Hamu ya tendo la ndoa imepotea baada ya kupima HIV

Hamu ya tendo la ndoa imepotea baada ya kupima HIV

kadovela

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2016
Posts
471
Reaction score
679
Katika rukaruka za ujana nishawahi kutembea na wanawake ambao kuna watu wanawahisi ni waathirika wa HIV, hii kitu ilinifanya nijihisi mfu ninaetembea na nikawa muoga sana kwenda kupima, lakini katika kipindi hicho chote utendaji wangu katika lile tendo ulikuwa mzuri japo nilikuwa nahisi kama nawaambukiza mabinti wa watu bila hatia maana mimi si mfuasi wa condom.

Zoezi la kutoa damu kwa mtu muhimu kwangu lilinifanya nisiwe na namna ya kukwepa kupima, baada ya kupima na kugundulika mzima nikatoa damu kwa mtu muhimu, lakini ile hali ya kujua ni salama imenifanya kuwa na hofu na kufanya mapenzi kiasi cha kukosa hamu kabisa.

Wataalamu wa saikolojia na wenye uzoefu juu ya hali hii naomba msaada wa kujinasua katika hili maana hata mpenzi wangu kaanza kunihisi vibaya.
 
Oa mkuu..utulie na wako maisha yatakuwa mazuri tu..
 
katika rukaruka za ujana nishawahi kutembea na wanawake ambao kuna watu wanawahisi ni waathirika wa HIV, hii kitu ilinifanya nijihisi mfu ninaetembea na nikawa muoga sana kwenda kupima, lakini katika kipindi hicho chote utendaji wangu katika lile tendo ulikuwa mzuri japo nilikuwa nahisi kama nawaambukiza mabinti wa watu bila hatia maana mimi si mfuasi wa condom. zoezi la kutoa damu kwa mtu muhimu kwangu lilinifanya nisiwe na namna ya kukwepa kupima, baada ya kupima na kugundulika mzima nikatoa damu kwa mtu muhimu, lakini ile hali ya kujua ni salama imenifanya kuwa na hofu na kufanya mapenzi kiasi cha kukosa hamu kabisa, wataalamu wa saikolojia na wenye uzoefu juu ya hali hii naomba msaada wa kujinasua katika hili maana hata mpenzi wangu kaanza kunihisi vibaya.
Ukimwi sio kivuli kiasi kwamba kila mtu awe nao
 
Endelea na hali hiyo hiyo!itakunusuru na mengi
 
Kwaiyo unatafuta hamu ya kungonoka ili uupate au sio coz kama umepona sasa c ndo utulie
 
Kwaiyo unatafuta hamu ya kungonoka ili uupate au sio coz kama umepona sasa c ndo utulie
hapana ila kukosa hamu kabisa nalo nitatizo na kwanini linikumbe baada ya kujua usalama wa afya?
 
Sasa hivi unapougopa tulia, ukirukaruka tuu ndo unakupata...hahaaaah ogopa sana misambwanda
 
Katika rukaruka za ujana nishawahi kutembea na wanawake ambao kuna watu wanawahisi ni waathirika wa HIV, hii kitu ilinifanya nijihisi mfu ninaetembea na nikawa muoga sana kwenda kupima, lakini katika kipindi hicho chote utendaji wangu katika lile tendo ulikuwa mzuri japo nilikuwa nahisi kama nawaambukiza mabinti wa watu bila hatia maana mimi si mfuasi wa condom.

Zoezi la kutoa damu kwa mtu muhimu kwangu lilinifanya nisiwe na namna ya kukwepa kupima, baada ya kupima na kugundulika mzima nikatoa damu kwa mtu muhimu, lakini ile hali ya kujua ni salama imenifanya kuwa na hofu na kufanya mapenzi kiasi cha kukosa hamu kabisa.

Wataalamu wa saikolojia na wenye uzoefu juu ya hali hii naomba msaada wa kujinasua katika hili maana hata mpenzi wangu kaanza kunihisi vibaya.
Anakuhisi vibaya ki vipi? mbona na mie naanza kukuhisi vibaya? lol........ kwanza mshukuru sana mwenyezi mungu kwakukuepusha na hilo na Inshallah akuepushe hili na jengine,akupe moyo wauwoga usiwe una fanya vitu vibaya akupe moyo wakuoa uwe na mwezako uoe..
 
Back
Top Bottom