GE2025 Hamisi Kigwangalla ashauri kesi ya Tundu Lissu ifutwe

GE2025 Hamisi Kigwangalla ashauri kesi ya Tundu Lissu ifutwe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Nzega Vijijini (CCM) Dkt. Hamis Kigwangalla ameshauri kutafutwa kwa namna itakayowezesha kufutwa kwa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu

Katika machapisho yake ya septemba 30.2025 aliyoweka kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram Kigwangalla ameandika, "Tena kama mkifikiria vizuri zaidi mtatekeleza dira ya Mama Samia Suluhu Hassan ya 4R's (Maridhiano, Mabadiliko, Kujenga upya na uvumilivu) na slogan yake ya 'Kazi na Utu' kwa kutafuta kifungu kitakachoisaidia Mahakama kuifuta kesi inayomkabili ndugu Tundu Antipas Mughwai Lissu"

Katika hatua nyingine, Kigwangalla ambeye pia ni Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii amesisitiza kutopuuzwa kwa sauti za wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini

“Watanzania wamechimba mkwara (kuhusu madai ya kutaka kuandamana na kuzuia uchaguzi), sote tunajua hawawezi kuandamana, lakini sauti yao imesikika, wamesema na tumewasikia, tusiwapuuze, tutoe uongozi, tuunganishe Taifa, tujenge" -Kigwangalla
1759296434060.png
 
ngoja nicheke mana simu yangu sio smart siwezi kweka emoji.baada ya jaribio la sarakas zote.kaondolewa kwenye mchezo,kaona haitoshi akatengeneza mabango ya mahaba aise wakaja wakulungwa wakayatoa mabango .

saiz kanyoosha mikono
 
Mtu akiwa nje ya mfumo wa ccm ndo anapata akili timamu ila ukiwa ndani ya ccm unakuwa zwazwa
Uking'ata na kupuliza kwa namna hiyo, wakuu wanakupa attention, wanakujadili na kama utabahatika utalamba teuzi.

Ila ukiliwa kichwa na ukawa kimya, huna wafuasi, na wewe mwenyewe husemisemi basi ndo bye bye.
 
Kesi iende mpaka mwisho na maza atimbe pale mahakamani

Lissu alishasema hataki huruma ya mahakama ila haki itendeke.
 
Back
Top Bottom