ni historia yangu.

Naweza kukupa mifano mingi kukuthibitishia kuwa mimi ni sehemu ya historia
hii niandikayo hapa.

Ikiwa wewe unaona kuwa historia hii ni ''udini,'' hii ni bahati mbaya sana kwako.

Kabla yangu kuna vitabu vingi tu vilivyoandika historia mathalan ya hii yangu
na vitabu hivi ni mashuhuri na ni rejea katika kusomesha historia ya Tanzania.

Unaweza kuangalia kitabu cha Augustus Nimtz, ''Islam and Politics in East
Africa, P van Bergen, ''Religion and Politics in Tanzania,'' kwa kutaja vitabu
vichache na hivi vitabu havikuandikwa na Waislam.

Bahati mbaya hayo usemayo ni hofu tu ambayo iko muda mrefu na ndiyo
sababu ya kufutwa kwa historia ya wazee wetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom